Kenya Election 2007: Outcomes

Kenya Election 2007: Outcomes

Wamesema Coast pia bado, kuna sehemu Coast ilikuwa ya ODM na nasikia nyingine ya Kibaki.

Pia kuna matokeo ambayo hata Mwenyekiti amekubali yamepikwa, sasa kama hayo yamepikwa, ana uhakika gani kama hata hayo mengine hayajapikwa?

Baada ya kuanza kutoa kauli hizo na huku akiendelea kutangaza matokeo nilimshangaa sana. Yule anajua nini kinaendelea na PNU wanafanya nini. Nadhani matokeo aliyoyazuia ni yale ambayo waliopiga kura wamekuwa wengi kuliko waliojiandikisha, lakini akasema hawawezi kufuta matokeo ya jimbo zima bali wataangalia vituo kwa vituo, na vilivyo na kasoro watavifuta, je ana uhakika gani hivyo vituo vingine hawakufanya madudu?

Kwanini asiombe zile fomu zilizosainiwa na mawakala wa vyama vyote kuthibitisha matokeo ya kituo? Yaani hapo ndipo nilipouliza huyu jamaa ni mtu wa wapi.

Eti returning officers wamelala mbele na matokeo na simu zao haziko hewani bado utaendelea kuamini matokeo watakayokuletea? Kwanza hao returning officers wanatakiwa kufungwa, kwanini aishie na matokeo ya uchaguzi? Hilo ni kosa linaloweza kuhatarisha vurugu kama ilivyotokea leo. Lakini kwa kuwa kapotea kwa maslahi ya Kibaki hakuna mtu atawauliza hao returning officers!
 
Ni kweli lakini majimbo yanayokuja yana kura nyingi za Kibaki, ndio maana nikasema Kibaki anaelekea kushinda.

In fact kura za mwisho walizotangaza, haziko kwenye hiyo jumla. Kwenye namba hizo Kibaki ana zaidi ya laki tatu na Raila ana zaidi kidogo ya 80,000.

Ukijumlisha unakuta Kibaki anaongoza kwa zaidi ya laki mbili.

....dawa ni kuondoa kibaki kwa no confidence vote,its clear wamecheza dirty game,na akishinda tuu watamsubiri kwenye house wammwage chini!
 
Tukiambiwa 'Africans are less intelligent', tunakuja juu. Inakuwaje?

Invicible,

Mjinga hawezi kila mwaka kuja na mbinu mpya za kuiba kura, hao wanaofanya hivyo wana akili ila wanazitumia kwa mambo mabovu badala ya kuzitumia kuleta maendeleo ya nchi zao.

Ukiangalia mabalaa ya Afrika, utagundua yanaletwa na wasomi ambao
badala ya kutumia usomi wao kujenga nchi, wanautumia kufanya mambo ya ajabu.
 
Tukiambiwa 'Africans are less intelligent', tunakuja juu. Inakuwaje?

Labda tuseme kuwa most or some of africans are less intelligent maana kuna wengi hapa inaonekana wana akili. Ninachoona hapa ni kuwa waafrika wengi kuna matatizo fulani ya akili na kinachofanyika hapa ni upuuzi mtupu.
 
....dawa ni kuondoa kibaki kwa no confidence vote,its clear wamecheza dirty game,na akishinda tuu watamsubiri kwenye house wammwage chini!

ili kufanikisha hilo lazima ODM iwe na number bungeni (nadhani 2/3). Kibaki nina uhakika hao wabunge wa vyama vingine atawapora wote wajiunge na serikali ili angalau kupunguza pressure toka kwa wapinzania. akifanikiwa kuwapora basi anaweza ku-survive!
 
Aljazeera TV (kiingereza) just now, RAILA anaongoza kwa kura 38,000 ikiwa 86% ya kura zimehesabiwa tayari.
 
....dawa ni kuondoa kibaki kwa no confidence vote,its clear wamecheza dirty game,na akishinda tuu watamsubiri kwenye house wammwage chini!

Je wana kura za kutosha kufanya hivyo bungeni? Watahitaji msaada wa Kalonzo. Nafikiri watahitaji wabunge at least 148.

Sheria ya Kenya inasemaje kuhusu vote of no confidence?

Si mnamwona huyo prof. kwenye TV? Anaongea utafikiri hakuna kitu cha ajabu sana kinachotokea. Anacheka kama huo ni mchezo wa wanasiasa, kumbe Kenya yote itaumia.
 
Baada ya kuanza kutoa kauli hizo na huku akiendelea kutangaza matokeo nilimshangaa sana. Yule anajua nini kinaendelea na PNU wanafanya nini. Nadhani matokeo aliyoyazuia ni yale ambayo waliopiga kura wamekuwa wengi kuliko waliojiandikisha, lakini akasema hawawezi kufuta matokeo ya jimbo zima bali wataangalia vituo kwa vituo, na vilivyo na kasoro watavifuta, je ana uhakika gani hivyo vituo vingine hawakufanya madudu?

Kwanini asiombe zile fomu zilizosainiwa na mawakala wa vyama vyote kuthibitisha matokeo ya kituo? Yaani hapo ndipo nilipouliza huyu jamaa ni mtu wa wapi.

