Kithuku:
Sioni somo hapa.
Mambo yangeendelea kwa mkondo wake wa kawaida, na matokeo kutangazwa bila ya haya yaliyojili, hapo labda ningekubaliana nawe kutoa sifa hizo ulizomimina. Pamoja na hayo, bado sikubaliani na tabia ya kuuana kila panapokuwepo na uchaguzi kama huu. Waache kuuana kwa sababu za kisiasa, hapo tutawakubali kuwa mfano wa kuigwa.
How low do we have to go to stop proclaiming ourselves as models for everyone else?
Hata kama Kibaki akishinda kwa wizi, lakini a very STRONG message has been sent already!!! i can guarantee you, sisiem saa hii wanakuna vichwa kutafuta formula ya kuchomokea incase wanakutwa na tsunami la mabadiliko kwa ballot box kama hili la next door........hii lakini ni aibu kuu!!!!!.
WAHESHIMIWA,
HIZI HAPA NEWS ZA KUWA KEEP IN TOUCH NA HALI VILE ILIVYO.
1. NATIONAL ELECTION VOTES ZA URAIS: KTN, 3.50PM
1. RAILA - 3, 880, 053
2. KIBAKI - 3, 842, 053
2. INAONEKANA BADO HATA KAMA HAWA WATU WAMEIBA RAILA ANAWEZA SHINDA.
3. WAMEHESABU SASA ZIMEBAKIA ENEO BUNGE 18 PEKEE. ZA HUKO KWA KIKA KIBAKI WAMEMALIZA.
4. HIZI VITI ZIKO KAMA IFUATAVYO: NDANI YA MABANO NIMEWAONYESHA NI NANI ATAIBUKA MSHINDI WA KURA ZA RAIS KWA MAENEO HAYA.
6 constituencies in Ukambani, (Zote kwa Kalonzo)
6 in the Coast, (Raila na Kibaki wakipishana)
2 in Central (Kibaki)
2 in Rift Valley (Raila)
1 in North Eastern (Raila/Kibaki wakipishana padogo)
Kivuiti amekataa kura za eneo moja iitwayo Mathira huko kwa akina Kibaki yaan Central ambako matokeo yalionyesha live kuwa kura kaibiwa eti yakiwa kwenye 115%. kifupi kulikuwa na kura nyingi kuliko hata wapiga kura!
Kivuitu pia amekataa kura za Kamukunji hapa Nairobi. Amesema lazima zitarudiwa baadaye.
MUHIMU: ENEO HIZI MBILI ZINGEMPA RASI KIBAKI KURA NYINGI SANA TAKRIBA 80-130, 000.SASA RAILA AWASHUKURU WENZAKE WALIOKUWA HAPO KICC NA ORENGO JAMES.
Kithuku:
Sioni somo hapa.
Mambo yangeendelea kwa mkondo wake wa kawaida, na matokeo kutangazwa bila ya haya yaliyojili, hapo labda ningekubaliana nawe kutoa sifa hizo ulizomimina. Pamoja na hayo, bado sikubaliani na tabia ya kuuana kila panapokuwepo na uchaguzi kama huu. Waache kuuana kwa sababu za kisiasa, hapo tutawakubali kuwa mfano wa kuigwa.
How low do we have to go to stop proclaiming ourselves as models for everyone else?
Wembe:Kalamu,
Usidhani kuwa watu huwa wanapenda kufanya fujo tu eti kwa sababu wanapenda.Hawa watu wanaelekea kuchoshwa na umasikini wa kupindukia,rushwa,kunyinywa haki zao za msingi,uonevu,unyanyasaji na kadhalika.Hivyo wanapoona mtu au kiongozi au serikali inawanyima sauti yao kupitia sanduku la kura huwa hawana namna isipokuwa kumalizia hasira zao kwa njia mbadala.
-Wembe
Kithuku:
How low do we have to go to stop proclaiming ourselves as models for everyone else?
Ninachowasifu mimi ni jinsi walivyoshughulikia hayo matatizo yaliyojitokeza bila kuburuzwa na serikali, na pia jinsi wanaodhulumiwa walivyofanya jitihada ya kujaribu kuzuia fujo (ingawa bado zimetokea, nahisi zingekuwa zaidi kama wasingejitahidi). Kwamba kulikuwa na jitihada za wazi za kuiba kura, na hapohapo jitihada za wazi za kupambana na hali hiyo, wanastahili sifa. Maana wangenyamaza tu halafu mwishowe wakasema wameibiwa, tungekuja na msemo wa kiswahili wa "mbaazi kukosa maua na kusingizia jua". Lakini wamepambana kiume, ndio perseverence ninayozungumzia. Tume ya Uchaguzi imewasikiliza wadau na kuridhia hesabu ipitiwe upya usiku huu, hapo ndipo nilipowasifu kwa kuweka maslahi ya taifa mbele, maana tume hiyohiyo inayo madaraka ya kutangaza matokeo iliyoyapata, lakini wametumia busara na kuamua kuachana na ubabe (kama ule ambao huwa unatokea Zanzibar).
