Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Mtanzania.. bado sijaelewa how can Kenyan leaders justify the killing of 300 people kwa kusema ati matatizo ya Africa na matatizo ya Magharibi ni tofauti... Tunaiga magharibi mambo mengi kweli hadi lafudhi.. sasa kwanini hatuigi jinsi wanavyotatua matatizo!!?

Hivi ni wapi ambapo hawa wame-justify hayo mauaji? Nimemsikiliza Raila akihojiwa leo na Andrew Marr wa BBC kwa zaidi ya dk 15, sijaona hata sehemu moja ambapo ame-justify mauaji, nimesoma pia maandishi mbalimbali yanayom-qiote Raila, sijaona, au mimi sijui maana ya "justify"?
 
Wa kulaumiwa ni huyo mwizi Kibaki. Kama kuna vitu vya kuiga basi tungeiga culture ya kukubali kushindwa pale unaposhindwa na si kung'ang'ania ushindi ambao hukuupata. Hivi maisha yako kwenye uraisi/ siasa tu? Kwani kushindwa uraisi ndio imekuwa mwisho wa dunia? I can't stand these motherfu.ckers. I just can't stand them. Tatizo hapa ni Kibaki na the only way ya kulitatua ni yeye kuachia ngazi. Sijui lini tutastaarabika.

Wengine watakwambia Raila akubali yaishe ili wakenya waishi na rais wa bandia for 5 years!
 
Wengine watakwambia Raila akubali yaishe ili wakenya waishi na rais wa bandia for 5 years!

Kwa Odinga kukubali yaishe atakuwa msaliti kwa wapenda haki na demokrasia. Wa kulaumiwa hapa ni mwizi Kibaki. Angekuwa muungwana na kukubali kushindwa haya yote yasingetokea kwa sababu hakuna mtu anayependa kudhulumiwa
 
Mtanzania.. bado sijaelewa how can Kenyan leaders justify the killing of 300 people kwa kusema ati matatizo ya Africa na matatizo ya Magharibi ni tofauti... Tunaiga magharibi mambo mengi kweli hadi lafudhi.. sasa kwanini hatuigi jinsi wanavyotatua matatizo!!?

Mwanakijiji,
Labda kama unamsema Mtanzania mwingine lakini hakuna mahali niliposema
Kenyan leaders wamejustify au wanaweza kujustify hayo mauaji. Badala yake
mimi nilikuwa na maana baada ya kuiba kura na kuonekana wazi kura zimeibiwa kwa hali ya Afrika ya sasa hakuna kiongozi ambaye angeweza kusimamisha hizo vurugu pamoja na mauaji yaliyofuatia.

Kulinganisha Afrika na Florida ni dalili tosha kuonyesha huelewi historia na perceptions za Waafrika walio wengi.

Suluhu ya Kenya ni kwa Kibaki kuondoka na baada ya hapo kuanza reconciliation ya kweli ambayo itaambatana na kutunga katiba bora, tume ya uchaguzi, pamoja na mahakama huru. Palipo na haki hata siku moja hapawezi kuzaa vurugu. Vurugu ni matokeo ya injustices mbalimbali kwenye jamii.
 
Mtanzania, nami nikubaliane na wewe katika hili maana:
-nashindwa kuelewa iweje, Kibaki aibe kura, aapishwa within 1 hour, watu wakereke, wafanye fujo, kisha watu wamlaumu Raila on this?
-Nashindwa kupata picha, raila anaingiaje hapa, alisikika akiwaambia 'watu wake' wakachukue mapanga na sime? kalianza Kibaki kwa kuiba kura, sasa kwa nini alaumiwe raila?
-iweje,hawa wanaoitwa mediatore, kutoka marekani, afrika kusini, AU, nk, wanakuja na suala la 'serikali ya umoja wa taifa' as if uchaguzi haukuwa na mshindi? Mshindi alikuwepo, na anafahamika, na ni jukumu la mshindi kuona kama kuna haja ya serikali ya mseto, umoja wa kitaifa or whatever!
-Ndio maana ni muhimu kwa Kibaki kustep down, awaombe radhi wakenya na dunia nzima, kwa kuiabisha demokrasia kiasi hiki, kisha kama vipi, uchaguzi urudiwe na yeye akiwa brave enough asigombee tena!
-Kinyume na hivi, tutaendelea kuona fujo ma mauaji kenya, hadi hapo haki itakapopatikana!
 
