Kazini kwangu ninaowasimamia hawanisikilizi, naomba ushauri

Kazini kwangu ninaowasimamia hawanisikilizi, naomba ushauri

We ushawaonesha meno na mazoea kedekede watu kama hao ulitakiwa toka unaingia uwaoneshe heshima ila mazoea no.

Alafu jenga utaratibu wa kuwaita vikao kila mwanzo wa week na uwatengenezee passion kwenye kazi yao mfano; “Jamani usafi wa jana uongozi umependezwa nao sana nafikiri tukiendelea hivi tunaweza kupewa favour yoyote” Sometimes shiriki nao katika kufanya nao usafi ili wakuone hujikwezi bali unahitaji kazi bora, Jaribu kuwajua wote na uwe unauliza taarifa za wale waotokea kutokufika kazini kwa sababu mbalimbali na uwe unatuma salamu za pole, Hii itafanya wakuone unajali na watakupenda, Kuwa mcheshi kiasi unazungumza nao.

Badala ya kutumia maneno “Fanyeni Usafi” tumia “Tufanye usafi” Jiingize nawe kama mwenzao kimatamshi japo ufanyaji wako utakuwa wa kudonyoa donyoa ili kuwa-motivate

Hizo ni baadhi ya njia ambazo zitakufanya uwe kiongozi wa tofauti na waliokuwapo kabla, Ukiwa mzuri kwenye ku-pretend hao hao wanaweza kufanya ukapanda cheo maana watapenda kukuona ukiwa kiongozi kila mara.

Kingine Umuombe Mungu sana maana ukishatengeneza attractive kwa watu ukawa na ushawishi sana unatengeneza vita walio juu yako maana unawapa wasiwasi wa kuja kupora nafasi zao.
 
Ushauri mzur sanaa wenye kumsaidia Sana huyu junior leader.
Kikubwa azingatie ushauri wako utamfaa Sanaa
 
Ni kweli hapa kuna ujinga sana
We jamaa una matatizo,shida ni kwamba una amri unapenda amri smri,hauna ile art ya ushawishi.

Ndio maana comment ambazo unazisapoti ni zile zinazohimiza kutumia ubabe ubabe,zile zinazokutaka uwe more diplomat hauzikubali.

Sasa hiyo personity yako itakusumbua sana kuishi na watu,tatizo lako unataka kuwaamrisha watu wazima ambao wanajua kazi yao.

Wewe ni wale watu wa amri amri,sasa wenzio wa hivyo hawaogopi lolote wao ni potelea mbali.
 
Malizana nao sio kuwaripot ripot bos anaona hujui kazi we implement makato kama mtu ajafanya kazi ipasavyo akatwe kiasi inaleta ahueni we uongei sana unaweka makato,kama mtu ajaja kazini ela ya siku inalambwa, anategea inalambwa so we uongei nao unacheza na pesa zao tu, makato huchukui wew unasema una hire watu waziada kufill utendaji wao
 
Mimi sio naowatimua mkuu viongozi wenyewe wanataka niendenao hivyo
Mkuu siumesema ni vibarua maana yake kesho getini Waite vijana wengine waingie kufanya kazi yani saa kumi na mbili alfajiri wahi mapema chakua vijana wapya.
 
Wiki mbili chache sana kufanya tathmini ya uongozi.
Unahitaji muda kuwaelewa unaowaongoza ili uanze kubadili culture ya hapo kiwandani.
Kama walivyokushauri wengine itisha kikao.
Inaonekan hata hujakaa nao kikao ukawapa nini unatarajia kutoka kwao na namna ya kufikia matarajio.
Pia uelewe changamoto zao ambazo zinaweza Fanya malengo yasifikiwe uanze kuzipunguza ili zisikukwamishe.
Utawala nawaunga mkono wanapokuambia malizana nao sababu wanataka uwe mtu wa kutatua matatizo na sio kuyaripoti kwao.
Kama kila kitu utawaambia wao utakuwa na kazi Gani hapo?
Pambana tatua changamoto hiyo uongozi si lele mama.
Pia kama hujasoma management anza kupitia theory zake.
Anza na zile za udikteta ukifuatia na hizi za kisasa.
 
Nina wiki mbili toka niajiriwe katika kiwanda kimoja hapa mtwara. Mimi ni msimamizi wa vibarua wa wanaofanya usafi.

Changamoto iliyopo ni kua nikiwapa maelekezo kua usafi ufanyike katika maeneo yao wanaleta dharau, jeuri, kejeli. Wanataka niwe fea ila fea sidhan kama inafaa kazini

Majibu yao ni kua walikuepo hapa zaidi yako Leo wametimuliwa, hili jambo linanipa hofu na kutojiamini. Had hapa nishagombana na watu wawili ile tu kuwapa maelekezo wananimaindi.

Uongozi wa juu nao wananiambia nijitahidi kumalizana nao nisiwe naripoti ripot kila kitu. Nimekuja hapa kuomba ushauri jinsi ya kuitatua hii kadhia. Nahisi kuchoka.
Habari,
Ni kawaida, kwasababu wewe ni “mpya” hapo kazini, wanajaribu kukupima. Hii ni kawaida,sehemu yeyote utayo kwenda,ikiwemo hata ukiamia kwenye department mpya.

Kama kiongozi, nadhani unaweza kuwa na meeting kila hasubui,kabla ya kuanza kazi.unaweza eleza vipaumbele vya siku nzima na unaweza toa kama mtu anakuwa na nyiongeza au dukuduku kuongea. Lengo ni kuwapa picha halisi ya siku na kuwapa nafasi ya kuongea kama wanao wanaonewa.

Baada ya hapo,panga kazi kwa kila mmoja, awe anajua siku hiyo anafanya kazi au usafi sehemu gani. Husiwape kama group, gawa kazi vipande vipande.

Ukifika mwisho wa siku, unaweza kugagua,na kama haijafikia viwango, unaweza kujadili na mhusika. Tengeneza kitu kama file, ku monitor “performance “. Hii itakusaidia kupeleka malalamiko yako kwa management maana utakuwa na evidence.

Husikimbilie kushitaki kila siku, management watajua “hauna” sifa ya kuwa kiongozi. Sifa moja ya kuwa kiongozi ni uwezo wa kutumia mbinu mbali mbali ikiwemo “siasa” kushawishi watu kufanya kazi. Ukiwa na mentality ya kuwa wewe ni “boss” lazima wakusikiliza, sidhani kama utapata matokeo mazuri
 
Back
Top Bottom