Kenya: Hakuna pasu kwa pasu tena, Mahakama imeamua wanandoa wanaoachana kila moja achukue chake au kuonyesha ushahidi wa mchango wa mali ya kugawana.

Kenya: Hakuna pasu kwa pasu tena, Mahakama imeamua wanandoa wanaoachana kila moja achukue chake au kuonyesha ushahidi wa mchango wa mali ya kugawana.

Kwani kwa nchi yetu utaratibu wa kugawana machumo ni wapasu kwa pasu au unazingatia uchangiaji wa wahusika.
Naomba kuelimishwa hapa
 
Ubaya wake kila mtu atakuwa anaendeleza kwake.

Mwanaume anajenga na mwanamke anajenga kwake.

Ndani kutakuwa na mgawanyiko wa hiki ni changu na kile ni chako.

Ndoa inaanza kugawanyika siku ya kwanza baada ya kufungwa.
 
Mahakama ya juu nchini Kenya imesema kuwa sheria mpya kwa wenzi wa ndoa wanaoachana itawanyima haki ya moja kwa moja ya kugawana asilimia 50 kwa 50 ya sehemu ya mali ya ndoa baada ya talaka, bali hivi sasa kila mtu atapaswa kuondoka na kitu chake alichotafuta kwa jasho lake, hata kwa mali za kugawana kuwe na ushahidi wa kina juu ya mchango wa kila mhusika.

Ni hatua nzuri sana, ndoa za kimkakati zitapungua, Kuna wale wanawake wenye tamaa ya pesa huwa wanaingia kwenye ndoa kwa lengo la kuja kuvuna mali kirahisi kwa mbeleko za pasu kwa pasu, uoga wa kulazimisha ndoa iliyoshindikana kwa kuogopa kugawana mali nako kutapungua. wanawake waliotokea familia masikini wataepukana na ndugu wanaowashawishi wavunje ndoa ili familia ipate pesa.
hakika
 
Kweli bwana maana mwanaume unapigana yeye yupo bize kusafishwa kucha bado ndani maugomvi mambo yakienda vizuri anaanza kukuvizia utangulie mbele ya haki ama mgawane, ije tu ili mkitalakiana akaendelee na kucha zake huko, pia swala la 50/50 litakuwa limefanyiwa uvumbuzi kuli sasa.
Kwa nini wakuvizie sasa? Wanaume wengi wanakufa natural deaths kutokana umri. Unakuta mwanaume amemzidi miaka 9+ mke wake, hapo probability ya mume kutangulia inakuwa kubwa sana.
 
Back
Top Bottom