Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Duh ebana matokeo vipi? bbc swahili niliitegemea naona haipatikani sijui vipi
 
Mimi nafikiri tunamatatizo ktk bongo zetu ,kumbe tunawasingizia bure akina Bush eti ndio wametega mitego ya kutunyonya.

upumbafu huu ndio unawapa chansi ya kutunyonya watakavyo
mimi nafikiri tuanze kuhoji IQ yetu ipo vipi? tusikimbilie kusema ni kashifa maana inaashiria IQ yetu ipo kutenda mambo mabaya

mfano mtaani kijana mhuni ndiye anaonekana mjanja,kijana malaya anayechukua wasichana na wake wa watu ndiye mjanja ,Fisadi ndiye mwenye kuheshimika.
Hapana jamani tuhojini pia IQ yetu ,upumbafu wa kibabu kimoja hiki ki KIBAKI kitie watu milion kadhaa roho juu .
 
Duh ebana matokeo vipi? bbc swahili niliitegemea naona haipatikani sijui vipi

Mtu, kuwa na subira kidogo. ECK bado wanaweka chumvi, nyanya na viungo (wanapika) ili mambo yatoke hivyo sivyo. Si unajua TENA, mapishi ndani halafu KIBAKI kuleta barazani tu kwa ulaji!!!!
 
Hivi nikumbusheni ile Taasisi ya Mwl. Nyerere si ilikuwa iwe na mafunzo ya wanasiasa wa Afrikaa kuhusu mambo ya maridhiano?,,, kwa maoni yangu yangewapika viongozi wa siasa wa Afrika wawe tayari kuachia madaraka pale wananchi wanavyopenda iwe hivyo, je walifikia wapi? au bichwa langu linanidanganya hapakuwa na kitu kama hiki?

Somo hilo probably lingekuwa la lazima kwa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani na tawala Africa

...hilo somo linafanya kazi kwenye highly democratic states,sio kwetu ambako wanaosimamia mifumo yetu ndio wakandamizaji wakubwa,yaani nilikuwa na matumaini makubwa sana na huu uchaguzi ungeonyesha jinsi demokrasi yetu ilivyokuwa na nilikuwa nategemea katiba mpya ya kenya baada ya miezi sita ambayo Raila aliahidi ambayo ilimwangusha Kibaki kwenye ile referendum,na main thing ya hiyo katiba ilikuwa inaweka check & balance kwenye utawala wa nchi na ina strip some powers from the president kuacha kuonekana mungu mtu kama ilivyo sasa na kupelekea nguvu wananchi wahusika ambayo ndio naamini ndio ilipolala true democrasy ...ukiisoma vizuri hiyo change ya katiba waliyoahidi kuiweka ungefurahi sana
 
Mtu, kuwa na subira kidogo. ECK bado wanaweka chumvi, nyanya na viungo (wanapika) ili mambo yatoke hivyo sivyo. Si unajua TENA, mapishi ndani halafu KIBAKI kuleta barazani tu kwa ulaji!!!!
Mkuu ukiangalia http://www.raila07.com/ tovuti ya raila katoa matokeo yaliyotoloewa na ECK....sijui namna hapa(mnakumbuka msemo wa Chalzi Hilary....)
 
Hii sina hakika kama itakuwa Breaking Nyuuzi au ilishavunjwa saa nyingi
Official ECK Results

Raila Odinga 3,880,053 48 %
2. Mwai Kibaki 3,842,051 47 %
3. Kalonzo Musyoka 346,214 4 %
4. Ngacha Karani 16,010 0 %
5. Pius Muiru 6,856 0 %
6. Kenneth Matiba 6,830 0 %
7. Nazlin Omar 5,048 0 %
8. Waweru Ng'ethe 4,674 0 %
9. Kukubo Nixon 4,246 0 %


Source:http://kenyaelections07.marsgroupkenya.org/data/results/
 
Wanabodi wakati mkisubiria Matokeo Ya Uchaguzi Kenya!!!

Kwenye mapumziko haya Mafupi naomba mupitie post ya mchangiaji mmoja kwenye ISSAMICHUZI.BLOGSPOT.COM

Swali langu kwa Mwakilishi wetu Mh. Zitto(MB),
Hivi wakati mkila kuku pale Dodoma kwenye kale ka mtaa mchana barabara usiku mkahawa mmoja wa nguvu., au sehemu yoyote ya Vijiwe vyenu kuna siku kama wabunge munaongelea mambo ya ICT kama infrastructure muhimu... Maana naona Rwanda na Kenya wanawapiga bao la hali ya juu!!!


