KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

KENYA: Mahakama yatengua matokeo ya Uchaguzi wa Rais. Kurudiwa upya ndani ya siku Sitini(60)

Mahakama kuu nchini Kenya imetengua matokeo ya uchaguzi wa raisi hivyo uchaguzi utarudiwa tena ndani ya siku 60 kwa mujibu wa katiba

1.Uchaguzi haukufanyika kwa taratibu zote zilizotakiwa kulingana na Katiba
2. Utaratibu haukufuatwa katika usafirishaji wa matokeo
3. Kulikuwa na kasoro kadhaa za uchaguzi


Sent using Jamii Forums mobile app
Du hao majaji lazima watapelekwa mikono salama ya chatu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HAPA
Kwa vile leo ni mapumziko na niliowataja wako majumbani sasa hivi basi sio vibaya wakafungulia Luninga zao na kuona Supreme court ya Kenya inafanyaje maamuzi yake kwa uwazi na bila woga kwa kesi ya Uchaguzi wa Urais wa nchi hiyo.
Nimefurahishwa sana na uwazi mkubwa unafanywa na mahakama hiyo ya Kenya na ni wazi tunalo la kujifunza kutoka kwao
NIPO NAFUATILIA HUKU, NGOJA TUONE NANI NI SHUJAA WA GAME HILI
 
Huu ndo UKUDA wa nchi za AFRICA, Vijana hawana AJIRA, Kina mama wanateseka, PESA ZOTE ZINAPELEKWA Kwenye UCHAGUZI Masikini WANATESEKA. Hata huo UCHAGUZI wa MARUDIO hautakuwa PERFECT

ukuda ni kuleta figisu na wizi wangeacha mambo yaende sawa yasingetokea haya
 
Mungu wangu, ina maana uchaguzi utarudiwa tena? gharama za uchaguzi? uwiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii. Mungu shusha amani yako kwa majirani zetu, kusitokee ghasia yoyote!
mafisadi wa kisiasa wanazungumziaga gharama ili wabaki madarakani kiharamu
 
Back
Top Bottom