Kenyatta anaposimama na Odinga, CHADEMA mnayo ya kujifunza

Kenyatta anaposimama na Odinga, CHADEMA mnayo ya kujifunza

Nachoona hapa ni uoga wa wanasiasa wetu kuwaambia ukweli wafuasi wao, hasa kuhusu masuala yenye ukakasi kama hili la ushoga.

Wanaogopa kupoteza wafuasi kwasababu jamii yetu kwa asilimia kubwa bado iko gizani, tunaishi kwa kujidanganya tunampenda Mungu kumbe ni unafiki tu wa kuficha madhaifu yetu mengine, kama vile dhambi iko moja ya ushoga pekee.

Wanajua wakigusa hapo kwenye ushoga watashambuliwa toka kila upande, hapa ndipo namkumbuka Fatma Karume anavyokuwa wembe kule twitter kusimamia kile anachoamini, bila kujali upinzani anaoupata toka kwa wajuaji.

Naamini ule uthubutu na upeo Fatma ameupata kwasababu ya kuishi kwake nje ya nchi kwa muda, najua leo tunamshangaa kwa msimamo wake kwa sababu ya ushamba wetu, ila iko siku ataonekana shujaa, ni suala la muda tu.
 
Jambo la kujiuliza ni kama Katiba Mpya itayatambua haki za makundi mbalimbali, na kama ikiyatambua vipi hawa wabishi wataiona Katiba Mpya imekosewa?

Kwasababu nikitazama hili jambo kwa upeo wao, ni kama wanaona hii nchi inaendeshwa kwa sheria za kidini, ndio maana wanatumia maandiko matakatifu kuwahukumu mashoga, wao wanasahau serikali yetu haina dini.

Haya mambo yanawahitaji watu kupanua fikra zao sana, ndio maana tumeachwa mbali na wazungu tunaowaona washenzi, kumbe sisi ndio wajinga tunaojidanganya kwa kujivika utakatifu ambao kimsingi hatuna, tumeamua tu kuishi gizani na kuridhika.
Kwenye mada suala la ushoga limetajwa tu kwenye kuweka msisitizo. Ushoga si msingi wa mada hii.

Mada hii Imekuwa ni mwendelezo ule ule wa kufuatilia kuona CDM kama chama tunakwama wapi? Mbona Kariakoo au machinga wanaweza?

Mbona Kenya wanaweza?

Mada inaweka bayana kuwa wenye kumhusisha Odinga na ukabila au upuuzi, imedhihirika wapuuzi ni wao. Ndiyo maana hakuna mmoja kanyanyua pua hapa.

Zaidi sana inawatambua wapuuzi wengine ni mashabiki wa urusi dhidi ya Ukraine, washabiki wa Israel dhidi ya Palestine, nk.

Kwamba Kama mfano, ni wapuuzi pia washabiki wote wa dhuluma yoyote dhidi ya haki yoyote hata kama haki hiyo ni dhidi ya mashoga.

Kwamba Chadema ni movement yenye msingi wa haki, makundi hayo ya wapuuzi hapo juu kama yapo chadema yamepotea njia.

Hayo ni Bora yakawahi Lumumba au yakasaidiwa haraka kwenda yanako belong Kwa kufurushwa unceremoniously!

Hai ndiyo wanaotucheleweshea kiu yetu ya kupata katiba mpya sasa.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Imekuwa ni kawaida kwa wajuaji uchwara wa bongo kumwona Raila kama mkabila na mpuuzi fulani.

How Ruto allies provoked Uhuru to get involved in politics

Kenyatta kusimama na Odinga njoo 2027 kama bado siyo funzo kwa wajuaji uchwara hawa watajifunza lini?

Cha kusikitisha zaidi baadhi ya wajuaji uchwara hao wamo hata ndani ya vyama tegemeo kama Chadema.

Watu wasiojua maana ya haki, wasioamini katika haki au wasiosimama na haki bIla kujali maslahi binafsi hawana msaada wowote katika chama au nchi.