Tarehe Sunday, December 23, 2007 9:35:00 AM EAT, Mtoa Maoni: Mchangiaji

Maendeleo ya Kenya, sisi tutafika..Bring on Technology Super Highway....Then we will start moving somewhere...

Forwarded by mchangiaji

World next outsourcing Hub: Kenya ??
Read article...

By Rob Crilly
Correspondent of The Christian Science Monitor
(AXcess News) Nairobi, Kenya - The six clocks on the wall track time zones from the US Pacific seaboard, through the Midwest and across the Atlantic to Britain. Twenty or so computers sit idle, headsets resting on mouse pads waiting for the next shift of call center workers.
It could be a phone bank anywhere in the world but for the clock on the far right labeled "Kenya."
"People say to me, 'Wow, this is happening in Kenya? We only think of you for athletics and wildlife,' " says Gilda Odera, managing director of Skyweb-Evans in the heart of the capital, Nairobi. "But people are getting really interested in us."
Her call center and a dozen others are seeds of an industry that the government hopes will put the East African country on equal terms with India as an outsourcing destination.
The government is pumping millions of dollars into improving the country's outdated telecom system in an effort to capitalize on Kenya's large pool of English-speaking graduates.
Eventually it wants Kenya to be as well-known for its call centers as its lions, tea, and coffee.
But for now, companies like Skyweb-Evans are limited by shoddy infrastructure and ferociously expensive internet connections.
Ms. Odera employs more than 40 people in two shifts. They mostly dial Canada to collect market research and polling data, but she says it can be a struggle to break even.
"Sometimes we have clients that need more than 20 seats but, because we haven't been able to ramp up, we haven't been able to take the work, even though it was attractive work," says Odera.
That is all about to change. In February, her company will open a 75-seat call center, expanding capacity more than threefold.
New fiber-optic cable
Last week, the Kenyan government signed an agreement with French-US telecom group Alcatel-Lucent for a fiber-optic cable linking the Kenyan port of Mombasa with the United Arab Emirates.
More important, it will connect East Africa to the rest of the world's Internet capacity and replace the slow and costly satellite links that act as a brake on the country's fast developing industry in business process outsourcing (BPO).
At the signing, Bitange Ndemo, permanent secretary at the Ministry of Information and Communications, said the connection would allow more ordinary Kenyans to surf the Internet. But the real driving force behind the deal, he said, was the potential for creating jobs in call centers and the rest of the outsourcing industry.
"A year ago we started pushing ourselves as a BPO center," he said. "But if you look at the price and compare it with our competition, we are simply not competitive. "
Typical monthly charges are $7,500 for one megabyte of bandwidth. Elsewhere in the world it costs no more than $400.
"If we can get it below $500 for that megabyte we can make ourselves more competitive, " said Mr. Ndemo.
Work on the 3,062-mile East African Marine System (Teams) cable is due to begin early in the new year.
The $82-million cable will run from Fujaira, in the UAE, along the seabed of the Gulf of Oman and down the African coastline to Mombasa. It is expected to bring the cost of connectivity down to about $500 per month immediately on completion in January 2009.
In the meantime, the government will use $9 million from a World Bank loan to subsidize connections and kickstart the industry in the new year.
Two other cables are also being planned.
The much delayed East Africa Submarine Cable System will eventually run along the Indian Ocean coastline, connecting 10 African cities with India and Europe. And a third will run from Europe to South Africa.
Ndemo said the cost will continue to come down as Kenya becomes a hub for East Africa, selling bandwidth to neighbors such as Tanzania, Uganda, and Sudan.
Mark Kobayashi-Hillary, off-shoring director of Britain's National Outsourcing Association, says Kenya is putting itself in a strong position.
"In Kenya - and the East African region - they have quite a good recent history of democracy, so it is a stable region and there are lots of well-educated people," he said. "That's a good start, but what they don't have is the infrastructure and I guess that's the importance of this fiber-optics deal."
A promising future
Research by the London-based business analysis group Datamonitor supports the optimistic outlook.
In a report published last year, the group forecast that Africa would see the fastest growth in the number of call centers for the rest of the decade, and singled out Egypt, Botswana, Ghana, and Kenya for particularly rapid expansion.
Egypt already has a booming outsourcing industry with many Western companies operating there.
Meanwhile, Botswana, Ghana, and Kenya - all former British colonies - have the sort of linguistic skills and education systems that make them well placed for call centers, according to the report.
And signs of a shift in the global pattern emerged earlier this year as several Indian companies began looking to outsource their own outsourcing operations, as rising wages and crumbling infrastructure took their toll.
Across town from Skyweb-Evans, Kencall is the posterboy for Kenya's outsourcing industry.
Kencall employs 500 people in a converted avocado warehouse on an industrial estate close to Nairobi's international airport.
Nicholas Nesbitt, its chief executive, says there is a ready pool of investors looking to enter the Kenyan industry, particularly from South Africa where labor costs are much higher.
"We've had a good three or four very big international call center companies coming through Kenya and kicking the tires," he says.
"As long as we can keep the drumbeat of Kenya as a good and positive place to invest, then when the time comes people will move in."

