Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

akkkqw234gs7.jpg



Dhoruba kubwa inayoelekea kwenye gharika.
Ni kwenye mitaa ya Nairobi, Kenya
( Picha ya Reuters)​

Jamani mimi napata wasi wasi na hali ya jirani zetu sasa. Tukumbuke aliyoyafanya Robert Mugabe kwa Zimbabwe ambao uchumi wao ulikuwa ni mkubwa kuliko wa Kenya almost 10 times lakini sasa hivi ni basket case, Mungu apishie mbali. Naomba wale wanaosali leo wawaombee Kenya wamalize mtafaruku huu salama.

Kenyan Tanzanian

Shukran kwa updates.
 
Mimi nafikiri kibaki angekubali tu yaishe.
Mambo ya kuendekeza ukoloni mweusi yamepitwa wakati na hata hivyo maslahi ya mtu mmoja yasihatarishe maslahi ya jamii nzima ya Afrika mashariki.
Hali tete ktk moja ya nchi za afrika mashariki ni tete pia ktk nchi zote hivyo tunakuomba kibaki kubali matokeo unusuru wajukuu wako.
 
Mkuu

Ucheleweshaji huu unatupatia experience nyingine miaka ijayo au chaguzi zijazo.

Kumbe kwenye sheria za uchaguzi kunatakiwa kuwepo na kipengere kinachozungumzia muda wa kuhesabu kura pamoja na kutangaza matokeo.

Dawa ni kushirikisha vyombo vya habari. Kila wakimaliza kuhesabu kura basi matokeo yanabandikwa na kupigwa picha.

Kama tume wanataka, kuna njia nyingi za kufanya maana sasa technology rahisi, lakini lazima tume ya uchaguzi wawe tayari kukubali technology itumike kuzuia wivi wa kura.

Hivi kwanini Afrika wanatumia boxes nyeusi badala ya transparent boxes?
 
K-T

Wakati tunasubiria final moment kama unaweza kutupa brief summary hadi kufikia sasa. Nakumbuka jana ulisema kulikua na majimbo 18 leo umesema bado 9 ungetupa hali ilikuaje wakati tunajiandaa kunywa wine kwa uchungu au kwa furaha.


BADO ECK HAIJASEMA HASA HALI ILIKUWA VIPI KWA ZILE 9 WALIZOHEABU USIKU NA 9 ZILIZOSALIA.

KTN WANASHUGHULIKIA HII STORI YA KUNGOJA HAPA KICC.

SASA MACHO YOTE YAPO HAPA

RAFIKI YANGU MMOJA AMBAYE NI MNDANI WA MP MMOJA WA PNU AMENITUMIA SMS IFUATAYO

"Mwalimu, these are the results Kivuitu has been ordered by statehouse to release this afternoon
Kibaki: 4,176,437
Raila: 4,117,223

Kalonzo has been asked to concede defeat and declare the election free and fair in return for the VP seat.

Leo ni leo!"

Kwa maoni yangu hatungoji tena hesabu za hizo maeneo jili inasemekana baada ya zile 9 usiku kuhesabiwa Raila alimshinda Kibaki kwa 200, 000 na kitu. ikulu waliposikia hio waliitisha mikutano wao wenyewe kwa wenyewe akina Moi na Kibaki na wakuu wa idara mbali mbali za usalama na serikali. Sasa inaesemekana Kivuiti anakataa ku announce hizi results alopewa na Ikulu. Wacha tusubili litakalotokea
 
K-T,
Ina maana sasa bado sina uhakika kuja Nairobi Jan. kunywa Tusker baridi na kusherekea ushindi wa Kibaki?

Well mimi -nitakuja tu hata kama Raila akishinda- nawaombeni wandugu mnipokee tu kama ndugu yenu toka Tz!
 
Dawa ni kushirikisha vyombo vya habari. Kila wakimaliza kuhesabu kura basi matokeo yanabandikwa na kupigwa picha.

Kama tume wanataka, kuna njia nyingi za kufanya maana sasa technology rahisi, lakini lazima tume ya uchaguzi wawe tayari kukubali technology itumike kuzuia wivi wa kura.

Hivi kwanini Afrika wanatumia boxes nyeusi badala ya transparent boxes?

Mzee tamaha ya madaraka ndiyo tatizo na UFISADI.

Siyo kwamba hawajui kuwa technologia ndio suluhisho.

Hawawezi kukubali yapigwe picha maana wanasema ni nyara za sirikali
 
Nafahamu kenya kuna mtandao wa simu unaosapoti gprs,CDMA,HSDPA na kutuma mafail hayo ya matokeo ni Simple,just they creat a vpn na nashuri watumie MPLS VPN ,upelekaji matokeo unaweza ukawa automated hapo nadhani hawataiba ,isipokuwa wasitumie machine kupiga kula yasije yakatokea ya ya Bush
 
K-T,
Ina maana sasa bado sina uhakika kuja Nairobi Jan. kunywa Tusker baridi na kusherekea ushindi wa Kibaki?

