Kuna kipindi nilikua natakiwa Kusafirisa Gallstones kwenda Hong Kong, nimeenda Fedex wakanambia nije na Vibari vya Serikali, nikaenda Wizara ya Kilimo, story zikawa mingi kama unavyosema, nikarudi Fedex kuwaeleza changamoto nilizokutana nazo Wizara ya Mifugo, Fedex wakanishauri niende tu kwa Mkemia Mkuu kufanya kipimo then watanisafirishia kifurushi changu kwa Documents toka kwa Mkemia!
Kufika kwa Mkemia, hawajui Gallstones ni nini, issue yangu ikawa kubwa hivi mpaka kukutana na Mkurugenzi wa kitengo fulani, kujieleza.....!
Sasa safari zote hizo nafanya na Business Partner raia wa Nje, akaanza kuniuliza, Mbona hii Tanzania iko very Complicated hivi!?
Hizi Stones mm husafirisha kila siku kwenda Nje, kwa nchi yangu sihitaji Documents yoyote ku export hizi stones, Coz Serikali yangu inajua nauza nje, ntalipwa Dollas, ntafanya kitu Nyumbani.....!
Nikamwambia sio Tanzania, wafanyakazi wengi wa umma wamekua kama Jokala Mdimu...