Kelele zimepungua redioni. Elimu haitaki kelele

Kelele zimepungua redioni. Elimu haitaki kelele

Hata mimi naweza kua mwandishi. Ila ni nani ataniwajibisha nikiyavurugua humo ndani kama bodi ya wahusika hainijui kisa sina vyeti?

Daktari anatakiwa kua na leseni na ajiandikishe MCT. Akivuruga wanazuia leseni, mimi nikiyavuruga unaniwajibisha wapi?
we andika habari kama unajua habari inaandikwaje, peleka kwenye media house kwa mhariri, huyu mhariri ni mwandishi mwandamizi ataipitia kazi yako kama inafaa kuchapishwa gazetini au ni ya kutupwa jalalani. Ikichapwa utalipwa ila kwenda kwenye redio na tv kutangaza hapo pana ugumu labda kama unaomba kazi na itabidi ufanyiwe majaribio kwenda hewani. Ni ngumu huwezi kwenda kutafua kazi wakati wenyewe hawajatangaza kutaka watangazaji
 
Niambieni nirudi kusikiliza redio. Niliacha kabisa, maana ilikuwa makelele tuuu asubuhi mpaka jioni
 
Hata mimi naweza kua mwandishi. Ila ni nani ataniwajibisha nikiyavurugua humo ndani kama bodi ya wahusika hainijui kisa sina vyeti?

Daktari anatakiwa kua na leseni na ajiandikishe MCT. Akivuruga wanazuia leseni, mimi nikiyavuruga unaniwajibisha wapi?
MCT? MCT ipi mjuba? unamaanisha Medical Council of Tanzania au Media Council of Tanzania?
 
we andika habari kama unajua habari inaandikwaje, peleka kwenye media house kwa mhariri, huyu mhariri ni mwandishi mwandamizi ataipitia kazi yako kama inafaa kuchapishwa gazetini au ni ya kutupwa jalalani. Ikichapwa utalipwa ila kwenda kwenye redio na tv kutangaza hapo pana ugumu labda kama unaomba kazi na itabidi ufanyiwe majaribio kwenda hewani. Ni ngumu huwezi kwenda kutafua kazi wakati wenyewe hawajatangaza kutaka watangazaji
Huu ushauri wagewe ambao hawakwenda darasani na wana hamu ya kuendelea kua wanahabari.
 
hivi we unafikiri kwenda chuoni huku unafanya kazi ni rahisi? Inahitajika rasilimali fedha na muda wa kwenda chuoni. Kwanza mshahara wa kutosha kulipia gharama za chuo na upate muda wa kutulia chuoni. Una familia inakutegemea, muajiri gani atakugharamia uende chuoni wakati anajua wewe ni product inayotakiwa kwingine? Kujigharamia mwenyewe chuoni ni shughuli pevu. Huu mpango ungeanza na watangazaji wapya, vijana ambao bado wanasomeshwa na wazazi wao
Fact
 
Leo nimefungulia ile redio ambayo jina lake linafanana na sabuni, nikitaka kusikiliza habari za magazetini.

Kiukweli nimeenjoy sana, kelele zile za Nipasheee🗣️🗣️🗣️ mwanga wa jamiii🗣️🗣️ hazikuwepo kabisa. Habari zilikuwa kwenye mtiririko mzuri sanaaa.

Nilichojifunza ni kuwa :- makelele mengi yanasababishwa na elimu ndogo. Watu wasio na elimu ili wahisi wanaeleweka lazima wapayuke.😂😂😂


mrangi
 
We ni mpuuzi na huijui taaluma ya habari na utangazaji. Hii dhana ya kudhani kuwa msomi ndio utafanya kazi kwa weledi na ubunifu mnaitoa wapi? Ungesikitika kwa kuondolewa magwiji hao wa utangazaji ungeonekana wa maana. Watu walibuni vipindi murua mpaka vikawa vinafuatiliwa na watu wengi wameondoka huku majina ya vipindi waliovianzisha yakitumika bila kubadilishwa na maudhui yake nayo yabadilishwe. Ingekuwa nchi zilizoendelea hao watangazaji wangedai fidia kwa kile walichokianzisha na kuki brand wanaondoka huku vipindi vyao vikitangazwa na wengine. Hawa wanaonekana wana sifa na ithibati nao wanzishe na kubuni vipindi vyao tena wasiige maudhui tuone tofauti na ubora wao, shame on you
achsa ujinga we zembwela nini ,Jina la kipindi ni mali ya taasisi na sio mfanyakazi .
 
kule kila mtu anathaminiwa kipaji chake mjuba, habari za vyeti ni kwenye siasa tu. Hata mfinyanga chungu ana hakimiliki kule huwezi kubuni kitu kiigwe na wengine wanufaike halafu familia yako ife njaa. Hivi vyeti ni kwa wajinga tu
Acha ufala sio Kila sehem inahitaji elimu pekee Kuna sehemu zinahitaji elimu kipaji ni kama passion tu

Wachukue watu wenye vipaji vya kuimba wape ulecture chuo wafundishe mziki

Bila shaka unaonekana hauna elimu na kama unayo basi hauna akili
 
Huu ushauri wagewe ambao hawakwenda darasani na wana hamu ya kuendelea kua wanahabari.
darasa ni muhimu mjuba, watu huanzia from nowhere, kama we ulianzia darasani huyo ni wewe, endelea kujivunia degree yako uliyoisotea kabla ya kuanza kazi
 
Leo nimefungulia ile redio ambayo jina lake linafanana na sabuni, nikitaka kusikiliza habari za magazetini.

