..Nyerere hakuwa muoga kwa mabeberu.
..hebu hakiki vyanzo vyako vya taarifa.
..Nyerere aling'ara kimataifa kwa sababu alikuwa akipambana na mabeberu kwa hoja.
..Kwa upande mwingine Magufuli alikuwa akijifungia hapa Tanzania akiogopa kushindanisha hoja zake na zile za mabeberu.
..Nyerere alishatimua wanadiplomasia wa Marekani. Alivunja uhusiano wa kibalozi na Uingereza na kukataa misaada yao. Alivunja mahusiano na Ujerumani magharibi. Alivunja uhusiano wa kibalozi na Israel.
..Kubwa kuliko yote Nyerere ali-support vita ya ukombozi kusini mwa Afrika dhidi ya mabeberu. Particularly ali-support kijeshi wapiganaji wa Frelimo ya Msumbiji dhidi ya wakoloni wa Kireno ambao ni wanachama wa NATO.
..Kwa upande mwingine hebu tuelezeni Magufuli alifanya jambo gani dhidi ya mabeberu ambalo Mwalimu Nyerere hakuwa na uwezo nalo.
..Mwalimu alikuwa akiwakemea mabeberu kwa ukosefu wao wa maadili.
..Magufuli alikuwa akikemewa na mabeberu kwa dhuluma na ukatili aliokuwa akiwafanyia wananchi wake mwenyewe.
Nguruvi3,
Kalamu1
Tatizo la watu wajinga kama huyo uliyemfundisha hapo juu, hata baada ya kufundishwa hivyo hawarudi na kukupa shukrani za kuwaelimisha.
Kwa hiyo, hawa siyo wajinga, ni WAPUMBAVU.
Magufuli alikuwa ni mtu wa misifa.
Kila alilofanya kwa kugezea, alifanya ili apate sifa yeye.
Na katika hayo aliyokuwa akigezea, kwa vile moyo wake haukuwa na nia ya kweli ya kuyafanya, aliishia kuyafanya kwa makosa.
Magufuli hakuwa na uwezo wowote wa ushawishi. Hakuweza kujadili jambo likaeleweka na watu, kwa hiyo badala ya ushawishi mabavu ndio ikawa nyenzo ya kulazimisha anayoyataka yeye yawe kwa mabavu.
Elimu ya Magufuli ilikuwa ni ya kukariri, hakuwa na uwezo wa kutumia elimu yake kwa manufaa ya nchi yake. Kwa kutafuta misifa mingi alikariri takwimu za barabara, hata wingi wa samaki majini..., huo ulikuwa ni uigizaji, ulimbukeni.
Linganisha elimu hiyo na elimu iliyompa uwezo Mwalimu kujadili jambo na mtu na kulieleza kwa ufasaha kabisa kwamba linaeleweka na mtu yeyote, hata awe na elimu ndogo.
Kiujumla, kama viongozi, Magufuli alikuwa ni mtu mwenye tabia mbaya. Mtu asiyekuwa na utu kwa watu wengine ambao hawamshuhudu au hawampi sifa. Ndiyo maana akina Lissu waliishia kutaka kuondoshwa duniani na akina Ben hata haijulikani ilikuwaje.
Lakini pengine la msingi zaidi kuliko yote katika kutofautisha, Magufuli alikuwa hataki kufuata taratibu, hakuheshimu taratibu kabisa. Ndiyo maana yeye kuvunja sheria au katiba kwake halikuwa jambo la kusita au kumzuia asifanye alichotaka kufanya.
Mtu yeyote, na hasa kiongozi asiyependa kufuata taratibu zilizowekwa na jamii, huyo hawezi kuwa kiongozi mzuri. Ni kama jambazi tu!.
Ndiyo maana alitafuta na kuteua watu wenye tabia za ajabiu ajabu sana ili wamfanyie uchafu wake kinyume na sheria.