Nchi hii inawajinga wengi sana nandio maana tunachelewa kwa sababu ya kuwa na watu vilaza kama baadhi ya wachangiaji hapo juu.
Magu anakubalika 24/7 na wananchi kwa mamilioni, na wengi hawana access JF.
Nyerere alikuwa muoga kwa mabeberu Magu hakumuogopa mtuyoyote linaokuja swala la maslah ya nchi hata ccm wenzake wanajua.
..Nyerere hakuwa muoga kwa mabeberu.
..hebu hakiki vyanzo vyako vya taarifa.
..Nyerere aling'ara kimataifa kwa sababu alikuwa akipambana na mabeberu kwa hoja.
..Kwa upande mwingine Magufuli alikuwa akijifungia hapa Tanzania akiogopa kushindanisha hoja zake na zile za mabeberu.
..Nyerere alishatimua wanadiplomasia wa Marekani. Alivunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza na kukataa misaada yao. Alivunja mahusiano na Ujerumani magharibi. Alivunja uhusiano wa kibalozi na Israel.
..Kubwa kuliko yote Nyerere ali-support vita ya ukombozi kusini mwa Afrika dhidi ya mabeberu. Particularly ali-support kijeshi wapiganaji wa Frelimo ya Msumbiji dhidi ya wakoloni wa Kireno ambao ni wanachama wa NATO.
..Kwa upande mwingine hebu tuelezeni Magufuli alifanya jambo gani dhidi ya mabeberu ambalo Mwalimu Nyerere hakuwa na uwezo nalo.
..Mwalimu alikuwa akiwakemea mabeberu kwa ukosefu wao wa maadili.
..Magufuli alikuwa akikemewa na mabeberu kwa dhuluma na ukatili aliokuwa akiwafanyia wananchi wake mwenyewe.
Nguruvi3, Kalamu1