Na zaidi ya hayo yaliyotokea katika siku hizi mbili za mwishoni, maandalizi ya uchaguzi huu tokea awali yalikuwa mazuri. Na hata mbinu chafu zilipojaribiwa, wamechukua hatua za kuzishughulikia badala tu ya kutangaza matokeo kibabe. Ndio msingi wa sifa nilizowamiminia wadau wa uchaguzi wa Kenya.
Because we are not! Model for what: cowardice, hypocrisy, ignorance of our civil rights, disinterestdneness on national matters/interests, fear of CCM and its leaders rather than God, vote rigging and raping or what? Give us a break; I understand your patriotic sentiments, but kaka we are the worst examples of democracy in the region; tena tupo hata nyuma ya Museveni na Uganda yake!
Iwapo Mwai Kibaki akitangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi huu basi ile mbegu ya demokrasi halisi ambayo wananchi wa Kenya walianza kupanda kwenye eneo letu la Afrika Mashariki itakufa.
Mh Zitto Kabwe(MB)
Kuna swali moja zuri sana umeulizwa, naamini wewe unajua nguvu ya IT katika kufuchua uchafu unaofanywa na serikali, huko Bungeni mnafanya nini kuhakikisha kuwa na watanzania wanafikia level ya Rwanda au Kenya kwenye mambo ya IT.
Tawala zote zenye tendecies za Kidikteta cha kwanza zinazopinga ni wanachi kupata habari, kama Tanzania utaona kabisa magaezeti kama "Kandanda kitandani", "udaku" hayasumbuliwi sana lakini magazeti makini kama Rai,Kulikoni serikali inayachachafya sana, sasa nyie wabunge(nina hakika wewe unajua umuhimu wa hili) mnafanya nini, kuwasaidia watanzania kupata internet access kiuruhisi na kwa gharama nafuu. Mimi kusema kweli huwa roho inaniuma sana ninapolipia internet, wenzetu nchi nyingine wanalipia dola 10, kwa mwezi huduma 24/7. Kenya It imeonesha makeke yake kwenye uchaguzi, tuambie juhudi zenu. Maana tumesikia hata baadhi yenu yaani nyie waheshimiwa hata kutumia computer, leave alone internet hamjui. Unaweza kutuambia huku tukiendelea kusubiri matokeo haya ya Kenya.
K-T,
mpaka sasa kuna mpya yoyote? vipi ile kazi ya kuhakiki kura za urais kwenye maeneo bunge ambayo yalikuwa na utata, imekwisha?
eti na PNU nao pasipo aibu wanadai kwamba kwenye baadhi ya maeneo bunge kulikuwa na wizi wa kura wakati wao wameshikilia kila kitu. hivi kweli mgombea wa serikali iliyomadarakani anaweza kuibiwa kura????????????????
Kwa kweli hakuna mpango wowote kwa sasa. Sera ya ICT ambayo iliandikwa na sekta binafsi wakati Mwandosya ni Waziri ni nzuri sana lakini haitekelezwi. Unajua Bunge letu ni la ajabu sana, kuna wabunge hawajui hata kutumia computer. Spika aliwalipia intriductory course, wachache sana walijitokeza. Sasa unapokuwa na Bunge kama hilo ni ngumu sana kuwa na utekelezaji wa sera na IT kukua.
Rwanda ndio inalead katika Afrika now. Wametekeleza E-government na niliambiwa na mmoja wa wabunge wa huko kuwa hata Order paper (mpangilio wa shughuli za Bunge) wabunge hutumiwa by emails midnight na hivyo wabunge wanakuja Bungeni wanajua kazi ya siku hiyo. Sisi huku unajua siku hiyohiyo wakati unaingia Bungeni.
Hata hivyo kuna wabunge kadhaa ambao ni exposed sana, wa pande zote CCM na Upinzani, na ajenda hii tukiijadili vema tunaweza kuiga toka Rwanda. Spika na wabunge wawili akiwemo Mhe. Balozi Kagasheki na Lucy Owenya walienda Rwanda. Ngoja tutacheki ripoti yao.