-iweje,hawa wanaoitwa mediatore, kutoka marekani, afrika kusini, AU, nk, wanakuja na suala la 'serikali ya umoja wa taifa' as if uchaguzi haukuwa na mshindi? Mshindi alikuwepo, na anafahamika, na ni jukumu la mshindi kuona kama kuna haja ya serikali ya mseto, umoja wa kitaifa or whatever!
Ndio unafiki wa siasa za dunia! Ati askofu mzima amefunga safari toka SA: kuja kusema suluhisho ni serikali ya kitaifa! mbona hilo ni jambo rahisi kuliko yote kwa Kibaki.
Wapi Mandela?!!! ndiye mwanamume aliyebaki huku duniani mwenye uwezo wa kuita spade a spade not a big spoon.
 
Ati askofu mzima amefunga safari toka SA: kuja kusema suluhisho ni serikali ya kitaifa!

Kilitime,

You rock man! Hahahaha...! You got it right. Yani mwenyewe nilikuwa najiuliza nini alichofanya cha maana hata simwelewi. Labda kwakuwa sijapata inside info ya alichokiongea kwa mapana zaidi.
 
Ndio unafiki wa siasa za dunia! Ati askofu mzima amefunga safari toka SA: kuja kusema suluhisho ni serikali ya kitaifa! mbona hilo ni jambo rahisi kuliko yote kwa Kibaki.
Wapi Mandela?!!! ndiye mwanamume aliyebaki huku duniani mwenye uwezo wa kuita spade a spade not a big spoon.

It is as if walikuwa wanangojea machafuko yatokee, ndipo wapate hizo 'ajira' za muda...mi wakati mwingine napata hisia kuwa kuna watu wanainterven just to have their names heard, ndo yale ya vita ya panzi......
 
Posted Date::1/6/2008
Polisi wamwagwa kuzuia maandamano ya wapinzani
*Wangwe alalamikia waandishi kwa 'kumchoma'

Na Mkinga Mkinga
Mwananchi

JESHI la Polisi jijini Dar es Salaam jana lilifanikiwa kuzima maandamano yaliyokuwa yamepangwa na vyama vinne vya upinzani yaliyolenga kupinga ushindi wa Rais wa Kenya, Mwai Kibaki na kumtaka kuachia ngazi ili kurejesha amani nchini humo.

Maandamano hayo yalikuwa yanaratibiwa na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Chacha Wangwe na yalipangwa kuanza saa mbili asubuhi katika eneo la Urafiki, Manzese jijini Dar es Salaam na kumalizikia katika ofisi za Ubalozi wa Kenya nchini.

Kuzuiwa kwa maandamano hayo kulifuatia hatua ya Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dare s Salaam, Alfred Tibaigana kuyakataza kwa kuhofia kuwa Wakenya wanaweza kujiunga nao na kusababisha uvunjifu wa amani.

Polisi walionekana kutanda katika maeneo ya Manzese kuanzia saa 12 asubuhi, huku wakiwa wamevalia kikamilifu kupambana na waandamanaji wa vyama hivyo kama wangetokea.

Askari hao walikuwa na bunduki, mabomu ya machozi (tears gas) pamoja na mbwa, walionekana kutanda katika eneo lote la Manzese na kila mara walionekana kuwa makini kufuatilia taarifa kama kulikuwa na watu waliolenga kuandamana.

Wapinzani hawakufika katika maandamano hayo licha ya kwamba juzi kupitia kwa mwakilishi wao, Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Tarime, waliahidi kufanya hivyo.

Kauli yao ya juzi ilionyesha kuwa hawana hofu ya aina yoyote na polisi na kwamba walikuwa radhi kuandamana na kwamba wangekubali kupokea matokeo ya aina yoyote kutoka kwa polisi hata kama yangekuwa yanayoambatana na matumizi ya nguvu ya dola.

Majira ya saa nne asubuhi Wangwe alipigiwa simu na gazeti hili kutaka kujua maandamano yangeanzia wapi na maelezo kati ya gazeti hili na Wangwe yalikuwa kama hivi ifuatavyo:

Mwandishi: Mheshimiwa Makamu mnaanzia wapi kuandamana maana hapa Mahakama ya Ndizi (Urafiki) naona kuna polisi tu.

Wangwe: Ebu njooni mpaka Mtaa wa Mwinjuma ndio mahali tumekutana hapa na kupanga maandamano yetu kuelekea katika ofisi za ubalozi.

