Kenya Abdallah Hassan, Katibu Mkuu wa kwanza Muislam Wizara ya Elimu, amefariki

Kenya Abdallah Hassan, Katibu Mkuu wa kwanza Muislam Wizara ya Elimu, amefariki

Huyu mzee wetu ana udini sana.
Zeus,
Kawaida ninapomsoma mtu akianza kunitambulisha kwa ''Huyu Mzee,'' uzoefu unakuwa umeshanitahadharisha kitakachofuatia.

Wako wazee wamenishinda umri lakini huwa hawatambulishwi kwa umri wao.
Bahati nzuri kwangu ni kuwa hili silioni kama tusi ingawa nia ya mwandishi huwa hivyo.

Unaweza kuendelea kuniita ''mzee'' ila ondoa ''huyu,'' ili uwe umezungumza kwa adabu na heshima na upambike kwa sura ya ustaarabu wa kijana aliyepata malezi mema kutoka kwa mama yake.

Hii ni kama unapenda la unaona raha kuniita ''huyu,'' hapana neno endelea.

Zeus,
Ikiwa unataka elimu uelimike na uongeze maarifa yako katika historia ya Tanganyika niko tayari kukuonyesha mengi na uchaguzi utakuwa wako mwenyewe kuamini au kutoamini.

Hayo hapo chini nimetoa Maktaba ni darsa tosha kwa atakae kujifunza na kuujua ukweli:

"Kitabu changu cha kwanza na ndicho kilicholeta mshtuko mkubwa katika historia ya nchi yetu ni kitabu cha maisha ya Abdul Sykes ambacho kupitia maisha yake nilieleza historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Mshtuko ulisababishwa na kule kutofautiana kukubwa kwa historia hii niliyoandika mimi na historia rasmi iliyokuwa ikifahamika na kuaminika.

Kitabu kilifanyiwa ''review'' na mabingwa wa historia ya Afrika - John Iliffe, Jonathan Glassman na James Brennan na ''review'' hizi zilichapwa katika Cambridge Journal of African History.

Katika mabingwa hawa watatu wa Historia ya Afrika wawili tunafahamiana vizuri - James Brennan na Jonathon Glassman na tumepata kuwa pamoja hapa Tanzania na Marekani.

Kitabu hiki kupita katika mikono ya mabingwa hawa ndiyo kukawa mwanzo wa kitabu hiki kufahamika na kusababisha mwandishi kualikwa kwingi na pia kutiwa katika miradi miwili ya uandishi wa historia ya Afrika chini ya Oxford University Press Nairobi na New York na kazi nilizoandika zote zilichapwa.

Umetaja majina ya viongozi kama Ali Hassan Mwinyi, Rashid Kawawa, Tewa Said Tewa na wengine wengi.

Bahati mbaya hukuwataja Aboud Jumbe na Kitwana Kondo ambao wamepata kutahadharisha kuhusu udini Tanzania.

Katika nafasi yangu kama mwandishi nina mengi nayafahamu kuhusu viongozi hawa ambayo wengi hawayajui na wenyewe hawawezi kuyasema hadharani.

Nina mswada ambao haujachapwa kitabu, ''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania,'' ndani ya mswada huu kuna sura ambayo nimeeleza yale ambayo Rais Mwinyi alikutananayo katika utawala wake na yalimtaabisha sana.

Moja ya matatizo yaliyomkabili ni taarifa kutoka kwa Waziri wa Elimu Prof. Kighoma Malima akimfahamisha yale aliyoshuhudia katika wizara hiyo ya vijana wa Kiislam kunyimwa nafasi za elimu ya juu.

Mzee Tewa kanieleza mengi kabla ya kifo chake na nilimwandikia taazia na unaweza kusoma maisha yake katika kitabu changu, ''Watu Maarufu Katika Uhuru wa Tanganyika,'' (2018).

Naandika mambo ambayo nimeyafanyia utafiti na nina hakika nayo.

Siandiki riwaya kama unavyodhani.

Huenda aandikae riwaya ukawa ni wewe.

