Kazini kwangu ninaowasimamia hawanisikilizi, naomba ushauri

Kazini kwangu ninaowasimamia hawanisikilizi, naomba ushauri

Nina wiki mbili toka niajiriwe katika kiwanda kimoja hapa mtwara. Mimi ni msimamizi wa vibarua wa wanaofanya usafi.

Changamoto iliyopo ni kua nikiwapa maelekezo kua usafi ufanyike katika maeneo yao wanaleta dharau, jeuri, kejeli. Wanataka niwe fea ila fea sidhan kama inafaa kazini

Majibu yao ni kua walikuepo hapa zaidi yako Leo wametimuliwa, hili jambo linanipa hofu na kutojiamini. Had hapa nishagombana na watu wawili ile tu kuwapa maelekezo wananimaindi.

Uongozi wa juu nao wananiambia nijitahidi kumalizana nao nisiwe naripoti ripot kila kitu. Nimekuja hapa kuomba ushauri jinsi ya kuitatua hii kadhia. Nahisi kuchoka.
Kuwa mtu wa maneno machache,usipige mkwara,for record waandikie barua ao vibarua ya insubordination nakala kwa meneja,wewe fuata taratibu watakaa sawa tu.
 
1. Wapangie ratiba ya kazi vizuri
2. Wahi mapema kazini
3. Anza majukumu yako mapema
4. Wakati wa kuwasimamia unaweza kuonyesha kufanya kazi kwa mfano
5. Usiwe Mtu wa majungu
6. Penda kusikiliza changamoto zao na kuzifanyia kazi
7. Jifanye uko pande wao kuliko wa viongozi kwamba unawapambania.
 
Back
Top Bottom