Kenya the giant of Africa is sleeping and the sleeping giant of east africa is waking up!! Viva Tanzania

Asilimia kubwa barabara ni za vumbi miji mingi imechoka sana
Yaani Barabara nzuri zile za Miji Yao mikubwa kama Accra,Kumasi nk ni zimechoka? Interchanges Kali na nzuri Bongo hakuna.

By the way sio saana kama Ivory Coast
 
Nakuambia hivi hamna sekita tunao zidi Kenya acha mambo ya miradi tu, nakupa mfano fanya simple comparison btn kenya airways na air Tanzania tu uone.
Unalinganisha shirika ambalo lina miaka zaidi ya 20 ambalo linashare na guant kama klm na shirika linalofuliliwa,linganisha basi kilimo cha cha chakula kati yetu na hao jamaa zako
 
Kujilinganisha ni lazima na muhimu Ili kuona kama unafanya progress au hapama.

Maisha ni mashindano bila hivyo huwezi pata sense ya kupambana utaridhika au fursa zako kuchukuliwa na jirani.
I beg to differ...mimi siamini katika kujilinganisha ili kushindana but rather katika kuhakikisha malengo yangu niliyoweka nayatimiza na hii ni kwa sababu malengo huwa hayafanani labda kama mtu anafuata mkumbo. Mfano mimi malengo yangu makuu mwanzoni mwa maisha yangu ilikua kuwa na biashara itakayoniwezesha kupata steady income. Kwa kuwa sikuwa na kipato cha kuanza nikasema hata nikiajiriwa lazima nisevu ili kutimiza lengo langu. So wakati marafiki zangu wakianza na malengo ya kununua magari, kujenga nyumba mimi nili focus kwenye lengo langu mpaka likatimia. Hata ilipofika kununua gari bado sikuona kuiga wenzangu kununua magari ya fashion kama Harrier nk but kununua gari multipurpose kwa lengo la kuweza kulitumia kwenye biashara na shughuli zangu zingine...
 
Unalinganisha shirika ambalo lina miaka zaidi ya 20 ambalo linashare na guant kama klm na shirika linalofuliliwa,linganisha basi kilimo cha cha chakula kati yetu na hao jamaa zako
Mkuu air Tanzania ni kongwe kuliko Kenya airways ya miaka ya 2000s, wenyewe wanaufanisi mkubwa sisi uswahili ni mwingi sanaa.
 
Swala la kujilinganisha hususani Kwa Nchi au taasisi shindani haikwepeki bila kujalisha malengo Yako sawa au hapana.

By the way malengo ya Nchi ni welfare Kwa watu wake na Ili upate welfare hiyo lazima kukuza Uchumi shindani.

Utakuzaje uchumi shindani bila kushindana?
 
Mkuu air Tanzania ni kongwe kuliko Kenya airways ya miaka ya 2000s, wenyewe wanaufanisi mkubwa sisi uswahili ni mwingi sanaa.
sasa hilo ni tatizo lako kutafuta vitu ambavyo tuna struggle na kuringanisha na kenya!!
Ikogo hivo kuna vitu utafanya vizuri kuna vitu utafanya vibaya.
Huwezi kushindwa kote na huwezi kufaulu kote ishi nayo hii itakusaidia
 
Tuna export nini? Kama tuna import vijiti vya kuchokoa meno na viberiti wakati tunaexport chakula zaidi na mali ghafi ambavyo thamani yake ni ndogo sana naona haina maana yotote. Kama tungekuwa tuna export zaidi kuliko Kenya basi thamani ya pesa yetu ingekuwa inaimarika lakini badala yake tunaona pesa yetu inapromoka zaidi hata dhidi ya shilingi ya Kenya.

Vv
 
Mkuu air Tanzania ni kongwe kuliko Kenya airways ya miaka ya 2000s, wenyewe wanaufanisi mkubwa sisi uswahili ni mwingi sanaa.
Mkuu ww umekariri halafu hata kenya kwenyrwe hujawahi kufika
 
Uko sahihi ni vema haya mafanikio ya reflect upatikanaji wa maji elimu afya na kukua kwa biashara na sekta binafsi kwa ujumla
 
Uko sahihi ni vema haya mafanikio ya reflect upatikanaji wa maji elimu afya na kukua kwa biashara na sekta binafsi kwa ujumla
Mbona ndivyo ilivyo? Umeme Kila Kijiji tayari,Kila kitongoji kazi imeanza.

Maji Kila Kijiji kazi inaendelea by 2026 Kila Kijiji Kitakuwa na maji ya bomba

Afya na Elimu ndio usiseme
 
labda ugiant wa kukariri na kurecite Kuran …
 
Thamani ya TZS kwa KES imepanda sana katika miaka mitano iliyopita. Ilifuka hadi Shilingi 16 za Tanzania kutoka Shilingi 23 za Tanzania.
KES imeyumba.
 
Hakuna siku Changamoto zitaisha labda zitapungua.

Hamuwezi kushinda Kwa mipango ya kutumia Trilioni 11 kujenga Sgr ya kutoka Dom-Dar ,huku ni kupoteza pesa bila sababu za msingi.
Huu ni uongo, gharama za ujenzi wa Sgr from dar to dodoma aio trillion 11
Ni trillion 7
 
Hizi media unazoweka link ni media za hovyo, hao shamba media wameweka sudan namba moja kwa uzalishaji tumbaku. Sasa Sudan na tumbaku wapi na wapi

Pia bado hatujafika mauzo ya dola milion 400, maana hiyo ni zaidi ya trillion 1

Tupo kwenye dola million 130+, ambazo ni around bilioni 300+

Pia uzalishaji wa hizo tani ni makadirio sio kuwa tumezalisha. Mwaka huu uzalishaji umeshuka sana compared to last year sababu ya hali ya hewa
 
Mbona ndivyo ilivyo? Umeme Kila Kijiji tayari,Kila kitongoji kazi imeanza.

Maji Kila Kijiji kazi inaendelea by 2026 Kila Kijiji Kitakuwa na maji ya bomba

Afya na Elimu ndio usiseme
Umeme kila Kijiji bado hatujafika. Ila tutafika kazi inaendelea na inaridhisha

Nb; Hawa watu mara zote unaojadiliana nao huwa hawajui chochote?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…