Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #41
Zeus,Huyu mzee wetu ana udini sana.
Kawaida ninapomsoma mtu akianza kunitambulisha kwa ''Huyu Mzee,'' uzoefu unakuwa umeshanitahadharisha kitakachofuatia.
Wako wazee wamenishinda umri lakini huwa hawatambulishwi kwa umri wao.
Bahati nzuri kwangu ni kuwa hili silioni kama tusi ingawa nia ya mwandishi huwa hivyo.
Unaweza kuendelea kuniita ''mzee'' ila ondoa ''huyu,'' ili uwe umezungumza kwa adabu na heshima na upambike kwa sura ya ustaarabu wa kijana aliyepata malezi mema kutoka kwa mama yake.
Hii ni kama unapenda la unaona raha kuniita ''huyu,'' hapana neno endelea.
Zeus,
Ikiwa unataka elimu uelimike na uongeze maarifa yako katika historia ya Tanganyika niko tayari kukuonyesha mengi na uchaguzi utakuwa wako mwenyewe kuamini au kutoamini.
Hayo hapo chini nimetoa Maktaba ni darsa tosha kwa atakae kujifunza na kuujua ukweli:
"Kitabu changu cha kwanza na ndicho kilicholeta mshtuko mkubwa katika historia ya nchi yetu ni kitabu cha maisha ya Abdul Sykes ambacho kupitia maisha yake nilieleza historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mshtuko ulisababishwa na kule kutofautiana kukubwa kwa historia hii niliyoandika mimi na historia rasmi iliyokuwa ikifahamika na kuaminika.
Kitabu kilifanyiwa ''review'' na mabingwa wa historia ya Afrika - John Iliffe, Jonathan Glassman na James Brennan na ''review'' hizi zilichapwa katika Cambridge Journal of African History.
Katika mabingwa hawa watatu wa Historia ya Afrika wawili tunafahamiana vizuri - James Brennan na Jonathon Glassman na tumepata kuwa pamoja hapa Tanzania na Marekani.
Kitabu hiki kupita katika mikono ya mabingwa hawa ndiyo kukawa mwanzo wa kitabu hiki kufahamika na kusababisha mwandishi kualikwa kwingi na pia kutiwa katika miradi miwili ya uandishi wa historia ya Afrika chini ya Oxford University Press Nairobi na New York na kazi nilizoandika zote zilichapwa.
Umetaja majina ya viongozi kama Ali Hassan Mwinyi, Rashid Kawawa, Tewa Said Tewa na wengine wengi.
Bahati mbaya hukuwataja Aboud Jumbe na Kitwana Kondo ambao wamepata kutahadharisha kuhusu udini Tanzania.
Katika nafasi yangu kama mwandishi nina mengi nayafahamu kuhusu viongozi hawa ambayo wengi hawayajui na wenyewe hawawezi kuyasema hadharani.
Nina mswada ambao haujachapwa kitabu, ''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania,'' ndani ya mswada huu kuna sura ambayo nimeeleza yale ambayo Rais Mwinyi alikutananayo katika utawala wake na yalimtaabisha sana.
Moja ya matatizo yaliyomkabili ni taarifa kutoka kwa Waziri wa Elimu Prof. Kighoma Malima akimfahamisha yale aliyoshuhudia katika wizara hiyo ya vijana wa Kiislam kunyimwa nafasi za elimu ya juu.
Mzee Tewa kanieleza mengi kabla ya kifo chake na nilimwandikia taazia na unaweza kusoma maisha yake katika kitabu changu, ''Watu Maarufu Katika Uhuru wa Tanganyika,'' (2018).
Naandika mambo ambayo nimeyafanyia utafiti na nina hakika nayo.
Siandiki riwaya kama unavyodhani.
Huenda aandikae riwaya ukawa ni wewe.
Nakuwekea hapo chini links ambazo zitakusaidia wewe kujua zaidi hili somo na pia kunielewa: