Kenya imeiacha Tanzania parefu sana kimaendeleo, shida ni nini?

subutu eti magufuli alikuwa ameshawapita aliwapita kwalipi labda kuminya democrasia unadhani kenya wao wamelala au wameridhika na hali yao lah sisi tumejenga bwawa la nyerere lenye 2100mgwatt wakati kenya wao wanaanda kinu cha kuzalisha umeme wa kutumia urenium itamalizika 2034 watazalisha mgwt 35,000sasa wewe utawapita wapi wanarusha chombo agani wana viuo vingi na sekondary nyingi kuliko sisi mtaala wao wa elimu uko juu wakulima na wafugaji wanafuga kisasa wanauza nyama nje na mazao mengi wana export shirika lao la kenya airways liko hai wanapokea watalii wengi kwakuwa na hotel zenye hadhi kenya wako juu ndugu hujatembea kenya vizuri gata mji wa turukana uko juu kuliko mji wa Tabora japo ni jangwa
 
Tanzania iko buzzy kupinga ushoga mtandaoni, na kuacha kushughurika na mambo ya msingi, huku kutwa kukicha kwenda kwa mashoga kupiga magoti na kuwalamba miguu wawape msaada na mikopoo.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wakenya wanaotamani bongo ni wale wanaoona fursa nyingi huko kwakuwa wengi wamelala na duniani kote maskini wapo hata burney inayo masikini na matajiri tukubali kenya imetupita sana mkuu hujatembea bongo vijiji bora jehanamu
 
Watu wenye kiwango chako cha akili ndio walioletewa yale mabehewa chakavu!!

Huwezi kutoboa kwa akili kama zako za kijamaa!

Kwasasa world economy is characterized by competition, lazima tuipite Kenya kiuchumi na sio mbali sana!! Soma data za WB nimeweka utaona foreign investors wanatua tz sio kenya tena!!
 
Hapa umeconclude man, umeandika kitaalam zaidi nq ndio hali halisi ya Kenya kwa anaejua
 
mimi na wewe na maguma kama siyo wewe unasifia ujamaa na viongozi wako wa ccm wanalogwa na kukimbiza mwenge nimeishi kenya vijijini na mijini nimeishi uganda vijijini na mjini nimeushi japan vijijini na mjini na tanzania nimeishi vijijini vingi vya shida sisi tukubali tumepitwa tunazo resimali lakini sifuri tunataka katiba mpya ndiyo tunaweza kuwakuta wakenya ndugu
 
Wananchi wanalia njaa Kila siku, Kenya tajiri ni tajiri na maskini ni maskini
 
Ni kweli kabisa, na mimi hutembelea Kenya mara nyingi. Wabongo wengi hapa watasoma hii mada kuwa Wakenya wana viwanda vingi, majumba makubwa na barabara nzuri. Hivyo wanavyo. Lakini maendeleo hasa ya Kenya ni juu ya watu wake. Wakenya wako mbali sana kifikra na kielimu, kiasi ambacho Mkenya hu fit popote ulimwenguni. Maelfu ya Wakenya wafanya kazi Ghuba, tena siyo kazi za kufagia tu...kuendesha ndege, mabenki, polisi, jeshini... (kazi ambazo Mtanzania hata kuziomba hawezi!) Na hivyo hivyo Ulaya na Marekani.
Watanzania ni wafinyu wa upeo wa ulimwengu, waoga, wachache wa elimu....kwa ujumla 'binadamu Mtanzania amejawa na shida, hofu na mashaka'. Ikitokea kwamba amekwenda nje, aghalabu ni hizo kazi za maboksii, kuosha wazee....ndiyo, pengine wawili watatu watakuwa tofauti.
Nitasema tena: hii inatokana na utawala wa muda mrefu wa vitisho na ukandamizaji- police state, unaoendelea hadi leo. Aidha elimu ya kujua kusoma na kuandika tu (hata hiyo siku hizi ni mbinde). Nakubali maneno ya mchangiaji hapo juu 'Tanzania is doomed to be poor.
Watasema tuko uchumi wa kati, hahahahaa! Ni nani huyo? Sijakutana na Mtanzania wa uchumi wa kati miye!
Nini kifanyike?
Si vyema kulaumu tu bila kutoa ufumbuzi.
1- Tupambane kuleta katiba mpya. Bila ya hii hatutoki. Maana tatizo kubwa la Tanzania ni siasa na uongozi. Viongozi mbumbumbu wenye madaraka makubwa ya kupita kiasi, huchagua mbumbumbu wenzao katika sehemu nyeti. Tukiliondoa hili, tukapata viongozi weledi wenye madaraka yatokayo kwa umma, tutakuwa tumepiga hatua ya mwanzo.
2- Kubadilisha kabisa mfumo wa elimu. Ikibidi tu copy and paste mfumo wa jirani zetu uliofanikiwa. Tulete walimu kutoka Kenya, Uganda, Zimbabwe, nk kwa miaka mitano. Wakati huo tunarudia kuwa train walimu wtu na hatimaye tuchague wenye sifa tu. (Ndiyo, tutumie matrilioni, hata ikibidi tukope).
3- Kuvunjwa kabisa kwa jeshi la polisi na kurudia kulisuka upya, kupata polisi wenye elimu ya kiraia na wenye maadili.
4- Kupambana na rushwa ikiwezekana adhabu ya kifo kwa atakayeiba, kula rushwa ya sh. milioni 20 na kuendelea. Hawa ni wauaji kama wauaji wengine, isipokuwa madhara ya mauaji yao hayajulikani (can't be quantified)
Utaona hapo nimejikita kwenye kumtengeneza mtu kwanza, kabla ya vitu.
Sasa endelea......kuleta mapendekezo ya kilimo, biashara, viwanda nk.
Tukiweza, hayo yatakuwa maendeleo ya kweli.
 
