Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

SGR na Nyerere Dam vikiisha Kenya watatafutana maana bandari ya Mombasa itakosa mizigo yote ya maziwa makuu!

Kenya elimu inafundishwa in English na kuiunga nchi na international transfer of capital , technology and international market maana Kenya wanauza nje bidhaa nyingi kuliko Tz sababu ya kuweza kuwasiliana in English

Kenya ni nchi masikini kuliko Tz ni suala la muda tu kuipita iwapo Rais atakomaa na miundombinu na kuzuia upigaji ambao tayari umeshamiri. Magufuli alishaipita Kenya katika ukuaji uchumi ila akafa kwasasa tumerudi nyuma!
 
Wakenya hawakufukuza Wazungu, mpaka leo ukienda maeneo kama Westgate kuna wazungu wanaishi kule,..sisi tulibaki na Wahindi.

Alafu Zamani nchi ya Kenya ilipeleka vijana wengi sana sana Ulaya na Amerika kusoma,..hiyo ilisaidia sana maendeleo ya Kenya mpaka leo.

Yote kwa yote Lugha(English),..sisi tulibugi kwny hili ndio maana wanatutesa mpaka hapa kwetu...
 
Kwenye ishu Lugha nakuunga mkono sana. Tumekwama hapo. Kiswahili hikihiki kilivyoweza kuenea Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania, ndio ingekua ni Kiingerza hicho, naamini tungekua mbali sana kwa mtanzania mmoja mmoja.
Kiingereza kinaongelea sehemu kubwa ya dunia ndicho hasa kinachounganisha mataifa mengi.
Wananchi tumekua kama mfanyabiashara bubu.
 
Sawa,ila hapo kwenye top 10 na sisi tukiwa #9 let me do my homework first
 
Hamuwalishi, hao sio watoto wenu.
Mnafanya nao biashara za mazao kama vile wao wanavyowauzia bidhaa nyingine za viwandani. Ndio maana wasipokuja kununua mananasi ya kutengenezea juice wanaoyazalisha wanapauka.
Halafu tunawalisha
 
Uliota ndoto nzuri,kalale tena
 
Umeandika pointless tupu,
Hujui sababu za wafanyabiashara kuikimbia bandari ya Dar es Salaam.
Hujui SGR ni mahususi kwa nini na itamalizika lini kufika hizo nchi zote za maziwa makuu.
 
Na still chakula wanategemea tz hilo halina ubishi
Hujajua tu walivyo wajanja kwenye kilimo,wanalima horticulture na floriculture wanauza nje kwa pesa nyingi sana then wanakuja Tz kununua mahindi tu huku kwenye akaunti zao wana mshiko wa kutosha uliotokana na mauzo ya nje ya nchi.
Nakupa mfano ,ekari moja ya mahindi piga ua garagaza huwezi toa milioni 3 ila ekari moja ya nyanya unaweza toa milioni 30,wanachofanya wanalima hizo horticultute wananunua mahindi,
 
Uvamizi uliopewa jina la muungano kwa Zanzibar utaendelea kuwatesa Watanganyika. Dua ya mwenye kudhulumiwa hairudi. Mumetuuwa sana na mnaendelea kutuuwa kila uchaguzi katika jitihada zenu Za kuweka kibaraka wenu. Wacha karma iwatese
 
Mjumbe umeanza hoja kwa kuachwa nyuma kimaendeleo lakini ushahidi wako ni ramani ya nchi, mbona haviendani? Vipimo vya maendeleo viko, GDP, per head, electrification, life expectancy, budget ya afya, elimu na huduma, vitu kama hivyo. Una hizo data?
 
Uchumi wa Tz upo Top ten ila uchumi wa Kenya ni mkubwa karibia mara 2 ya wa Tanzania. Uchumi wa Kenya ni mkubwa sawa ukilinganisha na nchi za zamani za Africa Mashariki kwa pamoja (Tanzania, Uganda, Rwanda na Burundi).
Usijisifie umekuwa wa pili darasani ukiwa na D wakati aliyekutangulia ana B+
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…