Eti returning officers wamelala mbele na matokeo na simu zao haziko hewani bado utaendelea kuamini matokeo watakayokuletea? Kwanza hao returning officers wanatakiwa kufungwa, kwanini aishie na matokeo ya uchaguzi? Hilo ni kosa linaloweza kuhatarisha vurugu kama ilivyotokea leo. Lakini kwa kuwa kapotea kwa maslahi ya Kibaki hakuna mtu atawauliza hao returning officers!

Hii ilikuwa ni propaganda tu alifanya Kivuitu. kampeni zilitumia helikopita kwenda nchi nzima kwa kampeni kwa hiyo wangeweza tu kutumia ndege kwenda kuwatafuta hao agents.

Basi bwana, mzee kibaki atakuwa madarakani for next five years mpaka akifia ofisini kwa uzee akiwa namiaka karibu 80! unless court ibadili matokeo.
 
Aljazeera TV (kiingereza) just now, RAILA anaongoza kwa kura 38,000 ikiwa 86% ya kura zimehesabiwa tayari.

Hiyo ilikuwa kabla ya kura kama laki nne ambazo wametangaza nusu saa iliyopita. Nina uhakika kabisa na hili maana nimesikiliza hata mahojiano ya kwenye TZ. Kwa matokeo yaliyotangazwa, Kibaki anaongoza kwa karibu laki mbili.
 
Je wana kura za kutosha kufanya hivyo bungeni? Watahitaji msaada wa Kalonzo. Nafikiri watahitaji wabunge at least 148.

Sheria ya Kenya inasemaje kuhusu vote of no confidence?

Si mnamwona huyo prof. kwenye TV? Anaongea utafikiri hakuna kitu cha ajabu sana kinachotokea. Anacheka kama huo ni mchezo wa wanasiasa, kumbe Kenya yote itaumia.

Huyo profesa ni mkikuyu na anafurahia ushindi wa kibaki. kumbuka kbc ni tv ya serikali.

uwezekano wa kupata support ya kalonzo sio mkubwa sana labda hivyo vyama vingine. Hata hiyo vote of no confidence haina nafasi sana unless ODM ipate wabunge 120 au zaidi.
 
kuna bogus prof. hapa kwenye TV ananipa kichefuchefu
 
45 Minutes ago

ODM, PNU Claim Victory

The East African Standard (Nairobi)

NEWS
29 December 2007
Posted to the web 29 December 2007

By Abiya Ochola and Brian Adero
Nairobi

The outcome of the hotly contested polls appeared headed for a deadlock as the opposition leaders and government ministers both claimed victory.

The Orange Democratic Movement declared its Presidential candidate, Mr Raila Odinga, the winner, and asked President Kibaki to concede defeat and prepare to hand over power.

Kibaki's ministers and officials later called a press conference and announced The Party of National Unity candidate President Mwai Kibaki had won by over 300,000 votes.

The declaration came as violence erupted in Nairobi, Kisumu, Kitale, Busia, Mombasa and Kakamega amid fears that the Government had hatched a plot to rig Kibaki back to power.

Addressing a press conference at Norfork Hotel, ODM running mate, Mr Musalia Mudavadi, read mischief at the delay by ECK in releasing the final tally and warned the Government against exerting undue influence on ECK chairman, Mr Samuel Kivuitu.

"We are clear that ODM has won the election. The will of the people is now known. They have voted out Kibaki sending home at least 18 cabinet ministers including the vice president. They have elected over 91 ODM MPs. Raila Amolo Odinga is therefore the winner and the fourth President of the Republic of Kenya," he said.

According to the results released by the ODM National Voter Monitoring and Tallying System, Raila had won the election garnering 4,215,437 trouncing President Kibaki who came second with 3,748,261. ODM-Kenya's Kalonzo Musyoka came a distant third with 630,849.

The Party of Natinal Unity leaders said Kibaki garnered 4,533,181 votes against ODM candidate Mr Raila Odinga's 4,206,062 votes. Kangaroo results given by any Tom, Dick or Harry deserve every contempt," said the party spokesman.

Science and Technology minister, Dr Noah Wekesa, said the party will however wait for the official results from the Electoral Commission of Kenya. He said they were waiting for the results of three constituencies, Kajiando North and Matuga represented by minister George Saitoti and Chirau Ali Mwakwere respectively.s

Official results, however, showed Odinga heading for a win with 3.73 million votes or 49 percent from 159 of 210 constituencies. Kibaki had 45 percent.

Odinga had led early tallies, but as Kibaki began to narrow the gap overnight, the ODM leaders feared PNU was rigging the presidential vote.

In Kisumu and other pro-opposition western areas, looters targeted businesses owned by members of one community.

"We have just started. We will loot all shops and kill them on sight," Mr Richard Ondigi, 23, a driver, told Reuters.

In Nairobi, streets were deserted as businesses remained closed and public transport vehicles stayed away. Police patrolled the city and ECK center at Kenyatta International Conference Centre, Nairobi, remained a no-go zone.