Watu wenye kuwanyanyapaa wapalestina, waukraine, na hata mashoga hawawezi katu kuwa hazina kwa chama au taifa lolote lenye kuamini kwenye ustaarabu.

Ushauri wa bure kwa Chadema, fukuza watu wote wa namna hiyo mara moja. Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria kuliko kuwa na rundo la wasiojitambua.

Waende kwa mambuzi huko ambako kukalia haki za wengine kwao ni jadi.
Kuna kitu unataka kuandika lakini hujui uandike nini!
 
Kuna kitu unataka kuandika lakini hujui uandike nini!

Nilichokiandika ninakijua. Nimekiandika na rejea nimeweka.

1. Asemaye Raila ni mkabila na harakati zaje ni za kikabila ni mpuuzi.

2. Wapuuzi hawezi kusaidia katika Mapambano ya kudai haki.

3. Haki haina double standard.

3. Chadema ni movement ya haki.

4. Tunakwama Kwa kuwaendekeza wapuuzi chamani ambao si waumini wa haki.

5. Ni heri kuwa na wachache waliodhamiria kuipigania haki badala ya rundo la wasiojitambua.

Ninakazia ulichoandika wewe hukijui kama si kuwa hujitambui au kuwa utakuwa umeguswa!
 
Kwenye mada suala la ushoga limetajwa tu kwenye kuweka msisitizo. Ushoga si msingi wa mada hii.

Mada hii Imekuwa ni mwendelezo ule ule wa kufuatilia kuona CDM kama chama tunakwama wapi? Mbona Kariakoo au machinga wanaweza?

Mbona Kenya wanaweza?

Mada inaweka bayana kuwa wenye kumhusisha Odinga na ukabila au upuuzi, imedhihirika wapuuzi ni wao. Ndiyo maana hakuna mmoja kanyanyua pua hapa.

Zaidi sana inawatambua wapuuzi wengine ni mashabiki wa urusi dhidi ya Ukraine, washabiki wa Israel dhidi ya Palestine, nk.

Kwamba Kama mfano, ni wapuuzi pia washabiki wote wa dhuluma yoyote dhidi ya haki yoyote hata kama haki hiyo ni dhidi ya mashoga.

Kwamba Chadema ni movement yenye msingi wa haki, makundi hayo ya wapuuzi hapo juu kama yapo chadema yamepotea njia.

Hayo ni Bora yakawahi Lumumba au yakasaidiwa haraka kwenda yanako belong Kwa kufurushwa unceremoniously!

Hai ndiyo wanaotucheleweshea kiu yetu ya kupata katiba mpya sasa.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
Suala la ushoga ni very complicated and delicate, ndio maana unaona hapa licha ya kuzungumzia mambo mengine kwenye mada yako, lakini wengi wameondoka na la ushoga pekee, hiyo ndio sababu iliyonifanya nami nikaona niweke kambi hapo ili lijadiliwe kwa kina.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.
 
Suala la ushoga ni very complicated and delicate, ndio maana unaona hapa licha ya kuzungumzia mambo mengine lakini wengi wameondoka na la ushoga pekee, hiyo ndio sababu iliyonifanya nami nikaona niweke kambi hapo ili lijadiliwe kwa kina.

Ni hayo tu ndugu mjumbe.

Nasikitika kusema Ma CCM bila aibu hayataacha kusema yataendelea kUtatutawala kwa miaka mia.

Kwamba tuna mada yenye kuhusu haki. Kwamba inafahamika hayupo asiyekuwa na haki zake. Kwamba tukijikita tu kwenye haki zetu kikamilifu kama taifa, tutapata Katiba mpya Sasa. Ila hizo tunaacha ila tungependa kwanza tujadili ushoga?

Kwani hata kwa utakatifu upi tulio nao sisi tusiokuwa mashoga basi? Ikumbukwe misahafu inakataa kujihesabia haki na hasa dhidi ya wengine.

"Yale Yale ya mdada kahaba aliyepelekwa mbele za Yesu wakitaka kumpiga mawe hadi kufa."