Mwandishi wa gazeti hili alipofika katika eneo hilo, alimkuta Makamu Mwenyekiti huyo pamoja na baadhi ya wafuasi wake wakijiandaa kwa maandamano hayo.

Katika kipindi hicho walikuwa wakijipanga kuhusu wapi pa kuanzia na tayari walikuwa na taarifa kuwa polisi wametanda maeneo waliyotangaza awali kuwa wangeyatumia kwa maandamano.

Wakati harakati hizo zikifanyika, palionekana dhahiri kuwa baadhi ya wahusika kutoka katika vyama vingine vitatu vya upinzani hawakuwepo na hivyo kuonyesha kuwa, maandamano hayo yalikuwa chini ya Wangwe peke yake huku akiwa na viongozi wa ngazi za chini wa Chadema.

Wakati majadiliano hayo yakiendelea katika Mtaa wa Mwinjuma, waandishi wa habari walizidi kumiminika katika eneo hilo wakiamini kuwa maandamano yapo, lakini ikawa vinginevyo.

"Naona hawa jamaa (Polisi) wamejipanga kwelikweli, bila shaka sasa itabidi tuandamane kutoka katika eneo la Manyanya kuelekea katika ofisi za Chadema, maana lengo letu ni amani, si fujo kama wao wanavyodhani, lakini lazima tuandamane tu," alisema Wangwe.

Huku akiendelea kutoa mikakati yake kwa waandishi wa habari, baada ya dakika chache tu eneo la Mwinjuma liliingiliwa na polisi ambao walionyesha kusaka walipo waandamanaji.

Kufuatia kufika kwa polisi katika eneo hilo, Wangwe aliondoka huku akiwaeleza waandishi wa habari kuwa, anawafuata vijana ambao walikuwa wamebeba mabango, ili kufanya maandamano hayo kama walivyokuwa wameyapanga.

Baada ya kuondoka katika eneo hilo, polisi wa kutuliza ghasia walivamia katika eneo hilo ambapo waandishi waliondoka pia katika eneno hilo huku wakiwasiliana na Wangwe, ambaye aliwaambia waende Makao Makuu ya Chadema ndiko wangefanyia maandamano yao kwa kuzunguka ndani ya viwanja vya ofisi ya chama hicho iliyoko katika eneo la Kinondoni.

Baada ya waandishi kufika katika ofisi hizo, Wangwe alianza kuwatuhumu akisema kuwa wanamuuza kwa polisi.

"Haiwezekani kila eneo ninalohamia ili kuwakwepa hawa polisi wawe na taarifa. Ni wazi kuna watu hapa wanafanya mawasiliano nao," alisema kwa hasira na kuongeza;

"Makamanda naona sasa mmeanza kuniuza, maana baadhi yenu wanatuma ujumbe mfupi wa simu kwa polisi katika kila hatua tunayoifanya, nimesikitika sana ila nitapambana mpaka dakika ya mwisho."

Wasomi:Kivuitu anyang'anywe digrii ya Chuo Kikuu(Gazeti la Majira)

*Ni kwa kutoa matokeo yenye utata uchaguzi Kenya
*Profesa Haroub:Amedhalilisha maadili ya kisomi
*Shivji:Kilichotokea Kenya ni ufisadi mkubwa
*Mtoto wa Mwinyi aeleza aliyoyashuhudia Kenya
*Wanafunzi Vyuo Vikuu nao kuandamana Jumamosi

Na Waandishi Wetu

WASOMI wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kampasi ya mlimani jana wametoa tamko zito kuhusu kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu wa Kenya huku baadhi wakipendekeza Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi nchini humo, Bw. Samuel Kivuitu ambaye alisoma nchini, apokwe shahada yake aliyotunukiwa kwa kushindwa kufanyakazi zake kisomi na kusababisha umwagaji wa damu.

Kauli hiyo nzito ilitolewa Dar es Salaam jana na baadhi ya wasomi waliohudhuria mdahalo maalum kujadili hali ya kisiasa nchini Kenya kufuatia Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika kwenye ukumbi wa Nyerere Art Theatre II chuoni hapo.

Profesa Othman akitoa maoni yake kuhusu uchaguzi huo mbali na kulaumu vitendo vya kubanagwa demokrasia, pia aligusia juu ya dhima waliyonayo wasomi kama Samuel Kivuitu katika kutoa maamuzi yenye maslahi kwa jamii.

