Kenya imecheza sana ujasusi wa kiuchumi dhidi ya Tanzania. Should this necessarily be "quid pro quo"?

Kwenye work permit mama asijaribu,huku tayari wakenya wengi sana kwenye mahoteri ya kitalii kuliko watz na sisi hawawezi kutupa ajira huko.
Ni lugha za kisiasa tu.
Wahuni wa Kenya hatuwezi kuwapa free movement hapa kwetu
 
Shame on you greedy Kenyan
 
Hahahhahhaahhaha
 
Reactions: SMU
Hivi wakati wa mwendazake kwanini Uhuru aliruhusu watanzania na raia wengine wa afrika mashariki kuingia Kenya mpaka Nairobi kufanya biashara? Au mmeshajisahaulisha?


Hii ilikuwa 2017 tunaweza kuendelea...
 
Unasema haya kwakua unaweza simama mwenyewe au unategemea favour za system na zikibadilika una dondoka!
 
Ndivyo tulivyolelewa toka awali.. matajiri waliitwa makabaila, mabwanyenye, wanyonyaji... wakanyang'anywa kila kitu ili tubiendeshe wenyewe mwisho wa siku vyote vilibaki chakavu huku nchi ikiwa taabani kiuchumi!!! Tumejisahaulisha!!!
Roho mbaya na chuki havijawahi kumsaidia mafanikio hasidi yeyote yule...
 
Utajiri wa halali ni mzuri ila ule wa kukwepa kodi hakika ni wa kupigwa vita na kila mtu
 
Hahahhahhaahhaha
Yaani ujinga, roho mbaya na 'wivu wa kike' walionao Watanzania ni wa ajabu kabisa. Wako radhi kuendelea kuishi maisha duni kuliko kuruhusu biashara itakayowapa ajira. Hivi Magufuli amepita na kauli mbiyu 'tumeliwa sana' imekuwa nongwa. Sababu kuu ni ujinga, elimu duni na kujifungia au kufungiwa Kilugha usione dunia yaelekea wapi.
Mbona uhuru wa biashara na kuondoa visa upo baina ya Kenya na Rwanda? Tofauti ni kuwa Rwanda wanajiamini kwa vile wana wasomi wengi. Hili tatizo la elimu lisipotatuliwa hakuna matumaini kwa Watanzania kuwa na hali bora ya maisha. Maana hata wakijenga Gas, SGR nk watakaokuja fanya kazi kubwa si Watanzania. Tayari sekta ya hoteli ikifunguliwa leo Mtanzania utakutana naye chooni akifagia tu. Badala ya kuikaba serikali izidishe juhudi na kuweka fedha nyingi katika elimu na training.....wenye maono mafupi wanawalalamikia jirani 'kwa elimu yao'!
 
Watanzania wanajiamini sana tena ni wasomi kweli kweli.
 
Reactions: Ame
Ukweli mchungu huu,sasa ni kama tunaanza moja,
Tuliongozwa na wajinga wenye mawazo ya kimasikini,

Walioamini kila mwenye hela ni mwizi, na matatizo /umasikini wao umesababishwa na wenye hela,

Hakika Kama mateso tuliyapata hasa
Waliokuwa na hela walikuwa percent ngapi na wakati huo social services zilikuaje? Unatakakusanya kodi kwa wengi kisha watumiaji wawe kundi la wateule?

Msimpoteze Mh. Rais mnao waimba kila siku ooh sukuma gang etc ndiyo population kubwa Tanzania, ndiyo ambao kweli waki gang up wanaweza sababisha distabilization kwa nchi hii...Tuache uchonganyishi na tuache kupenda kubebwa bebwa ki makundi, kila mtu afanye kazi na ale jasho lake lakini kuwe na fair competition...Msijidanganye, Tanzania haina mwenye hati miliki kila mzaliwa wa Tanzania ana haki hiyo na anaweza akapewa nafasi ukashangaa hayo unayoyatazamia yakafutika kwa siku moja...

Tuipende nchi yetu, tuwapende raia wenzetu na tuheshimu viongozi wetu....Ibaada tumpe Mungu pekee ajuaye kesho ya kila moja...Aweza kumdhili huyu na kumpandisha yule!
 
Safi sana mkuu. Hakika kipande hiki kimeugusa moyo wangu.
 
Reactions: Ame
Summarize ujumbe wako basi tupate maana
 
..nipe mfano wa " ujasusi wa kiuchumi " uliofanywa na Tz au Watz na unieleze jinsi ulivyotusaidia.
elimu ya uraia hainipi nafasi ya kusema, lkn amini zipo kazi zimefanyika hata wewe unajua
 
Tanzania inaweza kushindana na Kenya Ila watanzania hawawezi kushindana na wakenya
You put it very simple but precisely...Kenya kwa Tanzania lazima inashindwa kwakua serikali ya Tanzania ina nguvu kuliko corrupted and individualistic Kenya...Ila watu wa Kenya wameishi ubepari hivyo wale wenye muscles ndiyo watakao kuwa backed na mifumo ya serikali yao wakiwemo viongozi na makampuni yao ambao bila kuwawekea vizuizi wanaweza sababisha cartel na kuwezesha rushwa kushamiri...Hata hivyo kushirikiana nao siyo dhambi ila the how matters a lot!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…