Nakuwekea hapo chini links ambazo zitakusaidia wewe kujua zaidi hili somo na pia kunielewa:

mohamedsaidsalum.blogspot.com

Tewa Said Tewa Mmoja wa Waasisi wa TANU 1954

Tewa Said Tewa 1924 1998 Mmoja wa Waasisi wa TANU Aliyesimama wa pili kutoka kulia ni Tewa Said Tewa akiwa katika Baraza la M...
mohamedsaidsalum.blogspot.com
mohamedsaidsalum.blogspot.com

mohamedsaidsalum.blogspot.com

RASHID MFAUME KAWAWA KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA

MAPITIO YA KITABU SIMBA WA VITA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA RASHIDI MFAUME KAWAWA Na Mohamed Said Kwa mara ya kwanza Tan...
mohamedsaidsalum.blogspot.com
mohamedsaidsalum.blogspot.com

mohamedsaidsalum.blogspot.com

Uonevu na Udini Upo Tanzania - Aboud Jumbe

Uonevu na udini upo Tanzania Na Alhaj Aboud Jumbe HOJA zimekuwa zikijengwa kuwa nchi yetu imefanikiwa kujenga utaifa ambapo hakun...
mohamedsaidsalum.blogspot.com
mohamedsaidsalum.blogspot.com

mohamedsaidsalum.blogspot.com

USIA WA MAREHEMU KITWANA SELEMANI KONDO KWA WATANZANIA

Hotuba ya Mh. Kitwana Kondo (MB) aliyoitoa Bungeni Dodoma, 1999 Mohamed Said February 17, 2015 0 Annur Na.187- Feb...."
mohamedsaidsalum.blogspot.com
mohamedsaidsalum.blogspot.com
 
Hakuna muislamu anayezuiwa kusoma hata siku moja ila shule inaendana na historia kama ilivyo kwa mambo mengine!

Tuambie matokeo ya shule zinazomilikiwa na Waislamu ukilinganisha na za Wakiristo zipi zinafanya vizuri!
 
Mwaka niliomaliza Chuo Kikuu Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Wanafunzi waliobaki kufundisha wote walikuwa Waislamu lakini Waalimu (Lectuers) karibu wote walikuwa Wakiristo.

1. Dkt Bashiru Ally
2. Dkt Rasul
3. Dkt Lupa Ramadhani

Hao wote nilikuwa nao darasa moja la PS ila hawakubaguliwa kwa kuwa Waislamu ila walichaguliwa kutokana uwezo wao mkubwa darasani

Nchi yetu haina ubaguzi wa kidini kwenye elimu cha msingi ufanye juhudi za kujisomea na utafanikiwa
 
Sisi tunahangaika na mafisadi bandarini na hazina huko. Huyu anahangaikia udini.
 
Mwaka niliomaliza Chuo Kikuu Idara ya Sayansi ya Siasa na Utawala Wanafunzi waliobaki kufundisha wote walikuwa Waislamu lakini Waalimu ( Lectuers) karibu wote walikuwa Wakiristo

1. Dkt Bashiru Ally
2. Dkt Rasul
3. Dkt Lupa Ramadhani

Hao wote nilikuwa nao darasa moja la PS ila hawakubaguliwa kwa kuwa Waislamu ila walichaguliwa kutokana uwezo wao mkubwa darasani

Nchi yetu haina ubaguzi wa kidini kwenye elimu cha msingi ufanye juhudi za kujisomea na utafanikiwa
Uzalendo,
Unazo taarifa za miaka mingine?

Itakuwa vyema tukaangalia na miaka hiyo.

Halikadhalika tukaangalia na idadi ya wanaopata fursa ya kuingia chuoni mathakan katika miaka 10 iliyopita.

Mfano wa mwaka mmoja tena kwa idara moja PS haitoshi.

Weka na idara nyingine.
 
Sisi tunahangaika na mafisadi bandarini na hazina huko. Huyu anahangaikia udini.
Swet...
Hili si suala la udini ni suala la dhulma kwa dhalim kutumia dini yake kuwakandamiza wale wasiokuwa wa imani yake.

Suala hili halina uhusiano wowote na hayo ya bandarini.

Hayo ya bandarini ni ya leo.
Hili ni la azal yaani la muda mrefu.
 
Ujoka,

Katika Wakurugenzi watano Wizara ya Elimu wote watano walikuwa Wakristo.

Una fikra gani katika mgawanyo huu?
ni nani huyo alikupotosha kwamba dini inazingatiwa katika uteuzi?!? hamia Iran au saudia hapa hatujali dini ni uadilifu na madarasa sio madrasa
 
Hakuna muislamu anayezuiwa kusoma hata siku moja ila shule inaendana na historia kama ilivyo kwa mambo mengi!