Akitoa mfano kwa Bw. Kivuitu, Prof. Othman alisema Mwenyekiti huyo alishindwa kusimamia maadili yake ya kisomi na badala yake kutangaza matokeo ambayo inaonekana hakuwa akiyaamini.

"Ingekuwa amri yangu ningependekeza msomi yeyote ambaye anashindwa kusimama katika msimamo wake katika kuamua mambo makubwa basi avuliwe shahada yake kwani anakuwa ameshindwa kuitumia na hiyo ndiyo iliyooneshwa kwa Bw.Kivuitu," alisema

Msomi huyo mashuhuri nchini alisema amewahi kutoa pendekezo kama hilo kwa ofisa mmoja mwandamizi wa Jeshi la Polisi ambaye pamoja na kuwa na shadaha ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam lakini ndiye aliyeongoza mauaji ya 2001 ambapo polisi waliwafyatulia risasi wafuasi wa chama cha upinzani cha CUF waliokuwa wakiandamana visiwani Zanzibar.

Kitaaluma Bw. Kivuitu ni mwanasheria ambaye pia amesajili kuwa wakili wa Mahakama Kuu ya Kenya na ana kampuni binafsi ya uwakili ya Kivuitu and Company Advocates iliyoko jijini Nairobi.

Taarifa za kiuchunguzi zaidi za Majira Jumapili zinaonesha kuwa Bw. Kivuitu alisoma kwenye kitivo cha sheria cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwanzoni mwa miaka ya 1960 kabla ya kwenda Chuo Kikuu cha London, Uingereza kwa masomo zaidi.

Kwa upande wake msomi mwingine mashuhuri nchini, Profesa Issa Shivji akizungumza kwenye mdahalo huo, amesema ufisadi ndiyo yaliyosabababisha kuvurugika kwa uchaguzi wa Kenya na kusababisha mamia ya watu kufa.

Msomi huyo alisema tatizo hilo la ufisadi ambao umesababisha watu waporwe haki zao ni la kisheria zaidi hivyo akashauri, walioiba kura wakamatwe na wale walioibiwa haki zao warejeshewe.

Pia alisema matokeo ya uchaguzi wa Kenya hayana tofauti na matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar hivyo kuna mambo mengi ya msingi ambayo Watanzania wanapaswa kujifunza.

"Suala kubwa la kujiuliza hapa Watanzania ni kwamba tumejifunza nini kwa matokeo ya uchaguzi wa Kenya kwani yaliyotokea katika uchaguzi huo ndiyo yalitokea katika uchaguzi wa Zanzibar," alisema.

Joseph Butiku

Bw. Joseph Butiku ambaye ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Mwalimu Nyerere, alisema nchi nyingi za Afrika hujifunza kuendesha nchi kwa mfumo wa siasa za vyama lakini migogoro imekuwa mingi zaidi.

Naye aliunga mkono dhana ya ufisadi akisema hali hiyo inasababishwa na makundi ya watu wachache ambao wanajiingiza katika ufisadi kufanya kile wanachokitaka huku watu wasiokuwa na hatia wakipoteza maisha.

Alisema kilichotokea Kenya si suala la watu kugombana kwa sababu ya ukabila bali kupokwa demokrasia yao.

"Ukingalia kwa makini hali ya Kenya utagundua kwamba wananchi wanahitaji mabadiliko na ndiyo maana baada ya kuona matokeo yamekwenda tofauti na matarajio wameshikwa na hasira na kuamua kupigana. Lakini haina maana kwamba vurugu zao zinatokana na ukabila bali wanataka demokrasia ya kweli kwa kuwa na kiongozi aliyetokana na wananchi," alisema.

Alisisitiza kuwa wananchi wa Kenya walikuwa wanahitaji kiongozi makini na hawakufanya uchaguzi kwa kuangalia ukabila.

"Hasira ya wakenya imedhihirisha nini wanachotaka katika Serikali yao japo njia waliyoitumia haikuwa sahihi lakini kimsingi imefikisha ujumbe wa hisia zao kilichobaki warudi nyuma na kujadili hatima ya nchi yao," aliongeza.

Alisema suala la kurudia uchaguzi si la gharama kwa sasa bali gharama kubwa ni kurudisha damu ya watu ambayo tayari imemwagika na watu kupoteza maisha.