Yote hayo ni uongozi legelege.Tulianza kuelekea pazuri baadae tena nchi imevurugwa.
 
Yes, you are very right...

Tena Kenya sera zao, sheria zao za kibiashara ziko very flexible...

Kule biashara zote; mfano banking, maduka, supermarkets, transportation nk nk ni 24hrs, 7days a week...

Hakuna business restrictions za kipuuzi kama ilivyo hapa kwetu Tanzania...

Yaani serikali inawawekea watu vikwazo vingi vya kibiashara na ufanyaji kazi na wakati huohuo serikali hiyohiyo inawekekea watu wake tozo na kodi za kufa mtu za kila siku...

Hebu ona tu tatizo la umeme na maji yanavyorudisha maendeleo ya watu na nchi nyuma huku viongozi wakionekana kama kutojali chochote...

Haiwezekani tukawa hatuna vyombo vinavyo forecast mbele kujua kuwa zisipochukuliwa hatua A, B, na C sasa miaka miwili kutakuwa na shida ya maji au umeme ili hatua zichukuliwe kabla ya tatizo kutokea. Serikali ya Tanzania ni defensive zaidi kuliko kuwa offensive...

Mimi nasema moja ya tatizo linaloi - disqualify CCM na serikali yao ni namna wanavyo-deal na changamoto ya maji na umeme..

Yaani ni kana kwamba tulikuwa vitani au hatukuwa na serikali before...!

Ukirudi tena kwenye maswala ya biashara, ni matatizo matupu...

Mfano sheria ya kulazimisha biashara ya bar na maeneo ya starehe, usafirishaji wa abiria kutofanyika masaa 24 ni ya nini...?

Jamani, ni kweli tupende tusipende shida za umasikini na udhaifu wa uchumi wetu ni la kimfumo zaidi...

Mfumo huzaa tatizo la kiuongozi na hawa viongozi ndiyo hutuandalia sera na mipango ya hovyo inayozaa matatizo haya...
 
Hapo kwenye kilimo mbona umetupiga mkuu,60% ya chakula kenya wanategemea Tanzania,kilimo gani walichotupita wakenya!?

..wenzetu wanafuga kisasa zaidi.

..wanaongoza Afrika Mashariki kwa kuzalisha maziwa ingawa Tanzania inaongoza kwa idadi ya mifugo.

..pia tuna mengi ya kujifunza toka kwao ktk kilimo cha mbogamboga na matunda, kuongeza thamani ya mazao, na ku-EXPORT.
 

..nadhani lugha ya Kiingereza inatunyong'onyeza tunaposhindanishwa na Wakenya kimataifa.

..pia unaweza kukuta wasomi wetu sio wazuri ktk kutumia tehama, lakini nadhani hiyo gap imepungua sasa hivi.

..ukija kwenye mtaala naamini mtaala wa NECTA ni mzuri na mgumu kuliko mtaala wa nchi zote Afrika Mashariki.

..Kwa hiyo Mtanzania akishachangamka kwenye lugha na tehama majirani lazima wakae chini.
 
Huijui Kenya, na hata kusoma habari zake unazisoma lakini huzielewi.

Nina hamu sana ya kukujibu kwa kirefu, lakini sina muda wa kufanya hivyo sasa hivi.

Nikushauri tu kwa sasa hivi, ondoa kasumba kichwani mwako kwanza. Fungua akili uelewe mambo kwa uhalisia wake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…