Kelele zimepungua redioni. Elimu haitaki kelele

Kelele zimepungua redioni. Elimu haitaki kelele

Kenya ilitokea kesi ya kijana kujifanya mwanasheria akashinda kesi kadhaa. Na huyu atunukiwe uanasheria?

Kuna vijana walikamatwa Mloganzila na Mhimbili wakijifanya madaktari. Na hawa watunukiwe udaktari?

Kuna vijana walikamatwa hapa Tz wakijifanya wanajeshi. Watunukiwe uanajeshi?

Juzi waziri akiwa Njombe akakutana na kijana aliyejitambulisha kama mhandisi na mkurugenzi wa kampuni ya ujenzi. Ikagundulika siyo ila ni supervisor wa kampuni. Atunukiwe uhandisi na ukurugenzi?

Zembwela na wenzake walijifanya waandishi wa habari. Hawa ndiyo watunukiwe uandishi au siyo?
unachanganya mambo mjuba, angalia mukhtadha. Kina zembwela hawakujifanya ni waandishi, ilitokea tu wakawa wanaimudu kazi hiyo kutokana na kuwa ndani ya media. Usilinganishe na udaktari na unesi au kazi yoyote ile mtu hawezi kufanya kama hana code zake. Kama media waliwaamini na kuwapa kazi basi waliona wanamudu kufanya kazi hiyo, achana na matapeli wanaojiingiza kwenye taaluma
 
Vipindi vilikua vinamilikiwa na watangazaji au na Vituo husika?
Kwanini hao watangazaji wanaogopa sana shule?
Tangu mwaka 2016 ni miaka 9 imepita wakiambiwa wasio na sifa za kielimu wasome wengine wakasoma wengine wametulia tuli wakiona serikali inafanya mzaha.
Mtu kama Shigongo ametoka Lasaba mpaka Bachelor katika kipindi hicho wakati wengine wakiona haina haja sasa utekelezaji unapoanza wa kanuni na sheria husika kuna wakumlaumu na umepewa kujiandaa kwa miaka 9?
Shigongo Hana cheti cha form four na degree yake kaipata kupitia offer iliyotolewa na TCU na vyuo vyote vilimkatalia Ila akaenda Tumaini.
 
unachanganya mambo mjuba, angalia mukhtadha. Kina zembwela hawakujifanya ni waandishi, ilitokea tu wakawa wanaimudu kazi hiyo kutokana na kuwa ndani ya media. Usilinganishe na udaktari na unesi au kazi yoyote ile mtu hawezi kufanya kama hana code zake. Kama media waliwaamini na kuwapa kazi basi waliona wanamudu kufanya kazi hiyo, achana na matapeli wanaojiingiza kwenye taaluma

Ubunifu gani ambao unauzungumzia hapo .

Vipindi vyote havimilikiwi na watangazaji Ila vinamilikiwa na Radio husika na ukipeleka wazo lako katika radio husika utapewa malipo kadhaa .

Maulidi kitenge ule ubunifu wake wa kusoma magazeti anapanda katika meza huo ndo unaita ubunifu?.
 
Huu ni ujinga, siwezi kuanzisha vipindi na maudhui yake halafu nitolewe kazini kisa sina elimu wakati vipindi vyangu vinapendwa na watu wengi na media zingine zimeiga ubunifu wangu. Haki yangu ipo wapi hapa?
Una akili ndogo halafu unalazimisha kuongelea vitu vilivyokuzidi kimo, Sasa tukuulize kila mtangazaji anaanzisha tu anachokipenda halafu akiamka tu anaenda kurusha matangazo? Kuna wakuu wa vipindi na miongoni mwa makubaliano ni pamoja na mtangazaji mwenye wazo zuri kulifikisha kwa wakuu wa maudhui na wasimamizi wa vipindi, wakikubali kipindi kinakuwa mali ya redio husika.
Pili kuna kundi la watu ambao wanaleta wazo la kurusha mada au vipindi maalumu na hao wanalipia na ndio watakuwa wawasilishaji, mfano Daktari au hata Mwalimu akaamua kuomba muda arushe maudhui yake, huyo akimaliza anaondoka na kipindi chake na wakat wa kipindi anasimamiwa na mtangazaji wa zamu.
Sasa wewe unataka kila mtu anayejua kuongea akawe mtangazaji, unaonaje kila muongeaji mzuri awe mwanasheria? Kila anayejua gari aruhusiwe tu kuendesha? Maana ya kuwa na taaluma fulani ni takwa la kisheria na ikitokea kuna kipaji basi anapewa muda fulani kupata ithibati kwa kuhudhuria mafunzo.
Kuna siku utakuja useme kila anayejua kupigana ngumi wote wakawe wanajeshi na polisi bila kupitia mafunzo.
 
hivi we unafikiri kwenda chuoni huku unafanya kazi ni rahisi? Inahitajika rasilimali fedha na muda wa kwenda chuoni. Kwanza mshahara wa kutosha kulipia gharama za chuo na upate muda wa kutulia chuoni. Una familia inakutegemea, muajiri gani atakugharamia uende chuoni wakati anajua wewe ni product inayotakiwa kwingine? Kujigharamia mwenyewe chuoni ni shughuli pevu. Huu mpango ungeanza na watangazaji wapya, vijana ambao bado wanasomeshwa na wazazi wao
Kujisomesha kuliwahi kumgharimu Misanya Bingi kipindi hiko.

Lakini kuna Open University wangesoma huko.
 
