Kenya inaongoza uzalishaji Avocado Afrika. Tusipokuwa makini chini ya CCM kuna siku Kenya itailisha Tanzania

Kenya inaongoza uzalishaji Avocado Afrika. Tusipokuwa makini chini ya CCM kuna siku Kenya itailisha Tanzania

Sisi ni kuwasha mwenge kulikotutoa akili au kitu gani? Mbona hatuna focus na chochote?

..wakulima wa avocado wa Tanzania wamehangaika bila msaada wa serikali na wataalam kwa muda mrefu.

..wenzetu wa Kenya wanapata msaada wa kitaalamu ktk kila hatua mpaka kufikia hatua ya kuuza nje.
 
..Majirani wako makini kwelikweli ktk masuala ya kilimo, na wanazingatia viwango.

..angalia video hizi mbili kuna mengi ya kujifunza kuhusu namna ya kufanya kilimo.




Kenya hawana lolote, wanategemea parachichi za Tanzania. Tuache uvivu wa kutafuta masoko, tukiacha kuuza parachichi zetu Kenya exports za Kenya zitashuka
 
..hayo unayosema yamefanyika ni mambo mazuri na tunayaunga mkono.

..swali ni kwamba; ikiwa madaraja, barabara, hospitali, vyuo, nk, vinajengwa kila mahali, kwanini Watanzania bado tumekwama?

..Tanu/ Ccm imekuwa madarakani toka tupate uhuru hivyo inastahili lawama kwa mkwamo huu.
NIMEKUSOMA WE NI MWELEWA SANA UNAJIBU KWA HOJA VZR SANA ILA TUSILINGANISHE MAMBO KWA URAIS SABABU KILA AWAMU INA MAMBO MAZURI IMEYATENDA CHA MSINGI NI KUCHANGIA KWA KUTOA MAWAZO NINI KIFANYIKE NA JINSI YA KUKIANZA ICHO UNACHOWAZA ,UBARIKIWE SANA
 
Kumbuka Parachichi nyingi wanachukua Iringa na Mbeya wakifika kwao wanaziosha vizuri na kufanya packing wanaita za kwao wanakwenda masoko ya kimataifa... sisi tunaendelea kuwa watazamaji
KWELI UMEJIBU VZR NAKUSHAURI UTOKE KWENYE NAFASI YA UTAZAMAJI UFANYE IYO KAZI WW ILI KUONDOA MALALAMIKO PIA KWA KUFANYA IVO NAJUA UTAZALISHA AJIRA KWA WATANZANIA WENZETU NA KUKUZA KIPATO CHAO
 
na ndio role models wa madogo wengi, siku moja napita mitaa ya kinondoni nimepishana na mijamaa miili mikubwa ila stori zao sasa, mara diamond hivi mara vile nikasema duuh kazi ipo!
Heri ya mwaka mpya mwamba

Hahaha cmnt yk nmecheka sana

Kweli bongo sisi tunaongoza kwa kuwatoa wakata mauno tu sahv

Ova
 
EeenHeeee!
Hivi unajua ulichoandika hapo?
"Wakigoma"? kwani walipoweka ngumu kuhusu mahindi yetu kuwa na 'aflatoxin' hawakuwa wamegoma? Na hiyo ilikuwa siyo mara ya kwanza, au haya mambo wewe huyajui!
Soko hawana wao pekee yao kiasi kwamba wakigoma hatuwezi kuuza bidhaa zetu kwingineko, kama wao wanavyoweza kwenda kwingine, wakitaka.
NADHANI CHA MSINGI NI KUJIULIZA WAO WANAWEZAJE KUFANYA IVO CC TUNAKWAMA WAPI KAMA MTU MMOJA MMOJA ALAF KUTOKEA HAPO TUCHUKUE HATUA TUSIWE WATU WAKULALAMIKA NDUGU ZANGU
 
NADHANI CHA MSINGI NI KUJIULIZA WAO WANAWEZAJE KUFANYA IVO CC TUNAKWAMA WAPI KAMA MTU MMOJA MMOJA ALAF KUTOKEA HAPO TUCHUKUE HATUA TUSIWE WATU WAKULALAMIKA NDUGU ZANGU
Hueleweki unachochangia hapa!

Kwani ni lazima tufanye wanayofanya wao, sisi hatuwezi kufanya mengine tunayoona yanatufaa?

Walkilima parachichi, na sisi haraka haraka tukimbilie huko, kwa nini?

Wakikimbilia nchi za nje kwenda kuwa mayaya, na sisi tuhimize vijana wetu watoke kwenda kuwafanyia watu kazi za ndani?

Kwa nini watu mnapenda sana kushikiwa akili kiasi hiki?

Panua akili yako, fanya unayoweza kufanya kwa ufanisi ufanikiwe, siyo lazima uige kila wanachofanya wengine.
 
Back
Top Bottom