All,

Its no laughing matter, with 60% of GDP transferred to the local level under Raila's government, projects like TEAMS will have no funds available and there goes Kenya's dream of being the next Outsourcing power hourse!!! Vision 2030 will be a dream because a broke government will have no money to deliver on such projects! I see ICT as the biggest casualty under a Raila government, I tell you Kenyans better wake before its too late!!!

LK
 


1. KURA IMEHAIRISHWA MPAKA KESHO ASUBUHI.HILI NI JAMBO NZURI NA SIO MBAYA KAMA WENGI WATAKAVYODHANIA.

2. ECK IMEAMUA KILA MGOMBEAJI URAIS ACHAGUE WATU WAWILI KWA NIABA YAKE WAZIKAGUE TAKWIMU ZA MAENEO YENYE TETEZI KWENYE KURA YA URAIS. WAPO CANDIDATES 9 WA URAIS KWA HIYO KUTAKUWA NA TIMU TEULE YA WATU 18 LEO USIKU IKIFANYA KUSHUHUDIA HII UKAGUZI USIKU KUCHA HADI KESHO ASUBUHI PAMOJA NA ECK WENYEWE. INTERNATIONAL OBSERVERS WAWILI NA LOCAL OBSERVERS WAWILI PIA WATAJUMULISHWA KWA HII TIMU.

3. TIMU HII NDIO IMEFANYA ECK KUSITISHA UTOAJI WA HABARI LIVE HAPO KICC NA ILIUNDWA BAADA JAMES ORENGO, MAMA NGILU, BALALA, HENRY KOSGEI AMBAYE NDIYE MWENYEKITI WA ODM NA PROFESSA NYONG'O WALIPOPINGA KURA ZA URAIS FULANI ZILIZOONEKANA WAZI ZIMEIBIWA NA PNU.

4. HII HAINA MAANA KWAMBA ECK HAITAENDELEA KUSABUA ZILE KURA ZA CONSTITUENCY 18 ZILIZOSALIA. LA. MAAFISA WENGINE WATAENDELEA NA KUHESABU HIZI KWASABABU IFIKIAPO KESHO LAZIMA MSHINDI ATATANGAZWA.

5. NADHANI ODM ITAMCHAGUA PROF. NYONG'O NA WILLIAM RUTO AU HENRY KOSGEY NA PNU INAWEZA MCHAGUA MARTHA KARUA ( ALIKUWA WAZIRI WA HAKI NA KATIBA) PAMOJA NA KIJIZEE KIMOJA PENGINE MICHUKI.