Dkt. Mushumbusi Kibogoya

Kwa upande wake, Dkt. Kibogoya naye alisema wananchi wa Kenya wameonesha kuwa hawako tayari kuubeba ufisadi.

Alisema tofauti na mtazamo wa Wakenya kuukata ufisadi, hapa nchini ufisadi umekuwa sehemu ya kabila la watu fulani na kibaya zaidi baadhi yao wanashika nafasi za juu za uongozi wa nchi hivyo yanahitajika mabadiliko makubwa.

"Nchi nyingi za Afrika zipo katika Ufisadi na Tanzania hali ni mbaya zaidi kwani viongozi walio wengi ni mafisadi na wananchi wamebebwa na watu hao bila ya kujua wapi watakwenda kuachwa," alisema

Pia alidai Tanzania haina amani kama viongozi wanavyodai bali wananchi wengi ni waoga kwani wapo kama kondoo na lazima ifahamike sehemu ambayo haki haitendeki basi amani haiwezi kuwepo.

"Watanzania wanashindwa kupata chakula na huduma muhimu halafu ukiuliza unaambiwa watu wana amani.Kama huna kitu ambacho unakihitaji hiyo si amani," alisema.

Pia alitoa changamoto kwa Watanzania kuwa wakati wakipiga kelele kuhusu Kenya wajiulize nini kilitokea wakati wa uchaguzi mkuu wa Zanzibar.

Abdallah Mwinyi: Huu ndio ushuhuda

Akizungumza kwenye mdahalo huo,Mbunge wa Bunge la Muungano kupitia viti vya Zanzibar, Bw. Abdallah Mwinyi, ambaye pia ni mtoto wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Mzee Ally Hassan Mwinyi, aliwaeleza wasomi hao yale aliyoyashuhudia alipokuwa nchini Kenya.

Katika ushuhuda wake alisema walishuhudia jinsi ucheleweshaji wa matokeo ulivyotokea lakini kwa mengi zaidi alisisitiza kuwa watakabidhi ripoti yao kwa Tume ya Uchaguzi ya Kenya (ECK).

Hat hivyo Bw. Mwinyi alisema yeye alikuwa miongoni mwa Watanzania 14 waliokwenda nchini humo kuangalia uchaguzi huo na pia kujifunza demokrasia ya nchi hiyo lakini hawakuwa wachunguzi.

"Kazi yetu Watanzania ilikuwa ni kujifunza mazuri ya uchaguzi huo lakini hatukwenda kama wachunguzi hivyo kuwepo kwetu katika uchaguzi huo yapo mambo ambayo tumejifunza," alisema.

Vyuo Vikuu:maandamano yaja

Rais wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Daud Deo alisema vurugu zinazoendelea nchini Kenya wao zinawauma kila wanapofikiria na hasa wakiangalia maisha ya vijana wenzao hususan waliomo vyuoni wakipta tabu.

Bw. Deo ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki alisema unyama unaoendelea kufanyika nchini Kenya, wao wataendelea kuupinga na kulaani mwenendo mzima wa uchaguzi huo huku wakishinikiza kufanyika mazungumzo ya amani ili kuokoa maisha ya vijana wa nchi hiyo.

Naye Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania (TAHIRISO), Bw.Julias Mtatilo alisema kutokana na hali iliyopo Kenya hivi sasa wamepanga kufanya maandamano ya amani Januari 12 mwaka huu kwa lengo la kuhamasisha upatikanaji wa amani.

Alisema tayari wameshandika barua ya kuomba kibali cha maandamano kwa jeshi la polisi ambapo wamaamini wataruhusiwa kwani nia yao ni kuona vurugu za Kenya zinasitishwa.
 
Wa kulaumiwa ni huyo mwizi Kibaki. Kama kuna vitu vya kuiga basi tungeiga culture ya kukubali kushindwa pale unaposhindwa na si kung'ang'ania ushindi ambao hukuupata. Hivi maisha yako kwenye uraisi/ siasa tu? Kwani kushindwa uraisi ndio imekuwa mwisho wa dunia? I can't stand these motherfu.ckers. I just can't stand them. Tatizo hapa ni Kibaki na the only way ya kulitatua ni yeye kuachia ngazi. Sijui lini tutastaarabika.