Hivi mtu nzima asiyenihusu na viungo vyake au kiungo chake chochote akiamua kufanya au kufanywa lolote linalomhusu yeye, inanihusu nini mimi Nanjilinji huku?

Binafsi nitajikita kuona ndugu zangu wa karibu wanaonihusu ninawarithisha yale ninayoyaamini kama maadili mema yakiwemo kuheshimu amri 10 za Mungu.

Mambuzi kaamua kupelekewa moto na hata kuchomekwa kaa la moto nina nini cha kufanya nalo?

Kila mtu ana haki zake. Haki zetu za jumla ni pamoja na kupata Katiba mpya.

Chadema ni movement ya haki. Wasiolijua Hilo wafahamishwe. Kwa kuzijua haki zetu na kukomaa Nazi tunapata Katiba mpya Sasa!
 
Shoga atanyanyapaaje wenzie?

Swali ni kuwa "wewe unanyanyapaa mashoga?"

Hili lako ni jingine labda kama unatoa uthibitisho sasa kuwa kumbe mashoga huwa hamnyanyapaani.

Tumekusoma ndugu shoga.
 
Kwa hiyo Uhuru anaenda kugombea Uraisi tena? Sijawlewa

Mmieeeeee
 
Kudai haki ni ngumu sana, wengi wanaijua haki ni ile inayowahusu wao pekee, hawajui kama kuna haki za wengine nazo wanatakiwa kuziheshimu, haki zinatofautiana kulingana na makundi tofauti, heshimu haki za wenzio ili nao waheshimu zako, hii ndio sheria ya mchezo.

Mfano hilo la ushoga, huwa naona wengi wakilaani ushoga wanaegemea kwenye vitabu vitakatifu kwamba haviruhusu, sawa hata kama haviruhusu, nani anayetupa sisi wengine mamlaka ya kuwahukumu mashoga?

Ukweli ni kwamba wakati ukimnyooshea mwenzio kidole kimoja, tukumbuke vipo vingine vinatugeukia wenyewe, hilo ni kumbusho tosha toka kwa Mungu kuja kwetu wanadamu, kwamba ni yeye pekee ndie asiye na kasoro, mkamilifu.

Mbona tunajivika uungu kuwahukumu mashoga kinafiki ikiwa nasi tuna dhambi zetu nyingi tumezikalia kimya kimya? kazi ya kuhukumu ni ya Mungu pekee, wanadamu tusijivike hilo jukumu.

Pia kwa wazazi tunaolaani ushoga/usagaji kwa kuogopa wanetu wasijekujifunza, hapa la msingi ni jukumu letu kuwa karibu na wanetu kuhakikisha tunawasimamia karibu kimalezi, this is the only option.

Hii dunia haiwezi kwisha dhambi, wala tusipoteze muda kushindana na nature, Mungu kwa uwezo wake kama angekuwa hawataki mashoga hapa duniani angewaondoa, lakini siku zote andiko lazima litimie, kuhangaika kulifuta kwa midomo na kunyooshea wengine vidole ni kujidanganya.
Akihukumiwa na kulaaniwa bwana yule ni sawa ila wakihukumiwa mashoga ndio tunakumbuka kwamba Mungu ndio pekee mwenye haki ya kuhukumu.
 
Hebu acha kutokwa povu tupe uhusiano wa Kenyatta kusimama na Ruto.

Tuelezee historia fupi wako wapi chama kikongwe CHA KANU? Maana Kenya walikubali kuacha tofauti zao wakatengeneza katiba mpya na kuweka uwanja sawa wa kufanya siasa. Hawa majambazi ya CCM yasiyotaka kuweka uwanja sawa wa kufanya siasa siyo wajuaji uchwara bali ni wahanga wa ukatili ndio wakosaji? Bangi hizi!

Chama kinachotegemewa na nani? CHADEMA haiwezi kutegemewa na wajinga kama mtoa post hii. Sema ujuaji gani kama siyo undezi.