6. KUFIKIA WAKATI WA JIONI, KURA ZILISIMAMA HIVI KWA MUJIB WA ECK:

RAILA AMOLO ODINGA-----> 3,880,053
EMILIO MWAI KIBAKI-------> 3,842,051

7. The Presidential Results for 192 Constituencies have already been announced so far. Below are the Registered Voters for each of the remaining 18 Constituencies:


(1) Garsen---------------> 35,129 (KIBAKI, COAST)
(2) Starehe--------------> 158,056 (RAILA/KIBAKI, NAIROBI)
(3) Mandera Central------> 41,086 (RAILA, NORTH EAST)
(4) Kathiani--------------> 100,674 (KALONZO, EASTERN)
(5) Kitui West------------> 71,628 (KALONZO, EASTERN)
(6) Mwala----------------> 77,065 (KALONZO, EASTERN)
(7) Kibwezi---------------> 85,989 (KALONZO, EASTERN)

(8) Maragua--------------> 70,517 (KIVUITU KASEMA ITARUDIWA)
(9) Gatundu South--------> 64,603 (KIBAKI, CENTRAL)
(10) Turkana North--------> 46,250 (KIBAKI, RIFT)
(11) Turkana Central------> 60,384 (KIBAKI, RIFT)
(12) Kachileba------------> 23,085 (RAILA, RIFT)
(13) Changamwe----------> 107,533 (RAILA, COAST)
(14) Kajiado North---------> 107,381 (RAILA, RIFT)
(15) Malaba---------------> 67,250 (RAILA, WESTERN)
(16) Ikolomani-------------> 46,366 (RAILA, WESTERN)
(17) Emuhaya-------------> 81,034 (RAILA, WESTERN)
(18) Kamukunji------------> 119,015(HII KIVUITU KASEMA ITARUDIWA)
----------------------------------------------
TOTAL VOTES REMAINING-->1,363,045
==============================

ZINGATIA HIZI POINTI UKIKAGUA HIZO ENEO 18.

MUHIMU I: KWA KUTUMIA UFAHAMU WANGU WA SIASA ZA KENYA,USHINDI WA WABUNGE KWENYE MAENEO YANAYOPAKANA NA HAYA HAPA JUU NA UJUZI WA MIAKA MINGI YA KUIHAKIKI SIASA YA KENYA, NIMEWEKA HAPO PEMBENI MWA KILA ENEO YULE NADHAN ATAPATA KURA NYINGI WAPI.

MUHIMU II: SIO WAPIGA KURA WOTE WALIOJISAJILI NA IDADI YAO HIO HAPO WALIJITOKEZA KUPIGA KURA. KWA HIVYO NI MUHIMU KUFAHAMU HILI EG/ EMUHAYA , REG. VOTERS=81, 034 LAKINI UNAEZAPATA KWAMBA NI 40, 000 PEKEE NDIO WALIVOTI.

MUHIMU III: HIZO ENEO NIMEZOWEKA MISTAARI ZIPO EASTERN LAKINI SIO KWA WAMERU WANAOMSAPOT KIBAKI. ZIPO KWA ENEO YA KALONZO KWA WAKAMBA AMBAO WALIMPATIA KURA ZAO ZOTE ZA URAIS, KALONZO MUSYOKA. LAKINI KIBAKI AMEMFUATA KALONZO KIKURA KWA MAENEO HIZI ZA WAKAMBA KULIKO RAILA. KWA HIVYO KALONZO ATACHUKUA ASILIMIA 80 YA HIZI KURA ZILIZO NA MISTARI, KIBAKI 15 NA RAILA 5.

_________________________________________________


HABARI ZAIDI


1. GHASIA ZIMETANDAA KWENYE MIJI YOTE MIKUU YA KENYA.POLISI WANAPAMBANA VIKALI NA WANANCHI AMBAO WANFANYA RIOTS KWENYE MIJI ZIFUATAZO:

A. NAIROBI - BARABARA KUU MJINI IITWAYO JUJA ROAD KAMA ILE YA MWENGE IENDAYO MBEZI IMEFUNGWA NA VIJANA WENYE GADHABU.

B. KISUMU (NYANZA) - VIJANA WAMEFANYA GHASIA MCHANA KUTWA WANAOMBA RAILA ATANGAZWE MARA MOJA
C. ELDORET (RIFT VALLEY)( 2 BOYS WAMEUAWA KWA RISASI), BARABARA YA KWENDA UGANDA INAYOPITA KATI YA JIJI HILO IMEFUNGWA. VIJANA WA PNU NA ODM WANAZIDI KUVURUGANA. POLISI ZAIDI INAELEKEA HUKO. JIJI NI LA KIKALENJIN LAKINI KUNA WAKIKUYU KIBAO WALIHAMIA HUKO KITAMBO. VIJANA WANAULIZA KITUMBULISHO ID CARD ILI WAJUE HUYU KABILA GANI, WAMUUMIZE.HII NI NGOME YA ODM

D.KAKAMEGA (WESTERN) MALI YA MIMILIONI IMEIBIWA JINI NA WANANCHI WALIOPAMBANA YA POLISI VIKALI. HII NI NGOME YA ODM PIA.
E. MOMBASA (COAST)- VIJANA WAMESEMA HAWATOKI MABARABARANI HADI KURA ZITANNGAZE RAILA KASHINDA.