Msisahau kwamba Mfumo wa Mahakama amboa ndio unaotakiwa kutoa haki unaposhindwa kazi ya ndipo society inapo disintergrate !
kama mahakama ingekuwa inaaminkika na inafanya kazi yake ushahidi upo wazi kwamba there was rigging na Raila angelienda mahakamani kudai uchaguzi urudiwe .Alas hiki hakiwezekani Kenya wala kwingeneko Afrika.
 
Why the cost of losing elections is just too high

By JAINDI KISERO
The East African

Clearly, tribalism is at the core of the post-election conflict facing Kenya. Indeed, the ethnic factor is the main reason why a power sharing deal between the main protagonists, President Mwai Kibaki and Raila Odinga, is proving difficult to negotiate.

In Kenya, winning and losing elections is a high-stakes affair because it means exclusion of the losers from power and distribution of resources for five years.

Simply stated, losing an election in Kenya implies the sacking of permanent secretaries, parastatal heads, directors of state corporations and other public officials from the tribes that have lost.

On the other hand, winning elections also means preferential treatment of companies owned by the president's tribe in the award of government contracts and the major procurement deals floated by public corporations.

All the key ministries and critical government institutions - the Ministries of Finance, of Internal Security and Agriculture the Central Bank and the major parastatals providing critical utilities - such as electricity, ports, airports, roads etc - must be in the hands of the president's tribesmen.

Where some of these ministries and institutions are in the hands of other tribes, their permanent secretaries or boards are stuffed with the president's tribesmen such that, even though nominal power is in the hands of people from other tribes, it remains clear who wields effective power.

One of the reason members of the Kalenjin tribe of former president Daniel arap Moi voted so massively against Mwai Kibaki was the feeling that too many of their tribesmen were sacked when Kibaki took over in early 2003.

A nascent Kalenjin business class that had emerged during Moi's regime disappeared overnight, their links to sources of patronage having been suddenly cut off.

At the beginning of Kibaki's administration, there were four permanent secretaries from Odinga's Luo tribe in a government of 31 ministries. However, after Kibaki's government lost the referendum of 2005, most of them were sacked.

Currently, the Permanent Secretary in the Ministry of Trade and Industry, David Nalo, is the only permanent secretary from Odinga's Luo community.

Thus, when viewed in ethnic terms, the stakes involved in losing elections in Kenya are just too high to contemplate. International mediators may force Odinga and Kibaki to share power, but the long-term political solution for Kenya will be how to reform the politics of the country by introducing constitutional changes that ensure that neither the majority nor the minority are threatened with permanent exclusion from power and resources for development.

Perhaps the most poignant lesson from the conflict in Kenya is that the country needs to build institutions and systems that will put the stakes of losing a democratic election low enough to enable the contesting parties to accept the outcome of the elections and dissuade losers from resorting to violence.

An Electoral Commission stuffed with the president's appointees, whose actions routinely elicit charges of bias and rigging, is hardly feasible in an environment of such high stakes.

A power-sharing deal between Kibaki and Odinga will also be difficult to achieve in a context where the "big man" still enjoys imperial powers.

The president of Kenya can dangle the carrot of state resources for development and give out largesse to those in the opposition willing to co operate with him while freezing resources in opposition strongholds.

There is a dire need to address the issue of ethnicity and tribalism in the country. The elite of the country is at a point where they must look squarely in the mirror of history and concede that political tribalism is a threat to the unity of the nation state.

At independence, the elite of the country assumed that tribalism was a temporary phenomenon that would soon melt way.

In the words of scholar Yusuf Bungura, "The popular expectation was that the citizens of the new nation states would break out of the boundaries of ethnicity, embrace a secular-nation state identity, develop a rational scientific view of development and treat individuals as autonomous entities".

It was assumed that inter-ethnic marriages, employment outside ethnic territories, urbanisation and interaction of students in ethnically integrated schools and colleges would kill off tribal identity.

Experience has proved these assumptions wrong. As the post-election conflict has shown, the fact that the citizen in Kenya is ready to kill and die to defend his ethnic interests is a wake up call to start treating ethnic ideology rather more seriously.

Ethnically divided Kenya must urgently go back to constitutional reform and introduce systems that entrench the politics of inclusion.
 