Haki gani ambazo CHADEMA hakuna ukilinganisha na CCM? Haki za kuhujumiwa?

Kama siyo upumbavu CHADEMA wapi imewanyanyapaa hayo makundi uliyoyataja? Tupe uthibitisho.

Na unatarajia CHADEMA ni wapumbavu kama wewe wafanyie kazi upuuzi

Uko kila mahali hueleweki unaandika kwa niaba ya CCM au chadema. Kwa maana nyingine umechachawa huelewi kushoto au kulia ni wapi.

Hujui Wala huna habari kuwa siasa hazina rafiki wala adui wa kudumu bali agenda. Hujui kuwa chadema haijutii Wala kujisifu kwa kuwa na kina zitto, lowassa, slaa nk au awaye yote katika historia yake.

Kama mburumundu tu unaruka ruka kutaka upewe historia za kina Ruto au kina Kenyatta.

Iko hivi mjomba Raila anaendesha harakati za haki dhidi ya Serikali ya Kenya. Huo ndiyo ukweli wenye kueleweka na wapigania haki wote lakini si wapuuzi niliowaorodhesha.

Haina shaka utakuwa umeguswa wewe.

Siyo kwa povu hilo ndugu.
 
Kwa hiyo Uhuru anaenda kugombea Uraisi tena? Sijawlewa

Mmieeeeee

Uhuru yuko na Raila 100% kwenye harakati zake za haki dhidi ya dhuluma.

Harakati za Raila si za kikabila bali za taifa kama kwetu tu na katiba mpya.
 
Imekuwa ni kawaida kwa wajuaji uchwara wa bongo kumwona Raila kama mkabila na mpuuzi fulani.

How Ruto allies provoked Uhuru to get involved in politics

Kenyatta kusimama na Odinga njoo 2027 kama bado siyo funzo kwa wajuaji uchwara hawa watajifunza lini?

Cha kusikitisha zaidi baadhi ya wajuaji uchwara hao wamo hata ndani ya vyama tegemeo kama Chadema.

Watu wasiojua maana ya haki, wasioamini katika haki au wasiosimama na haki bIla kujali maslahi binafsi hawana msaada wowote katika chama au nchi.

Watu wenye kuwanyanyapaa wapalestina, waukraine, na hata mashoga hawawezi katu kuwa hazina kwa chama au taifa lolote lenye kuamini kwenye ustaarabu.

Ushauri wa bure kwa Chadema, fukuza watu wote wa namna hiyo mara moja. Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria kuliko kuwa na rundo la wasiojitambua.

Waende kwa mambuzi huko ambako kukalia haki za wengine kwao ni jadi.
Chadema inategemewa na nani? Hapo kwenye mashoga umeendelea kuharibu zaidi
 
We
Chadema, fukuza watu wote wa namna hiyo mara moja. Ni heri kuwa na watu wachache waliodhamiria kuliko kuwa na rundo la wasiojitambua.
Unawashauri wafanye kufukuza watu?? Unategemea kitu gani kitokee upande wapili wa shilingi? e.g NCCR-Mageuzi au ACT-Wazalendo

Je itakuwa sawa Watanzania wakasema tuwafukuze wawekezaji Uchwara kwa sababu wanakwepa kulipa kodi, kodi ambayo ni haki ya Mtanzania? Kwa sababu wapo watu wa namna hiyo au?
Uhuru yuko na Raila 100% kwenye harakati zake za haki dhidi ya dhuluma.
Ni dhuluma zipi hizo, Kwamba kashindwa Uchaguzi kwahiyo ni dhuluma?

Harakati za Raila si za kikabila bali za taifa kama kwetu tu na katiba mpya.
??
 
Chadema inategemewa na nani? Hapo kwenye mashoga umeendelea kuharibu zaidi
Hawa hapa:

Fw0SUfgaAAMsytO.jpeg

Tofautisha watu na mambuzi. Kwenye mashoga ni mfano tu tunaoambiwa Hadi bungeni wamo.
 
Back
Top Bottom