ODM presidential running mate Musalia Mudavadi claimed the party had evidence that Kivuitu was under undue pressure to delay the results and cause disharmony.

"In view of the growing anxiety and restlessness in the country over the extended delay in releasing the presidential results by ECK, we call upon the President to acknowledge and respect the will of Kenyan people and concede defeat."

He further called on Kibaki to direct his officers to begin the process of a smooth handover.

He blamed the riots on "those withholding the results" and wondered why the ECK, despite its modern communication equipment could not complete the job on time.

Asked why the party had gone public to release the result and declare themselves winners, Mudavadi said ODM was sending a strong signal to its opponents not to doctor the results.

Mudavadi said the party was awaiting official ECK results before making another move.
 
Sio UCHAGUZI tena, just UCHAFUZI sasa!
Walishasema PNU: Kibaki tena.
Najionea mwenyewe sasa
 
well,kupunguza pressure ngoja nisubili final verdict ya hii kitu lakini nipo very dissapointed na this & that thing ambayo its a clear cut wameiba
 
NASISITIZA HILI: NAIKO NAANGALIA KIVUTI LIVE KWA KTN

1. HAJA TANGAZA KURA ZOZOTE KWA MUDA WA SAA NDIMA IMEYOPITA

1. AMESEMA ZIMESALIA ENEO BUNGE 18 SASA. UPINZANI WAMESEMA HESABU ISIENDELEE MPAKA PALE WALE MAAFISA WANAFIKI WALETWE HAPO KUDHIBITISHA KWANINI HIZI KURA KIBAKI ANAPATA NYINGI SANA KAMA KIVUITU AMEKUBALI ETI MATHIRA CONSTITUENCY KIBAKI KAPATA KURA NYINGI KULIKO NAMBA YA WAPIGAJI KURA WALIOSAJILIWA!
2. ANASIKILIZA HOJA ZA VYAMA ZOTE ZA SIASA HAPO UKUMBINI, PNU NA HATA ODM
3. VIONGOZI WANAMUOMBA AJITOKEZE KAMA STATEMAN NA AKUBALI KENYA IPO HATARINI HIVI SASA
4. ANAOMBA MUDA AFANYA MEETING NA WENZAKE
5. MATOKEO HAYAJATANGAZWA NA ZILE NILIPOSTI HAPO JUU NDIO ZA KUTOKA KWA ECK.
6. TUSUBIRI
7. WACHA NICOMPAILI HII NEWS VIZURI NIWALEETENI
8. NASISITIZA BADO RAILA YUPO MBELE.
10. FUJO IMEISHA UKUMBINI
11. HABARI KUTOKA MASHINANE ( SIZIAMINI) LAKINI NAAMBIWA NA WATU MBALI MBALI MIKOA YA ODM INAJITAYARISHA KWA LOLOTE....MNAJUA NINACHOZUNGUMZIA
12. HII SASA NI MCHEZO WA WANAUME KAMILI, KAPITULA ZIMEKWISHA VALIWA NA SASA UWANJA WA KENYA UTAJUA NANI NI NANI
13. KWA MAONI YANGU JESHI NDIO LITACHUKUA MAMLAKA, KWA MARA YA KWANZA KWA HISTORIA YA KENYA. WATCH THIS SPACE.

Tanzanian-Kenyan:
Tunaendelea kukushukuru kwa habari kemkem unazotuletea.

Ujumbe wako huu ni mzito mno. Tunawaombea ndugu zetu wa Kenya mambo yasiende huko ulikokuelezea hapo juu.
 
just the same old story about afrika!

another country in africa shifts from a peaceful and prosperous to a war torn country.
 
well,kupunguza pressure ngoja nisubili final verdict ya hii kitu lakini nipo very dissapointed na this & that thing ambayo its a clear cut wameiba

Hata mimi, naona nimepoteza siku mbili kusubiri ushindi wa Raila.

Mwenyekiti wa ECK amesema pamoja na kutangaza lakini hawatamtangaza mshindi wa urais mpaka wapitie hizo karatasi kujua kama kila kitu kiko OK.
 
Siamini yanayotokea Kenya hata kidogo! Hata kama ni kuiba wizi huu ni wa ajabu kabisa. Huu wote ni woga tu, kuna watu waliapa Jaramogi au mluo mwingine yeyote hawezi kuwa Rais wa Kenya. Watamtangaza leo na kuapishwa kesho asubuhi mtaona tu.......

Inashangaza sana
 
Tanzanian-Kenyan:
Tunaendelea kukushukuru kwa habari kemkem unazotuletea.

Ujumbe wako huu ni mzito mno. Tunawaombea ndugu zetu wa Kenya mambo yasiende huko ulikokuelezea hapo juu.

Kweli Tanzanian-Kenyan, ametufaa kweli kweli. Tunakushukuru sana mkuu. Tunakuombea
ubaki salama na usipate na janga lolote kama matokeo ya uchaguzi huu.

Tunawaombea Wakenya wote amani maana hiki kipindi kitakuwa kigumu.

Ila kama Kibaki ameiba, hatakiwi kuachiwa nchi hivi hivi.
 
Back
Top Bottom