Kenya: Hakuna pasu kwa pasu tena, Mahakama imeamua wanandoa wanaoachana kila moja achukue chake au kuonyesha ushahidi wa mchango wa mali ya kugawana.

Kwani kwa nchi yetu utaratibu wa kugawana machumo ni wapasu kwa pasu au unazingatia uchangiaji wa wahusika.
Naomba kuelimishwa hapa
 
Kweli bwana maana mwanaume unapigana yeye yupo bize kusafishwa kucha bado ndani maugomvi mambo yakienda vizuri anaanza kukuvizia utangulie mbele ya haki ama mgawane, ije tu ili mkitalakiana akaendelee na kucha zake huko, pia swala la 50/50 litakuwa limefanyiwa uvumbuzi kuli sasa.
 
Ubaya wake kila mtu atakuwa anaendeleza kwake.

Mwanaume anajenga na mwanamke anajenga kwake.

Ndani kutakuwa na mgawanyiko wa hiki ni changu na kile ni chako.

Ndoa inaanza kugawanyika siku ya kwanza baada ya kufungwa.
 
hakika
 
Kwa nini wakuvizie sasa? Wanaume wengi wanakufa natural deaths kutokana umri. Unakuta mwanaume amemzidi miaka 9+ mke wake, hapo probability ya mume kutangulia inakuwa kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…