Anhaa, kutokana na umri na ugeni na mambo yote. Kwa kuanzia jiweke kama mjumbe zaidi wa kazi wanazotakiwa kufanya.
Basi fanya kama kujiondoa, mfano badala ya kutoa amri kama wewe, basi fanya kama kuiwasilisha. Mfano msemo wa jeshini wa "KAZI ZA WATU" . Wapangie kazi kama vile zimetoka kwenye MFUMO/UTAWALA etc.
Ukienda kikao na wakubwa unarudi unawasilisha kwamba, ajenda mojawapo ilikuwa tumejisahau sana kufyeka majani sehemu x. Ile sehemu tutaigawana ndani ya siku tatu iwe saaaafi.
Chukua inspiration hata kanisani mtu anaweza kuleta wazo lake na akaliwasilisha kama ni Roho wa bwana Amemtuma. Matokeo yake yeye na wazo lake linaheshimiwa kutokana na mamlaka yaliyo nyuma ya hilo wazo. "Roho wa Bwana amenituma tukawatembelee wagonjwa jumatano"
Kingine nao uongozi uangalie namna ya kuweka bonus, ambayo wewe ndio unaamua nani apate kiasi gani cha hiyo bonus kulingana na utendaji kazi wake kama inawezekana. Kama haiwezekani stiki na njia ya kwanza mr
nipo online