Naam ni aibu iliyoje kwa wasomi wa UDSM au vyama vya upinzani kutoandamana na kukemea ukiukwaji wa demokrasia na mauji ya wananchi wasio kuwa na hatia nchini Kenya.Tuko katika zama za uwazi na ukweli na hivyo vyama vya upinzani na wasomi ni lazima wawe mstari wa mbele kukemea,kufichua,kupinga na kuwakomboa wananchi ambao wengi wao hawana mtu wa kuwasaidia.
Hivyo basi mimi nawaunga mkono wasomi hao wa UDSM kutumia ujuzi wao wa kisheria,hekima na maono yao katika kukemea ufisadi,uvunjaji wa haki za binadamu,mauaji ya raia wasio na hatia, na ukiukwaji wa demokrasia nchini Kenya kwa kufanya maandamano yao Jumamosi ijayo.

Ni lazima waelewe kuwa serikali ya CCM haipendi uozo huo ufunuliwe na ndiyo maana imekaa kimya kama bakuli la maji! pia cha kushangaza kuna watu hadi hapa JF ambao kwa sababu wanazozijua nao wamechukua msimamo huo huo wa serikali ya CCM kushabikia na kuwanyima haki watanzania kufanya maaandamano ya amani kupinga umwagaji damu na maonezi wanayofanyiwa watu wa Kenya.Ni lazima tuelewe kuwa maisha ni haki ya kila mtu na hakuna mtu au chama au kabila linaloweza kunyima mtu kuishi.Hivyo basi tumeona mauaji yametokea nchini Kenya na hakuna hata sehemu moja inayosema kuwa wapinzani wa Kenya ndiyo waliwauwa wananchi hao.Hivyo suala la kuandamana kwa watanzania wakiwemo wasomi wa UDSM ni suala la muhimu katika kuonyesha msimamo wao katika kutetea haki za wanyonge popote pale duniani ikiwemo Kenya.
Hivyo wale wote ambao wamechukua ile propaganda ya serikali ya CCM na polisi wake ya kuwa maandamano ya amani ni ya kumpa support Raila na hivyo kupendelea upande mmoja wasutwe kwa sauti ya juu na fikra zao wenyewe kwa kuwa wameshindwa si tu kukemea maovu na udhalimu bali wanahalalisha mambo haya kutokea tena katika sehemu nyingine Afrika.
Afrika kama bara tumechoshwa na michezo hii ya ubabe ubabe.Waasisi wetu walisimama kidete kupigania haki,usawa na kukemea maovu ambayo watu wetu walikuwa wanafanyiwa na wakoloni, leo hii kuna baadhi miongoni mwetu wanajikweza na kujifanya wao ndiyo wakoloni wa kipindi cha sasa huku wakitumia nguvu za dola na mahakama kukandamiza na kuuwa wananchi wanyonge! na chakushangaza ni pale wale wanaoamua kukemea mambo hayo kwa kufanya maandamano wanaponyimwa haki hiyo na baadhi yetu tunashabikia uamuzi huo wakiwemo wachache hapa JF.Hii siyo sawa na si haki na kama mambo haya yakiendelea basi inabidi tufikirie njia mbadala kama aliyotumia samora machelli na vikundi vingine vya ukombozi katika kutafuta haki.
Na kwa kuanzia hapa hapa JF tuwapinge kwa sauti zote wale wanaondeleza propaganda za CCM na serikali yake katika kuwanyima wananchi haki zao za msingi.

-Wembe
 
Wembe, naona umekuwa mkali nadhani huu ni mpya umetoka dukani leo na hapa ndo kwanza umeanza kunyoa
 
Nakulilia Tanzania,

Hahaa.haaaaa...inabidi wembe uwe mkali kidogo kurudisha utu miongoni mwa waafrika.
 
I like the idea of revoking degrees, while on the subject can we also review doing the same for all UDSM graduates who compromised academic principles in signing fraudulent contracts?

Admittedly far fetched but worth the effort.
 
Pundit, unachozungumzia ni mambo ya "mkuki kwa nguruwe"... sidhani kama watapenda uelekezwe kwa "binadamu"...
 
I like the idea of revoking degrees, while on the subject can we also review doing the same for all UDSM graduates who compromised academic principles in signing fraudulent contracts?

Admittedly far fetched but worth the effort.

Pundit

It is ok!, but not only UDSM graduates.
 
I like the idea of revoking degrees, while on the subject can we also review doing the same for all UDSM graduates who compromised academic principles in signing fraudulent contracts?

Admittedly far fetched but worth the effort.

The idea is good but how can it be implemented? Especially now when we have graduates from universities all over the world?
 
Back
Top Bottom