Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,201
- 236
Lakini Museveni Na Kagame Ni Wauaji Wakubwa Pia Nao Wamepitia Udsm Kwanini Nao Wasiwajibishwe ?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naam ni aibu iliyoje kwa wasomi wa UDSM au vyama vya upinzani kutoandamana na kukemea ukiukwaji wa demokrasia na mauji ya wananchi wasio kuwa na hatia nchini Kenya.Tuko katika zama za uwazi na ukweli na hivyo vyama vya upinzani na wasomi ni lazima wawe mstari wa mbele kukemea,kufichua,kupinga na kuwakomboa wananchi ambao wengi wao hawana mtu wa kuwasaidia.
Hivyo basi mimi nawaunga mkono wasomi hao wa UDSM kutumia ujuzi wao wa kisheria,hekima na maono yao katika kukemea ufisadi,uvunjaji wa haki za binadamu,mauaji ya raia wasio na hatia, na ukiukwaji wa demokrasia nchini Kenya kwa kufanya maandamano yao Jumamosi ijayo.
Ni lazima waelewe kuwa serikali ya CCM haipendi uozo huo ufunuliwe na ndiyo maana imekaa kimya kama bakuli la maji! pia cha kushangaza kuna watu hadi hapa JF ambao kwa sababu wanazozijua nao wamechukua msimamo huo huo wa serikali ya CCM kushabikia na kuwanyima haki watanzania kufanya maaandamano ya amani kupinga umwagaji damu na maonezi wanayofanyiwa watu wa Kenya.Ni lazima tuelewe kuwa maisha ni haki ya kila mtu na hakuna mtu au chama au kabila linaloweza kunyima mtu kuishi.Hivyo basi tumeona mauaji yametokea nchini Kenya na hakuna hata sehemu moja inayosema kuwa wapinzani wa Kenya ndiyo waliwauwa wananchi hao.Hivyo suala la kuandamana kwa watanzania wakiwemo wasomi wa UDSM ni suala la muhimu katika kuonyesha msimamo wao katika kutetea haki za wanyonge popote pale duniani ikiwemo Kenya.
Hivyo wale wote ambao wamechukua ile propaganda ya serikali ya CCM na polisi wake ya kuwa maandamano ya amani ni ya kumpa support Raila na hivyo kupendelea upande mmoja wasutwe kwa sauti ya juu na fikra zao wenyewe kwa kuwa wameshindwa si tu kukemea maovu na udhalimu bali wanahalalisha mambo haya kutokea tena katika sehemu nyingine Afrika.
Afrika kama bara tumechoshwa na michezo hii ya ubabe ubabe.Waasisi wetu walisimama kidete kupigania haki,usawa na kukemea maovu ambayo watu wetu walikuwa wanafanyiwa na wakoloni, leo hii kuna baadhi miongoni mwetu wanajikweza na kujifanya wao ndiyo wakoloni wa kipindi cha sasa huku wakitumia nguvu za dola na mahakama kukandamiza na kuuwa wananchi wanyonge! na chakushangaza ni pale wale wanaoamua kukemea mambo hayo kwa kufanya maandamano wanaponyimwa haki hiyo na baadhi yetu tunashabikia uamuzi huo wakiwemo wachache hapa JF.Hii siyo sawa na si haki na kama mambo haya yakiendelea basi inabidi tufikirie njia mbadala kama aliyotumia samora machelli na vikundi vingine vya ukombozi katika kutafuta haki.
Na kwa kuanzia hapa hapa JF tuwapinge kwa sauti zote wale wanaondeleza propaganda za CCM na serikali yake katika kuwanyima wananchi haki zao za msingi.
-Wembe
May I respond to some people collectively..
Hivi unakumbuka kilichotokea kwenye uchaguzi wa Marekani mwaka 2000 ambapo George Bush alitangazwa Mshindi? Unakumbuka yaliyotokea Florida ya "hanging chad" na wadogo zake. Unajua jinsi gani Supreme Court ya Florida ilivyojaribu "kisheria" kumpa ushindi Gore ambapo baadaye wakawa thwarted na US Supreme Court ambayo nayo ikimpa ushindi George Bush. Unakumbuka Jaji Mkuu Rehnquist baadaye alijuta kwa Mahakama yake kuchukua kesi hiyo?