We ni mpuuzi na huijui taaluma ya habari na utangazaji. Hii dhana ya kudhani kuwa msomi ndio utafanya kazi kwa weledi na ubunifu mnaitoa wapi? Ungesikitika kwa kuondolewa magwiji hao wa utangazaji ungeonekana wa maana. Watu walibuni vipindi murua mpaka vikawa vinafuatiliwa na watu wengi wameondoka huku majina ya vipindi waliovianzisha yakitumika bila kubadilishwa na maudhui yake nayo yabadilishwe. Ingekuwa nchi zilizoendelea hao watangazaji wangedai fidia kwa kile walichokianzisha na kuki brand wanaondoka huku vipindi vyao vikitangazwa na wengine. Hawa wanaonekana wana sifa na ithibati nao wanzishe na kubuni vipindi vyao tena wasiige maudhui tuone tofauti na ubora wao, shame on you
Ile ni mali miliki/haki miliki ya kampuni sio ya mtangazaji.

Unapoajiriwa kwenye kampuni/taasisi moja ya masharti ya kimkataba ni kwamba chochote kinachozalishwa / kuanzishwa itahesabija kama mali ya kampuni na sio ya mtu binafsi.
 
We ni mpuuzi na huijui taaluma ya habari na utangazaji. Hii dhana ya kudhani kuwa msomi ndio utafanya kazi kwa weledi na ubunifu mnaitoa wapi? Ungesikitika kwa kuondolewa magwiji hao wa utangazaji ungeonekana wa maana. Watu walibuni vipindi murua mpaka vikawa vinafuatiliwa na watu wengi wameondoka huku majina ya vipindi waliovianzisha yakitumika bila kubadilishwa na maudhui yake nayo yabadilishwe. Ingekuwa nchi zilizoendelea hao watangazaji wangedai fidia kwa kile walichokianzisha na kuki brand wanaondoka huku vipindi vyao vikitangazwa na wengine. Hawa wanaonekana wana sifa na ithibati nao wanzishe na kubuni vipindi vyao tena wasiige maudhui tuone tofauti na ubora wao, shame on you
Fani ya uandishi na utangazaji imeharibika sana Tanzania kwa sababu ya hawa vilaza. Ila mimi nataka zichukuliwe njia ya kisayansi zaidi za kurekebisha mambo kuliko kupiga marufuku hao vilaza. Kuhusu kufuatiliwa na watu wengi kwa nchi kama Tanzania siyo kigezo cha kuwa ni wazuri. Hata pornography ina wafuatiliaji wabongo wengi sana... hata viroba vilikuwa vinanywewa vijana wengi sana.....
 
Nadhani hujui unachokiongelea; Moja Media ime evolve na wanahabari wale uliowazoea sasa hivi kuna citizen journalism; hata wewe hapo unaweza ukawa mwanahabari so long as una habari na unaweza kuiwakilisha vizuri ili watu wapende kukusikiliza (audience); Kinachoondelea ni kutaka /urahisi wa kufanya centralization na kwa watawala kuweza kutumia media hizi kwa urahisi kama propanda machines..., ila ni vigumu sababu sasa hivi ni contents / information on demand..., yaani hata kama wewe unasubiri kusikiliza magazeti kwenye radio ni mmoja kati ya kundi linaloendelea kupungua..., sasa hivi hata hizo habari mtu angeziweka kwenye podcast yake ili wewe uweze kuzipata kila unapotaka kwa mtu unayemtaka....

You can not stop the waves..., just learn how to Surf..., Media imekuwa a Competitive Jungle, ila kwa wenye jicho la tatu tunaona uwezekano wa nchi kama yetu kitengo hiki kikazidi kubanwa wameanza na elimu (which is not bad) na watakuja na vigezo vyao vya maadili which will be subjective na kuweza kuwafunga midomo...

1753505339103.png
 
Leo nimefungulia ile redio ambayo jina lake linafanana na sabuni, nikitaka kusikiliza habari za magazetini.

Kiukweli nimeenjoy sana, kelele zile za Nipasheee🗣️🗣️🗣️ mwanga wa jamiii🗣️🗣️ hazikuwepo kabisa. Habari zilikuwa kwenye mtiririko mzuri sanaaa.

Nilichojifunza ni kuwa :- makelele mengi yanasababishwa na elimu ndogo. Watu wasio na elimu ili wahisi wanaeleweka lazima wapayuke.😂😂😂
Unamaanisha Mr. Chumvi, Ndimu, Minyama na kale kengine sijui kenyewe kanaitwaje? Kwani wameenda wapi?
 
You can not stop the waves..., just learn how to Surf..., Media imekuwa a Competitive Jungle, ila kwa wenye jicho la tatu tunaona uwezekano wa nchi kama yetu kitengo hiki kikazidi kubanwa wameanza na elimu (which is not bad) na watakuja na vigezo vyao vya maadili which will be subjective na kuweza kuwafunga midomo...

​
Hii ya kubanwa ndiyo lengo kuu.
 
Hii ya kubanwa ndiyo lengo kuu.
Ila ndio hivyo sasa hivi kila mwenye smartphone ni mwandishi enzi za habari kutoka kwenye source moja duniani zimekwisha na sio huku tu kule Mpuuzi Trump anaendeleza mwendo wa kuwa Sue Media Houses left, right and centre na wengine wanaokubaliana nae kuhakikisha wanapata deals nzuri za mergers...., Ni uchawa all along wordwide...., Nadhani ndoto zangu za hiki hapa chini kutokea bado sana muda wake.... (If anything sasa hivi ndio imekuwa worse)

 
Nchi inapenda ujinga. Sasa hivi hata vipindi vya mijadala ya kiuchumi na siasa hakuna. Ni umbea, ushoga, michezo full stop
Inakera sana mkuu, yani watu wamekuwa wa hovyo mpaka kupitiliza..

Pia wapitie huku kwenye Channel za YouTube kuna wa Pumbavu wengi sana natoa taarifa zisizo na maadili kabisa.
 
Back
Top Bottom