Keir Starmer kuwa Waziri Mkuu mpya wa Uingereza huku Rishi Sunak akikubali kushindwa

Uchaguzi wa Uingereza hata siuelewi. Ndani ya mwezi umetangazwa na kufanyika. Nasikia waziri mkuu anaweza kuitisha uchaguzi muda wowote ilimradi tu ufanyike mara moja ndani ya miaka mitano. Anaeelewa vizuri uchaguzi wa UK anijuze.
 
Yalioikumbuka uingereza sio mapungufu kidogo
Unadhani ma PM wote watano walikua na mapungufu madogo madogo kama usemavyo
Kiukweli UK kuna majambo hayapo sawa haiwezekani nchi kama UK ndani ya miaka 7 sijui 8 wawe washabadilisha PM zaidi ya watatu kisa jambo dogo tuuu
 
Chama chao ilikua inasubiriwa elwction tu,
 
Nimemkumbuka

Liz Truss: I'm a fighter, not a quitter


Nabado akafurushwa


Sema wabunge wa huku naonaga wanapiga sana kelele

View: https://www.bbc.com/news/av/uk-politics-63313539
 
Asante kwa ufafanuzi huu
 
Ulaya na kwingineko zinaingia Serikali ambazo zinapinga uhamiaji holela na dini za kigeni.
 
Safi Sana
 
Sema kwa viongozi sio wananchi.
Viongozi wanaojitambua ama taasisi ama serikali inayojitambua.
Kama wananchi hawajitambui uhangaike kuiba kura ili iweje!?
Wananchi ndio chanzo!! Sasa hata unapoiba kura hakuna wanaloweza fanya, unategemea nini??! Viongozi wa kizungu wanajitambua toka utotoni, na hawana njaa, AFrica shida ni njaa na ubinafsi wetu.
 
Fuatilia vizuri siasa za UK kabla ya kutoa maoni yako. Nahisi hapa unatumia mihemko zaidi kuliko hali halisi ilivyo. Huyo Sunak alikuwa Waziri Mkuu wa tatu kipindi cha miaka mitano.
Ni vizuri ukijikita kwenye kutoa maoni yako. Masuala ya kuhisi mimi natumia mihemko zaidi, yanaingiaje hapa? Kama unazifahamu vizuri hizo siasa za Uingereza, ziweke hapa jukwaani na tutakuelewa vizuri tu. Huo ni mtazamo wangu tu.
 
Urusi ni noma sana, wamemuondoa madarakani waziri mkuu wa Uingereza huku wakimuweka wanayemtaka
 
hajatoka kwasababu ya kuipiga vita urusi bali kwasababu Rish hakuwa strong hivyo wanahitaj mtu atakae irudisha heshima ya UK na kulinda tamaduni zao UK
 
Wananchi ndio chanzo!! Sasa hata unapoiba kura hakuna wanaloweza fanya, unategemea nini??! Viongozi wa kizungu wanajitambua toka utotoni, na hawana njaa, AFrica shida ni njaa na ubinafsi wetu.
Hehehehe.
Umeongea vise versa mkuu.
Mtu keshakufa,unaweza kuwa na hofu naye!?
Viongozi wetu hawajielewi ndio maana wanatumia udanganyifu kukaa madarakani kwasababu uroho wao wa madaraka umewatoa akili.
Sio kwamba hawajui na hawaoni kama raia wanajua utumbo wanaofanya,wanaona na wanajua,ila kwa kutokuelewa kwao wanatumia nguvu kuwatuliza hao raia.
Viongozi wa wenzetu wanajielewa ndio maana wanafanya maamuzi sahihi kwa ustawi wao na raia wao.
Shida ni viongozi sio raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…