Kero kutoka mbagala hadi mjini, njia imerudishwa kwenye foleni

Kero kutoka mbagala hadi mjini, njia imerudishwa kwenye foleni

Jambo ambalo nashindwa fahamu aliyetoa ushauri njia ya mwendo kasi kuzuiwa kupita hadi magari madogo kuanzia mbagala hadi bendera tatu.

Njia hii inawakazi wengi na wapo ambao wanaenda tafuta mahitaji wapo wanaoenda kutafuta bidhaa na kuja wauzia waliobaki walipotoka na bado wapo ambao wanaenda wahudumia jamii sekta binafsi na umma kwa ujumla.

Sasa njia imerudishwa kwenye foleni ya kufa mtu na hapo hapo kuna malori yanayotoka na kuingia bandarini na zamani BP kufata mafuta. Kwanini msingeachia gari ndogo zikapita hiyo njia ya mwendo kasi? kwani zina uzito gani wa kuharibu barabara?

Fikiria mtu anatoka kuwahi hudumia jamii anajikuta kanasa barabarani zaidi ya masaa na bado akifika bosi wake anaanza mpa barua ya kujieleza huku jamii aliyotakiwa kuhidumia nayo inakuja juu kwa kuchelewa pata huduma.
Ni jambo la kumshukuru mheshimiwa lahisi daktari saamia kwa yote haya
 
Back
Top Bottom