Lakini Museveni Na Kagame Ni Wauaji Wakubwa Pia Nao Wamepitia Udsm Kwanini Nao Wasiwajibishwe ?
The Law Society of Kenya accused electoral officials of "dishonesty and ineptitude", called Kibaki's swearing-in "null and void", and urged a fresh vote.
"Honorable Kibaki lacks legitimacy to govern and this is the cause of the problems that we are facing as a country."
[SIZE="3 JAMANI HUYU JAMAA VIPI YANI WEWE UNA HALALISHA WIZI????? NAKUSHANGAA, HATA UANDIKE PAGE KUMI ZA KUTUELEWESHA LAKINI YOU CANT CONVINCE US.
WHAT DO YOU WANT MY DAUGHTER AND SON TO LEARN FROM THIS????? YOU CAN STEAL AND STILL GET AWAY WITH IT.
WEWE UNATOA MFANO WA USA, IT REALLY HAS COST MANY LIFES BY BUSH BEING IN POWER WATU WAMEKUFA KWA AGILI THE DECISION HE MADE WHEN INVADING IRAQ, HATA UKIANGALIA UONGOZI WAKE ULIKUWA WA UWONGO UWONGO, HE WENT TO IRAQ UNDER THE PRETEXT OF FINDING WEAPON OF MASS DESTRUCTION NA HAZIKUWEPO ALIWADANGANYA KAMA ALIVYOIBA KURA. WEWE UNATAKA TUWE HIVYO? AND BY THE WAY USA IS NOT EVEN A GOOD EXAMPLE BECAUSE HAWAFUATI HATA MAELEKEZO YA UN, THEY USE DEMOCRACY WHEN IT SUITS THEM.
Wakuu,
Hivi niwaulizeni, kwa maoni ya kibinafsi, Mh. Jakaya Kikwete na Tanzania kwa jumla inawezasaidia vipi kwenye kutafuta suluhisho la kudumu kwenye crisis ya kisiasa iliopo Kenya kwa sasa?
Najua Mwalimu angekuwepo hai na mamlakani hangesita kujiuliza swala hili.
K-T
Tatizo la Kikwete na serikali ya Tanzania kwa sasa hivi ni kuwa wako kama wanaishi kwenye nyumba ya vioo. Kwa namna moja ama nyingine walishafanya kama yale aliyofanya Kibaka. Kukosekana kwa moral integrity baina ya viongozi wetu ni jambo linalowakosesha authority kwa kiasi kikubwa sana kaitika kushugulikia mambo mbalimbali.
Jambo ambalo Kikwete (na Museveni pia) angeweza kulifanya ni kumpa moyo bwana Kibaki kuwa awe statesman zaidi na kukubali uchaguzi urudiwe kwa vile hiyo ndiyo njia pekee inayoelekea kuondoa tension iliyozuka hapo Kenya. Endapo anaona uwezekano wa kushindwa uchaguzi ukirudiwa na hivyo kufedheheshwa, basi asigombee tena kusudi apewe heshima ya kuwa rais mstaafu; tena kwa sasa hivi ana kisingizio kizuri sana cha kutogombea.
Na huyu odinga yuko dar es salaam sasa hivi kwa mazungumzo na baadhi ya viongozi wa tanzania wakati mkapa ameelekea kenya kusulugisha mambo
Hivi Kila Mtu anaweza kusuluhisha mgogoro wa Kenya?
Wakuu,
Hivi niwaulizeni, kwa maoni ya kibinafsi, Mh. Jakaya Kikwete na Tanzania kwa jumla inawezasaidia vipi kwenye kutafuta suluhisho la kudumu kwenye crisis ya kisiasa iliopo Kenya kwa sasa?
Najua Mwalimu angekuwepo hai na mamlakani hangesita kujiuliza swala hili.