Tuambie matokeo ya shule zinazomilikiwa na Waislamu ukilinganisha na za Wakiristo zipi zinafanya vizuri!
Uzalendo...

Shule zetu haziwezi kushindana na shule zenu na kwa sababu nyingi sana.

Makanisa yanapokea mabilioni ya shilingi kila mwaka kupitia MoU kati ya Serikali na Makanisa.

Huu mkataba ni kazi ya Lowassa na Mahalu.

Nyie toka ukoloni Waingereza waliweka elimu mikononi kwa Wamishionari na mkawa mnapokea Grant in Aid Waislam walinyimwa ingawa wakilipa kodi.

Wizara ya Elimu toka uhuru ilikuwa mfano wa kigango Waislam hawakuruhusiwa mle ndani.

Kuna mengi yakifanyika mle.
Msome Njozi (2002).

Serikali ilikipiga marufuku.

Msome Bergen (1981) na Sivalon (1992).

Kuna yaliyozifika shule zetu kupitia NECTA inayoendeshwa na waumimi wa dini moja.

Bubu alisema kwa uchungu wa mwanae.
Tunajua mengi.
 
ni nani huyo alikupotosha kwamba dini inazingatiwa katika uteuzi?!? hamia Iran au saudia hapa hatujali dini ni uadilifu na madarasa sio madrasa
Johnson,
Tujadili kiungwana hapana haja ya kutumia lugha za kejeli na kibri.

Mimi si wa kupotoshwa na yeyote awaye yule.

Ninao ujuzi kwa ninachokizungumza.
 
Johnson,
Tujadili kiungwana hapana haja ya kutumia lugha za kejeli na kibri.

Mimi si wa kupotoshwa na yeyote awaye yule.

Ninao ujuzi kwa ninachokizungumza.
mkubwa habari ya kulalamikia dini fulani inaonewa haina mashiko siku hizi bulaza!!! mwisho wa siku utaitwa mchochezi.
 
ni nani huyo alikupotosha kwamba dini inazingatiwa katika uteuzi?!? hamia Iran au saudia hapa hatujali dini ni uadilifu na madarasa sio madrasa
mkubwa habari ya kulalamikia dini fulani inaonewa haina mashiko siku hizi bulaza!!! mwisho wa siku utaitwa mchochezi.
Johnson,

Hilo jina la uchochezi mbona ninalo miaka mingi?

Lugha hii ya "bulaza," kwa hakika kuitumia hapa na kwangu si pahala pake.

Nakusihi tufanye mjadala wa adabu.
 
Mzee sikubaliani na hoja za ubaguzi wa dini hata kidogo

Nchi yetu imetawaliwa na Marais 3 ambao ni Waislamu ( pamoja na huyu wa sasa), Je na wao walichangia kuwabagua Waislamu wenzao?

Kama issue ni misaada kutoka nje kwanini msiombe hiyo misaada kutoka nchi zenye Waislamu wengi? Kwa mfano Mashariki ya Kati waliojaaliwa utajiri mkubwa wa mafuta!?
 
We jamaa ni mwandishi mzuri Sana ,tatizo kubwa ni udini,acha Basi unachefua sana utafikiri haujawahi kula kitimoto
 
Mzee sikubaliani na hoja za ubaguzi wa dini hata kidogo

Nchi yetu imetawaliwa na Marais 3 ambao ni Waislamu ( pamoja na huyu wa sasa), Je na wao walichangia kuwabagua Waislamu wenzao?

Kama issue ni misaada kutoka nje kwanini msiombe hiyo misaada kutoka nchi zenye Waislamu wengi? Kwa mfano Mashariki ya Kati waliojaaliwa utajiri mkubwa wa mafuta!?
Uzalendo...
Kuwa huamini lipo tatizo hii si kitu.

Hilo la kuomba msaada itakubidi nikupe somo zima kuhusu EAMWS walipokuwa wanataka kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam mwaka wa 1968 na hii ndiyo ikawa sababu ya EAMWS kupigwa marufuku na serikali kuwaundia Waislam BAKWATA.

IOC ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania miaka ya 1970 serikali ikakataa kutoa kibali.

IOC ikahamisha mradi huu Uganda chuo kikajengwa Mbale.

Muhimu kwangu ni kuwa tumejadilo tatizi hili na naamini lipo ulilojifunza kutoka kwangu.
 
