KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Habari!
Watanzania tumekuwa tukililia kuwa na tume huru ya kusimamia shughuli yote ya uchaguzi kwa kusema kuwa NEC haina. Hivyo wengine kudiriki kusema iko controlled na walio ktk dola kuweka matokeo kutokana na matakwa ya walio ktk dola.

Wenzetu wa Kenya wana IEBC kama tume huru ya kusimamia shughuli za uchaguzi. Ila ni wazi baada ya mahakama ya juu kutengua ushindi wa Uhuru Kenyatta ambaye alitangazwa na IEBC kuwa ni mshindi ktk uchaguzi ambao ilisemekana ni Free and Fair.

Mahakama kuu imetambua kuwa kuna udukuzi ulifanyika ktk mchakato ambao ulimwezesha Uhuru "kushinda", hivyo wametengua ushindi huo.

Je baada ya kuwapongeza sana wakenya kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi, je ni kweli kuwa na tume huru kutaleta matokeo huru?? Je tume huru italeta mgombea aliyechaguliwa na wananchi kihalali??
Ni wazi tume hii haiko "huru" maana imeingiliwa na ni wazi wajumbe wake wamehusika!!

Je kwa haya ya Kenya, je NEC huru ni moja ya solution ya uchaguzi huru na wa haki??
Sis bado...Bongo bahati mbaya!
 
Hahahahahaa the highest point of hypocrisy
 
muwakilishi wa uhuru kenyatta kwa upande wa JF ndg MK254, pole sana kwa yaliyotokea....ila hakuna namna,mahakama ya upeo(supreme court) imeshaamua.

kutaneni tena kwa debe tarehe 31 october au tarehe 1 november.

twawatakia amani katika kipindi chote cha kuelekea duru ya pili ya uchaguzi.
 
Wakuu Salaam
Kama Afrika naona tunasonga mbele na kuheshimu maamuzi ya vyombo vyetu mzee wetu jecha alionyesha njia kua uchaguzi wenye dosari ufutwe na kenya wameiga sio kukalia kimya kitu chenye dosari.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama Jecha nae ni Shujaa siku hizi basi nina imani BAKITA watakua wametoa tafsiri mpya ya hili neno.
 
Hata ukirudiwa Kenyatta atashinda tu
Hatuna shida hata Uhuru akishinda tena. Maana yake hata mahakama ingeliamua kivingine, tulikuwa tayari na kuendeleza shughuli zetu za kawaida. Ile kitu kama taifa tunadai ni kujenga uwazi kwa kutekeleza majukumu ya kitaifa na kijamii kwa manufaa yetu na kizazi kijacho.
 
Inawezekana endapo tukiuana kwanza
Hapo ndio akili itakuja
Nalo si suluhisho, mbona huko kwenye tume huru na katiba mpya na democracy safi bado watu wameuana. Pamoja na hayo yote bado kuna kelele kila kukicha mkuu..

Kubwa hapa ni kupunguza siasa, tuwekeze kwenye maisha yetu zaidi kwa faida ya watoto wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mungu wangu, ina maana uchaguzi utarudiwa tena? gharama za uchaguzi? uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Mungu shusha amani yako kwa majirani zetu, kusitokee ghasia yoyote!
kama sipo mbali na mtoa post gharama nasikia ni juu yao sasa sijui inamaanisha nn mwenye kujua atujuze
 
Back
Top Bottom