Habari!
Watanzania tumekuwa tukililia kuwa na tume huru ya kusimamia shughuli yote ya uchaguzi kwa kusema kuwa NEC haina. Hivyo wengine kudiriki kusema iko controlled na walio ktk dola kuweka matokeo kutokana na matakwa ya walio ktk dola.
Wenzetu wa Kenya wana IEBC kama tume huru ya kusimamia shughuli za uchaguzi. Ila ni wazi baada ya mahakama ya juu kutengua ushindi wa Uhuru Kenyatta ambaye alitangazwa na IEBC kuwa ni mshindi ktk uchaguzi ambao ilisemekana ni Free and Fair.
Mahakama kuu imetambua kuwa kuna udukuzi ulifanyika ktk mchakato ambao ulimwezesha Uhuru "kushinda", hivyo wametengua ushindi huo.
Je baada ya kuwapongeza sana wakenya kwa kuwa na tume huru ya uchaguzi, je ni kweli kuwa na tume huru kutaleta matokeo huru?? Je tume huru italeta mgombea aliyechaguliwa na wananchi kihalali??
Ni wazi tume hii haiko "huru" maana imeingiliwa na ni wazi wajumbe wake wamehusika!!
Je kwa haya ya Kenya, je NEC huru ni moja ya solution ya uchaguzi huru na wa haki??