jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 20,419
- 39,217
Huyu mzee wetu kila alipo yeye ni kuhisi tu wanatendewa uonevu na kubaguliwa wakati mimi nimekuwa na kuishi nao, ila sijawahi kusikia wala kuona wanabaguliwa maana hakuna sehemu kwenye nchi hii unapoambiwa toa cheti cha dini yako ndo uhudumiwe au huo ubaguzi uko huko tu kwenye ngazi za juu?Hakuna kuchelewa wala nini. Sehemu pakiwa na ubaguzi utajua tu. Unajua watu ambao hawana fursa ya kurekebisha uzembe waliofanya katika maisha yao wakati wa ujana au utoto huwa wanatafuta visingizio vya kuonyesha kuwa haikuwa wao bali walisababishiwa.
Unajua mtu mvivu wa kufiriki huwa anatengeneza nadharia na kuifanya kuwa ni majibu kamili. Ila ukimwambia akupe evidence utaona anavyotekenyeka na kubadili mikao.
Mimi mtaa nilipokulia kuna watu wa imani za kiislam na kikristo, tulisoma shule moja ya msingi na pia tulienda shule za sekondari tofauti ila zote zinatumia mtaala m'moja wa elimu.
Na tulipomaliza sekondari, kuna ambao walikwenda vyuo vya Tanzania, na wapo waliokwenda nje, mimi sikuwahi kuomba kusoma vyuo vya nje sababu nilikuwa muoga kuishi mbali na familia yangu.
Lakini still nilipokwenda chuo bado nilikutana na wengine na tulisoma wengine walifaulu kunizidi, wengine walikuwa viongozi serikali ya wanafunzi.
Na sasa nimemaliza elimu ya chuo nipo uraiani kupambana na uchumi ila bado nakutana na wenzangu tukiishi maisha katika hali ya ufanano.
Muda wote huu sikuwahi kufikiria kuwa kuna mfumo wa dini ambao unawabania watu baadhi wasiweze kupenya popote na kufanya maisha.
Sasa huwa nashangaa sana nikisikia kuna mtu analalamika kuwa kuna hicho kitu ambacho, mimi na wenzangu tusikione kweli.....?!
Aiseeee kuna watu sijui ni malezi waliopitia, unakuta mtu kalelewa na bibi huko tokea utotoni sasa anavyokuwa mtu mzima anaanza kutafuta wa kumdekea kama alivyodeka kwa bibi.
Maisha sio hisia, maisha ni uhalisia. Yeye sasa kama anaamini kuna udini haya akalage baho, wenzake ndio haoooo tunatafuta maisha tunajenga inchi. Fainali ni uzeeni huko.
Chiz...Mzee ilibidi uchezee ban hapa JF.kila uzi unazotoa unaleta udini sana.yani ungepewa nchi sijui ungetaka iweje
Boom...Huyu mzee wetu kila alipo yeye ni kuhisi tu wanatendewa uonevu na kubaguliwa wakati mimi nimekuwa na kuishi nao, ila sijawahi kusikia wala kuona wanabaguliwa maana hakuna sehemu kwenye nchi hii unapoambiwa toa cheti cha dini yako ndo uhudumiwe au huo ubaguzi uko huko tu kwenye ngazi za juu??
Uzalendo,Mzee elimu yako na uzoefu ulionao ni mkubwa sana
Niombe utupatie maoni yako kuhusu vikundi mbalimbali vya wanaharakati kama Alshababu au Alkaida au Boko haram ili tuweze ongeza ufahamu.
Je wanaharakati hao wanaotetea Uislamu kwanini wanapigwa vita kila kukicha?
Aksante sana
Uzalendo,
Nina mada niltoa University of Ibadan mwaka wa 2006 kuhusu ugaidi.
Naingia In Shaa Allah Maktaba kukutafutia.
Jiwe,Kulikua na haja gani ya kusema muislamu wa kwanza..acha udini acha inferiority complex..somesheni watoto.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee wangu,Sam,
Udini ni kule kueleza kuwa walikuwapo watu katika watendaji wa Wizara ambao hawakupendezewa na kuwa na Waziri na Katibu Mkuu Waislam?
Tafadhali nifahamishe.