F. PIA MIJI MIDOGO KAMA KAPSABET HUKO RIFT PIA MOTO BARABARANI NA MAWE TUU.

G. MKUU WA JESHI LA POLISI AMESEMA WATAKABILIANA NA HAWA NA KULINDA MAISHA NA MALI YA WENYEWE.

H. VIONGOZI WA PNU NA WA ODM NA MABALOZI WAMESEMA PASIPOTANGAZWA MSHINDI KESHO MAMBO YANAWEZA ENEA KOTE NCHINI.

_____________________________________

MIMI SINA BUDI ILA KUWAAGA, TUONANE TENA ASUBUHI.NA NIENDE NIKAWATAFUTE WANA ODM WENZANGU TUSAIDIANE KIMAWAZO. USIKU NJEMA NA JAMANI TUOMBE PAMOJA.
 

MIMI SINA BUDI ILA KUWAAGA, TUONANE TENA ASUBUHI.NA NIENDE NIKAWATAFUTE WANA ODM WENZANGU TUSAIDIANE KIMAWAZO. USIKU NJEMA NA JAMANI TUOMBE PAMOJA.

Mkuu, for sure umefanya kazi kubwa sana. Unastahili pongezi kubwa sana for keeping our people informed on what's up.

Hii ya ghasia inasikitisha na tunawaombea ziishe mapema kabla mambo hayajaharibika. Mambo yakichachamaa tafadhali wewe kimbilia Tanzania na uje na kitambulisho cha Kenyan-Tanzanian utapewa services zote pamoja na fringes muhimu 🙂

See what you can do kuwapunguza munkari vijana wenu ili amani itawale.

Invisible
 
Mkuu KT, ahsante sana kwa hizi updates. I think kwa utaratibu huo inawezekana kurudisha imani kiasi kwamba yeyote atakayeshinda itakubalika japo kwa uchungu. Kudos guys, yet that is another political maturity you have displayed.
 


1. GHASIA ZIMETANDAA KWENYE MIJI YOTE MIKUU YA KENYA.POLISI WANAPAMBANA VIKALI NA WANANCHI AMBAO WANFANYA RIOTS KWENYE MIJI ZIFUATAZO:

A. NAIROBI - BARABARA KUU MJINI IITWAYO JUJA ROAD KAMA ILE YA MWENGE IENDAYO MBEZI IMEFUNGWA NA VIJANA WENYE GADHABU.

B. KISUMU (NYANZA) - VIJANA WAMEFANYA GHASIA MCHANA KUTWA WANAOMBA RAILA ATANGAZWE MARA MOJA
C. ELDORET (RIFT VALLEY)( 2 BOYS WAMEUAWA KWA RISASI), BARABARA YA KWENDA UGANDA INAYOPITA KATI YA JIJI HILO IMEFUNGWA. VIJANA WA PNU NA ODM WANAZIDI KUVURUGANA. POLISI ZAIDI INAELEKEA HUKO. JIJI NI LA KIKALENJIN LAKINI KUNA WAKIKUYU KIBAO WALIHAMIA HUKO KITAMBO. VIJANA WANAULIZA KITUMBULISHO ID CARD ILI WAJUE HUYU KABILA GANI, WAMUUMIZE.

