Kazini kwangu ninaowasimamia hawanisikilizi, naomba ushauri

Kazini kwangu ninaowasimamia hawanisikilizi, naomba ushauri

Brow ukiingia nyumba ya mtu wewe hupaswi kupaza sauti jaribu kuangalia life style yao then jaribu kusoma mchezo wagawe then kila mtu atajua wewe una cheo gani
Soma ameandika imekuwa ni miezi miwili yupo kazini means tayari hapo mazingira keshayasoma.
Kitu kingine uongozi ni kipaji si kila mtu ana karama ya kuongoza watu.

Ulimwengu mwingine: wapo watu ili uwaongoze inabidi uwende kujiweka kinga au madawa, kuna watu wkongwe makazini huwa wanatingisha wageni, sasa hutumia kujiamini kwa madawa pia,hivyo ili uwamudu watu sometimes haya huhitajika, ndio maana kuna sehemu watu wapo tu miaka nenda rudi ofisini hawafukuzwi, ni wachawi
 
Mimi sio naowatimua mkuu viongozi wenyewe wanataka niendenao hivyo
Wewe jenga nao urafiki kiongozi bora huwasikiliza anaowaongoza kwa hio wasikilize kisha chambua kipi pumba na kipi mchele katika 10 utapata hata 5/6 wanaoendana na wewe kazi itakua na wepesi kwa hio jenga nao tu urafiki wasikilize katika kile wanachofanya kisha waonyeshe namna ya kufanya kwa wepesi au angalia ni nyenzo gani wanahitaji kurahisisha kazi mfano pa kukata na msumeno si sahihi kutumia panga maana utatumia nguvu nyingi kwa hio hao kuna kitu kinawakwamisha kwenye utendaji wasikilize kisha peleka changamoto zao kwenye uongozi waone wanavyowasaidia
 
Watanzania wengi tunapenda kufanya vitu kisela sela business as usual. Mimi katika shughli zangu ni watanzania wachache ambao huwa nashughulika nao kwa sababu nilishajaribu sana yani hawachukulii kazi kwa uzito mwisho huwa nashughulika na wakenya na watanzania wachache ambao wanafanya kazi kwa moyo.
Sahihi Watanzania huwa wana usela mavi wa kipuuzi sana kwenye kazi hasa mkizoeana, hawawi professional kabisa.
 
Tafuta sample kama wawili hivi timua then fanya replacement yao haraka iwezekanavyo..hao wengine wataingiwa na uoga
Haya mawazo ya kipumbavu
Nyie ndiyo mnateka na kuuwa watu ili wengine waingie uoga wasijiunge upinzan
Unafikir umetatua tatizo
 
Kazi imekushinda,huna management skills.Bosi atakushusha cheo muda si mchache.Not every body is born to be a leader
 
Wewe jenga nao urafiki kiongozi bora huwasikiliza anaowaongoza kwa hio wasikilize kisha chambua kipi pumba na kipi mchele katika 10 utapata hata 5/6 wanaoendana na wewe kazi itakua na wepesi kwa hio jenga nao tu urafiki wasikilize katika kile wanachofanya kisha waonyeshe namna ya kufanya kwa wepesi au angalia ni nyenzo gani wanahitaji kurahisisha kazi mfano pa kukata na msumeno si sahihi kutumia panga maana utatumia nguvu nyingi kwa hio hao kuna kitu kinawakwamisha kwenye utendaji wasikilize kisha peleka changamoto zao kwenye uongozi waone wanavyowasaidia
Ni wafanya usafi vifaa vipo mkuu
 
Nina wiki mbili toka niajiriwe katika kiwanda kimoja hapa mtwara. Mimi ni msimamizi wa vibarua wa wanaofanya usafi.

Changamoto iliyopo ni kua nikiwapa maelekezo kua usafi ufanyike katika maeneo yao wanaleta dharau, jeuri, kejeli. Wanataka niwe fea ila fea sidhan kama inafaa kazini

Majibu yao ni kua walikuepo hapa zaidi yako Leo wametimuliwa, hili jambo linanipa hofu na kutojiamini. Had hapa nishagombana na watu wawili ile tu kuwapa maelekezo wananimaindi.

Uongozi wa juu nao wananiambia nijitahidi kumalizana nao nisiwe naripoti ripot kila kitu. Nimekuja hapa kuomba ushauri jinsi ya kuitatua hii kadhia. Nahisi kuchoka.
Umeleta stori juu juu sana,na utaishia kupata ushauri wa juu juu tu ambao hauwezi kukusaidia lolote.

Ni vyema ukafungika wewe unasimamia nini,ni kampuni ama ofisi inayodili na nini.

Then hao unaowasimamia wanafanya kazi zipi na zipi na kwa mfumo upi na jee bila wewe kuwaambia hizo kazi hawafanyi au wanafanya.

Na je hao watu ni wasomi au sio wasomi,ysani level zao za elimu zikoje,na vipi wanavyoishi wao kwa wao wanaheshimiana au wanaishi kwa kukoseana adabu tu ?

Yako mambo mengi ambayo unatakiwa kufunguka hapa lakini umeyaficha labda kwa kuogopa kujulikana,ila hitopata ushauri ule ulioshiba.

Njia kuu ya kuwafanya watu wafanye unachokitaka ni kuwashawishi na uwape wanachokitaka ama uwaoneshe njia ya wao kupata wanachokitaka.
 
Ulitakiwa kujenga mahusiano mazuri nao! Wajue tabia zao shida zao,maisha yao! Then ndiyo ujue jinsi ya kuwasimamia!
Usije na mihemko na kiherehere cha kazi harafu ukaanza kuwafokea! Hawatakuelewa.
Kuna jamaa wawili nimeshazinguana nao
 
Back
Top Bottom