Kiukweli nimeenjoy sana, kelele zile za Nipasheee🗣️🗣️🗣️ mwanga wa jamiii🗣️🗣️ hazikuwepo kabisa. Habari zilikuwa kwenye mtiririko mzuri sanaaa.

Nilichojifunza ni kuwa :- makelele mengi yanasababishwa na elimu ndogo. Watu wasio na elimu ili wahisi wanaeleweka lazima wapayuke.😂😂😂
Mbona haya hapa nimeyakuta yapo? Hii ilikuwa ya 22 hours ago maanake ilikuwa ya jana!
Screenshot_20250726-123338_Instagram.jpg
 
Leo nimefungulia ile redio ambayo jina lake linafanana na sabuni, nikitaka kusikiliza habari za magazetini.

Kiukweli nimeenjoy sana, kelele zile za Nipasheee🗣️🗣️🗣️ mwanga wa jamiii🗣️🗣️ hazikuwepo kabisa. Habari zilikuwa kwenye mtiririko mzuri sanaaa.

Nilichojifunza ni kuwa :- makelele mengi yanasababishwa na elimu ndogo. Watu wasio na elimu ili wahisi wanaeleweka lazima wapayuke.😂😂😂
Ila wewe Jamaaa weweee! Nimecheka sana!
 
Taaluma iliingiliwa sana. Ukiwa maarufu tu, unapewa kipindi
Mkuu wale wachambuzi wa muchezo kwani na wao bado wapo?
Kama na wao walitakiwa watimuliwe wakatafute kazi za kufanya na nafasi zao zizibwe na wacha mbuzi waliocheza mpira kwa ngazi ya kuanzia ligi Daraja la kwanza.
 
Una akili ndogo halafu unalazimisha kuongelea vitu vilivyokuzidi kimo, Sasa tukuulize kila mtangazaji anaanzisha tu anachokipenda halafu akiamka tu anaenda kurusha matangazo? Kuna wakuu wa vipindi na miongoni mwa makubaliano ni pamoja na mtangazaji mwenye wazo zuri kulifikisha kwa wakuu wa maudhui na wasimamizi wa vipindi, wakikubali kipindi kinakuwa mali ya redio husika.
Pili kuna kundi la watu ambao wanaleta wazo la kurusha mada au vipindi maalumu na hao wanalipia na ndio watakuwa wawasilishaji, mfano Daktari au hata Mwalimu akaamua kuomba muda arushe maudhui yake, huyo akimaliza anaondoka na kipindi chake na wakat wa kipindi anasimamiwa na mtangazaji wa zamu.
Sasa wewe unataka kila mtu anayejua kuongea akawe mtangazaji, unaonaje kila muongeaji mzuri awe mwanasheria? Kila anayejua gari aruhusiwe tu kuendesha? Maana ya kuwa na taaluma fulani ni takwa la kisheria na ikitokea kuna kipaji basi anapewa muda fulani kupata ithibati kwa kuhudhuria mafunzo.
Kuna siku utakuja useme kila anayejua kupigana ngumi wote wakawe wanajeshi na polisi bila kupitia mafunzo.
Mkuu huyu anaongea vitu ambavyo havijui ansongea kwa hisia na siyo kwa ufahamu wa jambo na taratibu zake kisheria.
 
Wewe ni Zembwela nini?? Mwandishi wa habari sio kipaji, ni taaluma.

Siku hizi iliaminishwa kuwa uandishi wa habari ni kipaji. Kila anayeweza kuongea anataka kuwa muandishi wa habari. Ikawajaza maMC na wasanii. Watu wenye weledi wakakaa nje.
Mkuu ata Michezo ni taaluma ndiyo maana nchi zilizoendelea kuna vyuo vya michezo mtoto anaingia darasani, na kwa walimu wa michezo na waamuzi wa michezo wana kozi zao zinazofundishwa na Wataalam, ndiyo maana ili uruhusiwe mfano kufundisha timu ya inayoshirki mashindano yaki mataifa lazima uwe na cherish na leseni daraja A, Serikali yetu ilichelewa sana yani ata Chama cha mpira wa miguu Tanzania iliwashinda kwa kufata sheria kwa Walimu wa timu na wahamuzi.
 
Kwakweli ni jambo la kushukuru.

Weledi ndo kila kitu.
 
Back
Top Bottom