From ballots to bullets, why? Kwanini madaraka yanang’ang’aniwa kwa gharama ya maisha ya watu wengine? Kadiri ushindani ovyo ovyo wa kisiasa unavyozidi ndivyo mbegu nyingine za ukabila, uporaji nk zinapopewa fursa ya kumea! Na walio mstari wa mbele katika yote haya ni vijana ambao nguvu na utashi wao unaweza kuwasukuma kufanya chochote. Mwenyezi Mungu awabariki washindi na washindwa usiku wa leo waweze kukubali matokeo wakikumbuka kwamba maisha ni zaidi ya uchaguzi. Kwamba maendeleo ni zaidi ya demokrasia. Kwamba taifa ni zaidi ya siasa. Kwamba ubinadamu ni zaidi ya ushindani. Kwamba Rais ni mtu mmoja tu katika nchi. Kwamba utii ni bora kuliko sadaka. Kwanini mtu ang’ang’anie uongozi usiopatikana kwa haki? Ni akheri kutoa kiongozi kuliko kuwa kiongozi ambaye ushindi wako ni wizi uliolanishwa kwa damu, kiwango cha juu cha ufisadi! Wakheri wote waliokufa kwa kutetea haki, na ole wao walioua kwa kulinda uovu. Kwangu mimi, haijalishi nani ameshinda-ilimradi ashinde kwa ridhaa ya kweli ya umma! Tuiombee Kenya tukijua nasi tuko njiani. There is a thin line between love and hate…

JJ
 
From ballots to bullets, why? Kwanini madaraka yanang’ang’aniwa kwa gharama ya maisha ya watu wengine? Kadiri ushindani ovyo ovyo wa kisiasa unavyozidi ndivyo mbegu nyingine za ukabila, uporaji nk zinapopewa fursa ya kumea! Na walio mstari wa mbele katika yote haya ni vijana ambao nguvu na utashi wao unaweza kuwasukuma kufanya chochote. Mwenyezi Mungu awabariki washindi na washindwa usiku wa leo waweze kukubali matokeo wakikumbuka kwamba maisha ni zaidi ya uchaguzi. Kwamba maendeleo ni zaidi ya demokrasia. Kwamba taifa ni zaidi ya siasa. Kwamba ubinadamu ni zaidi ya ushindani. Kwamba Rais ni mtu mmoja tu katika nchi. Kwamba utii ni bora kuliko sadaka. Kwanini mtu ang’ang’anie uongozi usiopatikana kwa haki? Ni akheri kutoa kiongozi kuliko kuwa kiongozi ambaye ushindi wako ni wizi uliolanishwa kwa damu, kiwango cha juu cha ufisadi! Wakheri wote waliokufa kwa kutetea haki, na ole wao walioua kwa kulinda uovu. Kwangu mimi, haijalishi nani ameshinda-ilimradi ashinde kwa ridhaa ya kweli ya umma! Tuiombee Kenya tukijua nasi tuko njiani. There is a thin line between love and hate…

JJ

Asante JJ,

kwa kweli baada ya kuona kilichofanyika kenya nimegundua kazi ngumu kweli muliyonayo viongozi wa upinzani katika nchi za afrika .

Tuombe mungu mambo yaishe kwa amani, kibaki akubali kushindwa na arudi othaya akapumzike na alipe pesa ya kiinua mgongo nakupewa ulinzi na wafanyakazi mpaka siku akifa kwa raha na amani lasivyo hata akipata uraisi hakuna faida yoyote itakuwa tu kama wakati wa komandoo huko zanzibar!
 
nakumbuka ule ushenzi wa Zanzibar na Dar es salaam 1995 uliofanywa na hawa mafisadi ambao wanauza nchi sasa huku wananchi wao hawana hata ugali mmoja kwa siku huku wao wakisukuma landcruisers za milion mia mia!
 
SAMAHANI WAKUU KWA USUMBUFU,

NIMEONA NIWALETEENI HIZI RIPOTI MPYA ZIKIWA BADO ZINACHEMKACHEMKA.

SOURCE; KTN TV, NEWS ZA SAA TATU USIKU.


VIONGOZI WA ODM WA MAENEO YA EASTERN PROVINCE AMBAKO MAAFISA WA ECK WALIKATALIA MABOXI YA KURA, WAMEWASILI NAIROBI. TENA KWA KISHINDO.

2. WAMEFANYA MKUTANO NA WANAHABARI NA KUWAELEZA JINSI KURA ZILIVYOIBIWA USIKU WA JANA NA SERIKALI IKISHIRIKIANA NA PNU WAGOMEAMBAJI.

3. WAMESEMA HIZO KURA ZOTE ZAKUTOKA KWA MAENEO ZAO AMBAZO ZIMETANGAZWA NA ECK LEO NA KUMPATIA KIBAKI NGUVU YA KUMFIKIA RAILA, SIO ZA KWELI HATA KIDOGO.