Mzee ilibidi uchezee ban hapa JF.kila uzi unazotoa unaleta udini sana.yani ungepewa nchi sijui ungetaka iweje
 
We jamaaa ni mshmba sana udini umekujaa kila siku uislam uislam. Tatizo ndugu zako wakacha elimu wakakimbilia madrasa na bahati mbaya teuzi zinaangalia elimu dunia na sio madrasa.
 
Sam,
Udini ni kule kueleza kuwa walikuwapo watu katika watendaji wa Wizara ambao hawakupendezewa na kuwa na Waziri na Katibu Mkuu Waislam?

Tafadhali nifahamishe.
Hapana, udini ni kuamini kila maamuzi yanayofanyika aidha kiserikali na taasisi zake au kijamii na kimamlaka hafanyika kwa kufuata misingi ya dini au msukumo wa dini nyuma yake.

Inaweza ikawa ni coincidence kuwa viongozi wote waliopata wadhifa wa kuteuliwa ni watu wa karibu wa muhusika anae teuwa na mwisho wa siku hawa watu wakawa ni wa dini moja nae.....

But sidhani kuwa ni sahihi au yupo kiongozi ambaye anasema nitamuacha faulani kwasababu sio imani moja na mimi au dini moja na mimi na nitamchukua fulani sababu ni imani na dini moja na mimi.
 
Hivi mzee unajua hii nchi ina watu wengi ila tatzo lako wewe ni udini kati ya wakristo na waislamu ila kumbuka pia kuna kundi la kati hawako upande wowote ila maisha yanandelea, ukweli ni kwamba waislamu kuna sehemu mlichelewa wenyewe toka mwanzo labda kwa kukumbatia huo huo udini wenu au kutokubadilika kulingana na dunia inavyoenda
 
Hivi mzee unajua hii nchi ina watu wengi ila tatzo lako wewe ni udini kati ya wakristo na waislamu ila kumbuka pia kuna kundi la kati hawako upande wowote ila maisha yanandelea, ukweli ni kwamba waislamu kuna sehemu mlichelewa wenyewe toka mwanzo labda kwa kukumbatia huo huo udini wenu au kutokubadilika kulingana na dunia inavyoenda
Hakuna kuchelewa wala nini. Sehemu pakiwa na ubaguzi utajua tu. Unajua watu ambao hawana fursa ya kurekebisha uzembe waliofanya katika maisha yao wakati wa ujana au utoto huwa wanatafuta visingizio vya kuonyesha kuwa haikuwa wao bali walisababishiwa.


Unajua mtu mvivu wa kufiriki huwa anatengeneza nadharia na kuifanya kuwa ni majibu kamili. Ila ukimwambia akupe evidence utaona anavyotekenyeka na kubadili mikao.

Mimi mtaa nilipokulia kuna watu wa imani za kiislam na kikristo, tulisoma shule moja ya msingi na pia tulienda shule za sekondari tofauti ila zote zinatumia mtaala m'moja wa elimu.

Na tulipomaliza sekondari, kuna ambao walikwenda vyuo vya Tanzania, na wapo waliokwenda nje, mimi sikuwahi kuomba kusoma vyuo vya nje sababu nilikuwa muoga kuishi mbali na familia yangu.

Lakini still nilipokwenda chuo bado nilikutana na wengine na tulisoma wengine walifaulu kunizidi, wengine walikuwa viongozi serikali ya wanafunzi.

Na sasa nimemaliza elimu ya chuo nipo uraiani kupambana na uchumi ila bado nakutana na wenzangu tukiishi maisha katika hali ya ufanano.


Muda wote huu sikuwahi kufikiria kuwa kuna mfumo wa dini ambao unawabania watu baadhi wasiweze kupenya popote na kufanya maisha.

Sasa huwa nashangaa sana nikisikia kuna mtu analalamika kuwa kuna hicho kitu ambacho, mimi na wenzangu tusikione kweli.....?!

Aiseeee kuna watu sijui ni malezi waliopitia, unakuta mtu kalelewa na bibi huko tokea utotoni sasa anavyokuwa mtu mzima anaanza kutafuta wa kumdekea kama alivyodeka kwa bibi.......

Maisha sio hisia, maisha ni uhalisia. Yeye sasa kama anaamini kuna udini haya akalage baho, wenzake ndio haoooo tunatafuta maisha tunajenga inchi. Fainali ni uzeeni huko.
 
Back
Top Bottom