Well mimi -nitakuja tu hata kama Raila akishinda- nawaombeni wandugu mnipokee tu kama ndugu yenu toka Tz!

Wala usiwe na shaka Mh. Mzalendo,

Wee njoo tu. Unsksribishwa tena with open hands. Wakenya wameishi maisha ya udikteta awali chini ya uongozi wa Moi sasa Kibaki ndio atushinde kwendeleza life zetu za kila siku?

Amejipaka uchafu sana hata akishinda he has lost the battle in the hearts of the Kenyans waliofukuza baraza lake la mawaziri, vp wake na hata yeye.

No matter how good he will try to be, development, sijui economy sijui nini wakenya hawatamzimia pengine tuu wakikuyu wa kwake hao.

Wee njoo ntakunulia tusker lakini mimi ntakunywa nyongo siku zote hadi this tribal king atoke ikulu.

Bado tunasubiri
 
Jamani! jamani! mkoloni mweusi kishaingia, kibaki 76yrs anataka nini? haya ndio matokeo ya kuchagua upinzani! kuwatoa ikulu ni mbinde, Uhuru Kenyatta alikubali kushindwa japokuwa alikuwa chama tawala na sasa wanatembea kwa amani.
 
Currently Active Users Viewing This Thread: 79 (32 members and 47 guests)
kakindomaster, Jembajemba, mkamap, Halisi, Rwabugiri, kijunjwe, tanzactive, sabasaba, Kitila Mkumbo, COMRADE44, Mnhenwa Ndege, Kenyan-Tanzanian, Verily Verily, mkomboziufisadi, mnyamwezi, Koba, Mtanzania, NakuliliaTanzania, nampula, Kibanga, Invincible, jamco_za, kapinga, semanao, Shiduki, MSAUZI, mfwatiliaji, Mnairobi, wembemkali, green29, ntareyehirungu
.

Hawa wote watakuwa mashaidi jinsi Wanakenya walivyoyanganywa haki yao.
 
jamani huyu Moi/Kibaki na genge lao wanataka nini? Eti watatangaza tu hata watu wakikataa matokeo, watalinda uamuzi wao kwa nguvu zote.TVT sasa wako LIVE
 
Once again K-T

Huku hatuna source ingine ya updates so lolote linalojiri huko usisite kutuhabarisha japo two or three lines
 
ODM wanasema eti, ECK wanajiandaa kumtangaza KIbaki kwa kura 4.5m wakati Raila amepata 4.3m, na wao wanasema hawatakubali kabisa, maana hizo ni kura za kupika. TVT wako LIVE from Nairobi.. Inaonekana wameshajua mambo ni mazuri kwa "CCM/PNU"
 
TVT wanasema je, asipotangazwa Rais itakuaje? maana Kibaki muda wake unaisha leo.... Ulinzi ni mkubwa haijawahi kutokea tokea Uhuru, wanakumbuka jaribio la Mapinduzi ya 1982, unafanana na ulinzi wa jaribio la mapinduzi. Kuna mtu kutoka Nairobi anasema inawezekana hata kuna majeshi kutoka nje ya Kenya
 
Kuna kila dalili kwamba Kibaki atatangazwa kuwa Rais... hali ya ulinzi na mambo yalivyo yanaonyesha wamejiandaa kutangaza kura za wizi.. Inawezekana ndugu yetu K-T anakusanya data ama yumo katika mikakati ya kulinda ushindi wa UMMA
 
TVT wanasema je, asipotangazwa Rais itakuaje? maana Kibaki muda wake unaisha leo.... Ulinzi ni mkubwa haijawahi kutokea tokea Uhuru, wanakumbuka jaribio la Mapinduzi ya 1982, unafanana na ulinzi wa jaribio la mapinduzi. Kuna mtu kutoka Nairobi anasema inawezekana hata kuna majeshi kutoka nje ya Kenya

Inawezekan security ni maslahi ya pande zote maana hata Kibaki na wenzie wansupporters ambao hawampendi Raila so bothe scenario inawezekana kulindwa. Je Raila amewekewa na yeye ulinzi wa kutosha?
 
JAMANI KWA MUJIBU WA TVT KUNA KILA DALILI KWAMBA KIBAKI ANATANGAZWA KWA KUWA SASA WANASEMA BAADA YA KUTANGAZWA RAIS WANAKWENDA MOJA KWA MOJA IKULU KUMUAPISHA, kwa hiyo haiwezekani akawa ni RAILA AMBAYE ATAKWENDA KUAPISHWA MOJA KWA MOJA
 
ODM wanasema watakwenda mahakamani kama matokeo yatapikwa
 
Yaani ina maana kuna watu wameshaalikwa kwenye kwenye sherehe ya kuapishwa bila kujua nani mshindi? Je kutakuwa na watu kutoka nchi za nje tofauti na mabalozi waliopo Nairobi?
 
Hayo ndio maswali bila majibu. Wanaweza kuwa wamepigiwa simu watu kama Kikwete, Museveni na wengine marais jirani. Na wao wataruka mara moja kwenda Nairobi na kurudi
 
Back
Top Bottom