Jiwe...Kulikua na haja gani ya kusema muislamu wa kwanza..acha udini acha inferiority complex..somesheni watoto.
#MaendeleoHayanaChama
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkaruka,Mzee wangu,
Kiongozi akiwa wa dini fulani hilo linasaidia nini ??
Uzalendo...Twaisubiri kwa hamu kubwa
Enjai...We jamaaa ni mshmba sana udini umekujaa kila siku uislam uislam. Tatizo ndugu zako wakacha elimu wakakimbilia madrasa na bahati mbaya teuzi zinaangalia elimu dunia na sio madrasa.
Mrangi,Udini udini udini
Ova
malima na kenya walipokuwa Wizara ya elimu walileta mabadiliko gani ya maana unayokumbuka ambayo unaamini yaliondoa unachoita "dhulma." Miaka nenda rudi tunajua kuwa shule nyingi za kiislamu zimekuwa zinafanya vibaya sana wakati shule nyingi za kikatoliki zikifanya vizuri sana.KENYA ABDALLAH HASSAN KATIBU MKUU WA KWANZA MUISLAM WIZARA YA ELIMU AMEFARIKI
Kenya Abdallah Hassan nimemfahamu toka utoto wangu Moshi katika miaka ya 1960.
Siku hizo mimi nikiwa shule ya msingi madarasa ya chini sana yeye alikuwa Mawenzi Secondary School.
Kenya alikwenda Makerere, Uganda nilikuja kujua baadae.
Kenya angefariki na mimi wala nisingenyanyua kalamu yangu kuandika chochote kuhusu yeye kama isingetokea mwaka wa 1987 jambo lililogusa Waislam wengi Tanzania.
Mwaka huo Prof. Kighoma Malima alichaguliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Waziri wa Elimu.
Hili lilikuwa halijapata kutokea.
Ilikuwa kama vile Rais Mwinyi amevunja mwiko alioweka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere toka uhuru mwaka wa 1961kuwa nafasi hiyo haishikwi na Muislam.
Baada ya kuwa Waziri wa Elimu Prof. Malima Rais Mwinyi akamchagua Kenya Abdallah Hassan kuwa Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.
Rais alikuwa kapiga msumari wa moto juu ya kidonda.
Wizara ilichafuka na wahariri wa magazeti wakawa wanachonga penseli zao ziandike vizuri.
Kuna watendaji ndani ya wizara waliona kama vile sasa bwawa limeingia luba itakuwa tabu kuogelea kwa raha na salama.
Yaliyotokea sasa ni historia.
Prof. Malima aliondolewa kwenye Wizara ya Elimu baada ya kujadiliwa Dodoma.
Hayo ndiyo yaliyofanya mimi hii leo nimkumbuke kaka yangu Kenya Hassan.
Mola amghufirie dhambi zake na amlipe Pepo ya Firdaus.
Amin.
View attachment 1735030
Kichuguu,malima na kenya walipokuwa Wizara ya elimu walileta mabadiliko gani ya maana unayokumbuka ambayo unaamini yaliondoa unachoita "dhulma." Miaka nenda rudi tunajua kuwa shule nyingi za kiislamu zimekuwa zinafanya vibaya sana wakati shule nyingi za kikatoliki zikifanya vizuri sana.
Tatizo siyo wizara wala rais bali tatizo ni mfumo wa ufundishaji. Nakumbuka marehemu Dr Omar Juma wakati akiwa makamu wa rais aliwahi kuhutubia kikao fulani cha maulidi kwa kuhimiza waislamu kupeleka watoto shule na kutumia muda wa ziada kwenye masomo ya dini badala ya kutumia muda mwingi kwenye masomo ya dini na kuifanya shule kama kitu cha ziada. Bila kubadilisha mfumo huo, hata kama utapata rais, waziri wa elimu, katibu mkuu wa elimu, na wakurugenzi wote wizara ya elimu ambao ni wasilamu, tatizo hiyo la inequity katia elimu halitatoweka!
wewe ni nyoka mwenye sumu mbaya ya udiniUjoka,
Katika Wakurugenzi watano Wizara ya Elimu wote watano walikuwa Wakristo.
Una fikra gani katika mgawanyo huu?