Kelele zimepungua redioni. Elimu haitaki kelele

Wameondoa vijiwe vya wapiga kelele,machawa,wafitini wasengenyaji .......nk serekali ilichelewa sana
 
Shida nini brother kitenge ? Ithibati imekukosea sana kaka
 
Sasa walikuwa wanategemea kazi hiyo kwa maisha yao kwanini hawakuweza kujiendeleza kielemu na kusomea fani hizo hata kwa ngazi ya diploma tu..?
Kuna watu hawana vigezo hata vya kusoma certificate tu. Zile D4 hawana. Ni darasa la 7 tu. Wanatakiwa waanzie veta au Open university kufanya foundation course. Kwasababu ya umaarufu wao waliona aibu
 
Wewe ni Zembwela nini?? Mwandishi wa habari sio kipaji, ni taaluma.

Siku hizi iliaminishwa kuwa uandishi wa habari ni kipaji. Kila anayeweza kuongea anataka kuwa muandishi wa habari. Ikawajaza maMC na wasanii. Watu wenye weledi wakakaa nje.
 
Unaweza kuwa mtangazaji mzuri tu unaweza kuongea na kujenga hoja kwa umakini hadharani.

Uwe creative na idea za kutosha.
Maana hata huku nje vigezo sio elimu ya juu bali akili yako tu.
Ila elimu kama Una degree in broadcasting au journalism ni nzuri zaidi.

Kwa huko walizidi sana utoto
Lazima wakasome sasa
 
Mkuu unaundugu na maulidi kitenge?πŸ˜‚πŸ˜‚ maana umechafukwa sio pow
 
Sasa Media zitaanza kuongozwa KISOMI wanajazajaza wabwatukaji redioni jitu linabwatuka tu kwani umesikia hatukusikiii Mzee vipi?
Tunasubiri tuone hao wasomi wataleta mapinduzi gani.

Kila kitu kina ubunifu ndipo plus elimu kinamature, mfano dunia yote muwe wote mmesoma nasema wote haya nini kinafuata?.

Yaani tuseme ukweli lazima kuwe na pande mbili, ndiyo maana Almasi hajasoma na kapindua meza na akaajili wasomi.

Huo ndiyo upande wa pili sasa.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚huu mfano umemaliza kila kitu.

Hawa waandishi wauongo ni wanajamii wenzetu. Tunajua maisha yao nje ya media. Watoto zetu pia wanajua maisha ya hawa watu. Inafika muda mtoto anakwambia hataki shule anataka kuwa muandishi, tena anakupa mfano wa waandishi maarufu kama Swebe na Zembwela. Anakwambia hawakwenda shule na wamekuwa waandish wenye mafanikio
 
Tujiulize Watanzania wanataka kusikia nini, angalia hata serch history zao mitandaoni ni umbeya na xxx, Sasa hivyo vipindi serious watasikiliza?
Mbona watu wengi wanatumia mafundi Maiko kujenga maghorofa na serikali ikigundua huwa inasimamisha ujenzi na wakati mwingine faini zinahusika pia.

Watu wangeruhusiwa tu kujenga maghorofa kwasababu wanatamani??!!
 
NIPASHEEEEEEEEE .....
NI MWANGA WA JAMIII.

NDIYOOOO .

Kwenye daladala walikua wanawapenda kweli. Full kelele.
 
Elimu inayozungumzwa hapo sio ya biology na chemistry. Ni uandishi wa habari. Wakajue miiko ya fani husika.

Mfano tukisema dereva fulani hana elimu, hatuzungumzii degree na diploma. Inazungumzwa cheti cha udereva.

Duniani huwez kuepuka shule. Hata ukiokota taka, ukiwa mbobevu ukafungua na ofisi rasmi lazima uende NEMC kupigwa msasa ili usije kuokota chemicals hatari
 
Sasa kama hajasomea huyu si anajiingiza kwenye taaluma au uandishi wa habari ni jalala
 
Sasa kama hajasomea huyu si anajiingiza kwenye taaluma au uandishi wa habari ni jalala
kule hawapasui moyo na mifupa mjuba, hata mimi hapa ni mwandishi na sina degree ujue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…