Kelele zimepungua redioni. Elimu haitaki kelele

Kuna yule kiazi mwenye kidoti alikuwa ananiboa sana, kupayuka na kuropoka tu
 
unachanganya mambo mjuba, angalia mukhtadha. Kina zembwela hawakujifanya ni waandishi, ilitokea tu wakawa wanaimudu kazi hiyo kutokana na kuwa ndani ya media. Usilinganishe na udaktari na unesi au kazi yoyote ile mtu hawezi kufanya kama hana code zake. Kama media waliwaamini na kuwapa kazi basi waliona wanamudu kufanya kazi hiyo, achana na matapeli wanaojiingiza kwenye taaluma
 
Shigongo Hana cheti cha form four na degree yake kaipata kupitia offer iliyotolewa na TCU na vyuo vyote vilimkatalia Ila akaenda Tumaini.
 

Ubunifu gani ambao unauzungumzia hapo .

Vipindi vyote havimilikiwi na watangazaji Ila vinamilikiwa na Radio husika na ukipeleka wazo lako katika radio husika utapewa malipo kadhaa .

Maulidi kitenge ule ubunifu wake wa kusoma magazeti anapanda katika meza huo ndo unaita ubunifu?.
 
Huu ni ujinga, siwezi kuanzisha vipindi na maudhui yake halafu nitolewe kazini kisa sina elimu wakati vipindi vyangu vinapendwa na watu wengi na media zingine zimeiga ubunifu wangu. Haki yangu ipo wapi hapa?
Una akili ndogo halafu unalazimisha kuongelea vitu vilivyokuzidi kimo, Sasa tukuulize kila mtangazaji anaanzisha tu anachokipenda halafu akiamka tu anaenda kurusha matangazo? Kuna wakuu wa vipindi na miongoni mwa makubaliano ni pamoja na mtangazaji mwenye wazo zuri kulifikisha kwa wakuu wa maudhui na wasimamizi wa vipindi, wakikubali kipindi kinakuwa mali ya redio husika.
Pili kuna kundi la watu ambao wanaleta wazo la kurusha mada au vipindi maalumu na hao wanalipia na ndio watakuwa wawasilishaji, mfano Daktari au hata Mwalimu akaamua kuomba muda arushe maudhui yake, huyo akimaliza anaondoka na kipindi chake na wakat wa kipindi anasimamiwa na mtangazaji wa zamu.
Sasa wewe unataka kila mtu anayejua kuongea akawe mtangazaji, unaonaje kila muongeaji mzuri awe mwanasheria? Kila anayejua gari aruhusiwe tu kuendesha? Maana ya kuwa na taaluma fulani ni takwa la kisheria na ikitokea kuna kipaji basi anapewa muda fulani kupata ithibati kwa kuhudhuria mafunzo.
Kuna siku utakuja useme kila anayejua kupigana ngumi wote wakawe wanajeshi na polisi bila kupitia mafunzo.
 
Kujisomesha kuliwahi kumgharimu Misanya Bingi kipindi hiko.

Lakini kuna Open University wangesoma huko.
 
Ile ni mali miliki/haki miliki ya kampuni sio ya mtangazaji.

Unapoajiriwa kwenye kampuni/taasisi moja ya masharti ya kimkataba ni kwamba chochote kinachozalishwa / kuanzishwa itahesabija kama mali ya kampuni na sio ya mtu binafsi.
 
Fani ya uandishi na utangazaji imeharibika sana Tanzania kwa sababu ya hawa vilaza. Ila mimi nataka zichukuliwe njia ya kisayansi zaidi za kurekebisha mambo kuliko kupiga marufuku hao vilaza. Kuhusu kufuatiliwa na watu wengi kwa nchi kama Tanzania siyo kigezo cha kuwa ni wazuri. Hata pornography ina wafuatiliaji wabongo wengi sana... hata viroba vilikuwa vinanywewa vijana wengi sana.....
 
Nadhani hujui unachokiongelea; Moja Media ime evolve na wanahabari wale uliowazoea sasa hivi kuna citizen journalism; hata wewe hapo unaweza ukawa mwanahabari so long as una habari na unaweza kuiwakilisha vizuri ili watu wapende kukusikiliza (audience); Kinachoondelea ni kutaka /urahisi wa kufanya centralization na kwa watawala kuweza kutumia media hizi kwa urahisi kama propanda machines..., ila ni vigumu sababu sasa hivi ni contents / information on demand..., yaani hata kama wewe unasubiri kusikiliza magazeti kwenye radio ni mmoja kati ya kundi linaloendelea kupungua..., sasa hivi hata hizo habari mtu angeziweka kwenye podcast yake ili wewe uweze kuzipata kila unapotaka kwa mtu unayemtaka....

You can not stop the waves..., just learn how to Surf..., Media imekuwa a Competitive Jungle, ila kwa wenye jicho la tatu tunaona uwezekano wa nchi kama yetu kitengo hiki kikazidi kubanwa wameanza na elimu (which is not bad) na watakuja na vigezo vyao vya maadili which will be subjective na kuweza kuwafunga midomo...

​
 
Unamaanisha Mr. Chumvi, Ndimu, Minyama na kale kengine sijui kenyewe kanaitwaje? Kwani wameenda wapi?
 
Hii ya kubanwa ndiyo lengo kuu.
 
Hii ya kubanwa ndiyo lengo kuu.
Ila ndio hivyo sasa hivi kila mwenye smartphone ni mwandishi enzi za habari kutoka kwenye source moja duniani zimekwisha na sio huku tu kule Mpuuzi Trump anaendeleza mwendo wa kuwa Sue Media Houses left, right and centre na wengine wanaokubaliana nae kuhakikisha wanapata deals nzuri za mergers...., Ni uchawa all along wordwide...., Nadhani ndoto zangu za hiki hapa chini kutokea bado sana muda wake.... (If anything sasa hivi ndio imekuwa worse)

 
Nchi inapenda ujinga. Sasa hivi hata vipindi vya mijadala ya kiuchumi na siasa hakuna. Ni umbea, ushoga, michezo full stop
Inakera sana mkuu, yani watu wamekuwa wa hovyo mpaka kupitiliza..

Pia wapitie huku kwenye Channel za YouTube kuna wa Pumbavu wengi sana natoa taarifa zisizo na maadili kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…