Kenya inaongoza uzalishaji Avocado Afrika. Tusipokuwa makini chini ya CCM kuna siku Kenya itailisha Tanzania

Nyie endeleeni kuwekeza watu wawe kama wakina mwijaku,baba levo,manara na tktk zingine
Wakata mauno tu

Ova
 
Kuwauzia sio hisani kwao. Ni biashara ambayo tunaiihitaji kuboresha maisha na uchumi wetu. Mbona hujawaza iwapo wakigoma kununua hali itakuwaje kwa wakulima?
 
..Majirani wako makini kwelikweli ktk masuala ya kilimo, na wanazingatia viwango.

..angalia video hizi mbili kuna mengi ya kujifunza kuhusu namna ya kufanya kilimo.


Hawaongozi kwa uzalishaji wa parachichi Afrika. Wao wanachofanya ni kuja kwenye Nchi kama Tanzania wanalangua, halafu wanaweka nembo za kuwa zinazalishwa Kenya.
 
Wanalangua parachichi Tanzania, wanaenda kuweka label kama zimelimwa Kenya. Nenda Njombe pale wana ofisi za kununua parachichi wanapeleka Kenya. Zikifika Kenya wanasema zinalimwa Kenya
 
Mkuu upo sahihi juzi kati nilikuwa kwenye wilaya zote za Tabora wanalalamika asali imeshuka bei na wanunuzi wakubwa ni Kenya so tunategemeana
Naam, hiyo ndio hali halisi. Tatizo kuna mentality imeingia miongoni mwa wengi kana kwamba tunafanya hisani kuwauzia mazao. Uchumi ni kutegemeana kati ya nchi na nchi. Wao wanafaidika na sisi vilevile. Juzi tu waliacha kununua mahindi kwa kisingizio ati mahindi yetu yana sumu kuvu, ilikuwa ni mtafutano kwa wakulima mpaka rais Samia na mwenzake wa Kenya waliposawazisha mambo. Wote tuheshimiane kwa kuwa tunategemeana.
 
Wanalangua parachichi Tanzania, wanaenda kuweka label kama zimelimwa Kenya. Nenda Njombe pale wana ofisi za kununua parachichi wanapeleka Kenya. Zikifika Kenya wanasema zinalimwa Tanzania
Uko sawa ,hawa watu wanashindwa kuwa Kenya wanatembelea kwa mgongo wetu mfano,Mlima Kilimanjaro husema ni wa kwao,Mbuga ya Serengeti,kilimo cha mpunga,mahindi,parachichi,ndizi,ng'ombe,mbuzi na hata samaki.
 
Uko sawa ,hawa watu wanashindwa kuwa Kenya wanatembelea kwa mgongo wetu mfano,Mlima Kilimanjaro husema ni wa kwao,Mbuga ya Serengeti,kilimo cha mpunga,mahindi,parachichi,ndizi,ng'ombe,mbuzi na hata samaki.
Ndio wamewazidi akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…