Kelele zimepungua redioni. Elimu haitaki kelele

Kazi nyingi mtu anaweza zifanya bila elimu husika.

Hata tukimchukua kijana wa form six mwenye division four ila tukamuacha afanye on job training na daktari baada ya muda akivaa lile koti na stethoscope akakusikiliza complains zako anaweza suggest vipimo vya kupimwa.

Huyu kijana akitibu watu watano ataanza kuona udaktari hauna maana kwakua hata yeye anaufanya. Hichi ndicho kilitokea kwenye uandishi wa habari.

Watu warudi shule. Kama unaweza unamhonga principle kazurure ukimaliza utalikuta gamba lako.
 
Umenyoosha sana maelekezo
 
kule hawapasui moyo na mifupa mjuba, hata mimi hapa ni mwandishi na sina degree ujue
Hata mimi naweza kua mwandishi. Ila ni nani ataniwajibisha nikiyavurugua humo ndani kama bodi ya wahusika hainijui kisa sina vyeti?

Daktari anatakiwa kua na leseni na ajiandikishe MCT. Akivuruga wanazuia leseni, mimi nikiyavuruga unaniwajibisha wapi?
 
Kuna mtu kama Zembwela kama atakomaliwa kweli basi itambidi ajikite kwenye uigizaji. Hawezi kuwa na spirit ya kutafuta course work DSJ
Yule huwa anaziweza sana zile stori za kitaa kuzunguka na mic - alikuwaga na kipindi fulani hivi kitaa nafikiri alikuwa clouds (sikumbuki jina la kipindi) alikuwa anakifanyia haki
 
Hahahaha.....Mwijaku bado mnaye, ana Degree yake sasa sijui mtamkataa vipi
 
Niliacha kuwasikiliza juzi kati walipoanza kuzungumza eti magereza ni taasisi inayojitegemea haiwezi kusikiliza na kutekeleza amri ya mahakama. Nikajua hapa wapo maponjoro tu hamna kitu.
Duh huyo alifika mbali 😅
 
Yule huwa anaziweza sana zile stori za kitaa kuzunguka na mic - alikuwaga na kipindi fulani hivi kitaa nafikiri alikuwa clouds (sikumbuki jina la kipindi) alikuwa anakifanyia haki
Alianzia East Africa TV miaka ya 2006 hadi 2009 huko.
 
Niliacha kuwasikiliza juzi kati walipoanza kuzungumza eti magereza ni taasisi inayojitegemea haiwezi kusikiliza na kutekeleza amri ya mahakama. Nikajua hapa wapo maponjoro tu hamna kitu.
Hahahahaa
 
Hili ni jambo la hatari sana... ipo siku tutaambiwa kumiliki simu lazima uwe na cheti cha chuo kikuu... ndio tutajua hatujui!

Walipaswa kudhibiti maudhui sio watu.

Ila nao waache tu, maana wakati wenzao wanawekwa kikaangoni, walikuwa wanachekelea sana
 
Hivi huyu member anayejiita Wakili ana akili timamu kweli? mbona anamwaga dislike kana kwamba kalazimishwa? hebu awe mstaarabu
 
😁😁 Yan hii forum yote kitenge ndo anaongelewa sana sijui kwanini aisee,
Yan kila page ni yeye tu
Kuna mambo hua hayajifichi, jamaa ni mropokaji tuu afu pointless.

Mwenzake ataongea jambo, afu yeye ataanza kulirudia jambo hilo hilo hata mara mia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…