4. WALISEMA MA-AGENTI WA ODM AMBAO WALIKUWA KWENYE KILA KITUO HUKO EASTERN WALIFANYA HESABU SAMBAMBA NA MAAFISA WA ECK HUKO MASHINANE. NA HESABU ZILIZOFIKIA ECK ZIMEPANDISHWA JUU ILI KUMPAFANYA KIBAKI AFIKIE RAILA.

5. KWA MFANO WAMEZINGATIA MAENEO YAFUATAYO:

A) IGEMBE - KIBAKI ALIPATA 39,810 LAKINI ECK IKASOMA 61,289

B) NITHI - KIBAKI ALIPATA 71, 404 LAKINI ECK IKASOMA 95, 000

C) TIGANIA - KIBAKI ALIPATA 33,304 LAKINI ECK IKASOMA 37,688

D) S. IMENTI - KIBAKI ALIPATA 61, 441 LAKINI ECK IKASOMA 75,441

E) N. IMENTI - KIBAKI ALIPATA 78, 684 LAKINI ECK IKASOMA 98,000


NI MUHIMU KUKUMBUKA THAT AKINA KIBAKI WALIKUWA WANADHANI HII SIRI HAITATOKA NJEE JILI B4 HAWA WANA ODM WASAFIRI KUTOKA EASTERN AMBAKO NI MBALI KIDOGO NA WAFIKE NAIROBI, KIVUITU ATAKUWA ASHATANGANZA KIBAKI KASHINDA JIONI! SO, ILE KUSIMAMISHA KURA HAPO KICC YA AKINA ODM LEADERS ILIKUWA STRATEGIC SANA ILI IWAPATIE HAWA MAAJENTI WA ODM MDA WAFIKE NAIROBI.

SASA, KESHO HATA ODM HATIKUBALI KAMWE KWAMBA KIBAKI AMESHINDA. BECAUSE KAMA HII NDIO ILIFANYIKA HUKO KWA BINAMU WA WAKIKUYU YAAN WAMERU BASI JIULIZENI NI KIPI KILIFANYIKA KWA WAKIKUYU WENYEWE HUKO CENTRAL?

CONCLUSION: KENYANS WALIPIGA KURA KWA WINGI KAMA HAIJAONEKANA HISTORIA YETU. TENA KWA AMANI WALIIWEKA NCHI HATA WAKATI MGUMU WA KAMPENI. SASA WAMEFUKUZA 24 OF KIBAKI'S 33 MINISTERS INCLUDING VP. HII INAONYESHA WAZI WANANCHI HAWANA HATIA HATA KIDOGO. UPINZANI AMBAYO INA UWEZO YA KUTUMIA MAANDAMANO, GHASIA NA MENGINE NCHINI JILI WAKO POPULAR SANA, PIA WAO WALIJICONTROL NA WAKAWEKA HESHIMA MBELE.

MAKOSA YAKO NA KIBAKI NA PNU.

KENYA INAWALAANI HAWA WASALITI. WALICHOFANYA IS TREASON.

WALIIBA TAX, WAKENYA WAKAFUKUZA KWA KURA, SASA WAMEIBA HIO KURA.

LAANA KUBWA.


MUHIMU: MUNGU IBARIKI AFRIKA DHIDI YA MAADUI WAKE, SERIKALI ZETU.
____________________
 
Congratulation our ODM party it is something we have been waiting
for,its time we need a change.even though we are away from our
country our hearts are with you ODM.
 
mie huwa sielewi,wat is the definition of so called system?
 
kuna taarifa za mwaliko wa kuapishwa kwa rais siku ya kesho,nafuatilia kwa ukaribu kujua ukweli wake,
halisi..any info kama na wewe umezipata?
 
Iwapo Mwai Kibaki akitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huu basi ile mbegu ya demokrasi halisi ambayo wananchi wa Kenya walianza kupanda kwenye eneo letu la Afrika Mashariki itakufa.
 
Hata kama Kibaki akishinda kwa wizi, lakini a very STRONG message has been sent already!!! i can guarantee you, sisiem saa hii wanakuna vichwa kutafuta formula ya kuchomokea incase wanakutwa na tsunami la mabadiliko kwa ballot box kama hili la next door........hii lakini ni aibu kuu!!!!!.
 
Back
Top Bottom