Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hiyo kali aisee, kuna la kujifunza kwenye hiliWe ulizidisha adhabu yan ukatoa mahari alaf ukagoma kumuoa? Hapo lazma wao umemtia mtoto wao gundu
Baada ya kutemana na wife,nikaanza mchakato wa kutafuta toleo jingine kwa ajili ya kusongesha maisha kwani aliniachia watoto wa4 hivyo nilihitaji mtu wa kusaidiana nae nikapata binti fulani 18yrs lakini tayari ana mtoto 2yrs, nikaona isiwe tabu maana kuna kaundugu kwa mbali nikaona huyu atanifaa,posa nikatoa 60,000/=balaa ikaja mahali, nikaambiwa nitoe ng'ombe wa4 na mbuzi 6, ktk kujitetea mama akasema kama huna mahari hiyo muache mwanangu maana ww ndo mwenye shida ya kulelewa watoto, mama mzazi akaniplease mwanangu mchukue tu maadamu mahari utatoa nusu nyingine utamaliza taratibu, nikawaambia hamna shida kwa mahari hii mimi nataka mke tu mtoto abaki na bibi yake, nikajibiwa na mama mkwe huyu mtoto ni wako kama unataka mke na mtoto pia ni wako, ikawa shida kidogo maana baba wa mtoto aliyezaa na binti anamtaka mwanae wazazi wa binti hawataki wanasema aliyemtolea mahari binti ndo mwenye mtoto. ItaendeleaStaili hii ndio hufanyika kwa wapenzi wengi.
Familia za kimasikini zinachukulia Mahari kama sehemu ya kupata mtaji. Hawajui kuwa Binti akiolewa anawapa heshima wao
Wanamuongezea gundu binti yao maana tayari kawa singo mother na ana ujauzito wa mtu anaetaka kufunika aibu, bado wanaweka vikwazo vitavyomuumiza tena binti yao.
Umelazimishwa kulipa mahari?Swala sio kulipa mahari. Swala ni kulipa milioni tatu cash, in full amount kama dau la mahari.
Hivi inaingia akilini unalipia mahari ya shillingi million tatu kwa mwanamke ambaye kwanza si bikra, pili ana mtoto, na tatu, hao wakwe huko mbeleni hatutategemeana kwani?!
Me nikilipia hiyo nabeba familia yangu nduki, wasinitafute kwa lolote isipokuwa salamu tu na kujuliana hali.
Ulistahiki uchumbie Binti mkubwa kidogo zaidi ya huyo wa miaka 18 maana umri huo bado sio mkomavu wa kuvumilia mikwaruzo ya kwenye ndoa na atakuwa na tabia za kufanana na watoto wako.Baada ya kutemana na wife,nikaanza mchakato wa kutafuta toleo jingine kwa ajili ya kusongesha maisha kwani aliniachia watoto wa4 hivyo nilihitaji mtu wa kusaidiana nae.nikapata binti fulani 18yrs lakini tayari ana mtoto 2yrs,nikaona isiwe tabu maana kuna kaundugu kwa mbali nikaona huyu atanifaa,posa nikatoa 60,000/=balaa ikaja mahali,nikaambiwa nitoe ng'ombe wa4 na mbuzi 6,ktk kujitetea mama akasema kama huna mahari hiyo muache mwanangu maana ww ndo mwenye shida ya kulelewa watoto,mama mzazi akaniplease mwanangu mchukue tu maadamu mahari utatoa nusu nyingine utamaliza taratibu,nikawaambia hamna shida kwa mahari hii mimi nataka mke tu mtoto abaki na bibi yake, nikajibiwa na mama mkwe huyu mtoto ni wako kama unataka mke na mtoto pia ni wako,ikawa shida kidogo maana baba wa mtoto aliyezaa na binti anamtaka mwanae wazazi wa binti hawataki wanasema aliyemtolea mahari binti ndo mwenye mtoto. Itaendelea
Sasa hao wanaoelewa na mamilioni ya pesa nini huwa tofauti ya maisha ya ndoa na hao wanaolewa na vitanda tu.Mmezoea ndoa za kiislam MTU ananunua kitanda kazi imeisha ...poleni sana
Waislamu mahari anachukua anayeolewaHiz mahari za kupangwa na wazazi ni dolo sana ndio maana waislam wanaongoza kwa ku
[emoji28][emoji28]kwaiyo kijana apewe posho?Binti kuzalishwa na kuachwaisha anakuja kijana anajitolea kumchukua pamoja na kuzalishwa kwake, inabidi mzazi asgukuru, na lakini hao ndo kwanza na mahali inapanda eti na ya uchafuzi[emoji16][emoji16][emoji16], mtu hajakuta hata bikra na kabla ya mechi tayari 1:0, Yan m naona wao ndo ilibidi wampe posho kijana kawaondolea aibu.
Sasa kanjibai hayo maswali usituulize sisi nenda kawaulize hao wazazi wa huyo binti ambae unataka kumuoa.Ni kijana wa Miaka 25, shahada ya Ualim, ila hakubahatika kupata ajira rasmi.
Amejiajiri kwa kufungua twisheni za mitaani na kabahatika kupata mchumba ambae ni binti wa Miaka 21 ( Ila tayar ana mtoto wa Miaka 3). Amedumu kwenye mahusiano na binti kwa mwaka mmoja tangu Desemba 2020 na Sasa na mwezi Januari 2021 alishika ujauzito wake. Ambapo kwa Sasa anamimba yenye miez 5, kijana akaona afanye mchakato wa kuanza Kuishi rasmi pamoja na binti.
Kaandika barua ya uchumba ukweni imepelekwa na imekubaliwa, majibu yamerudishwa vimeorodheshwa vitu kadhaa na pesa taslim ambazo ukijumlisha inakuja jumla ya 4,600,000 (million 4 na laki 6)
Kijana akazungumza na mshenga kua icho kiwango Ni kikubwa na hawez kabisa kukimudu, mshenga kamshauri asiogope Ayo yanazungumzika na kitapunguzwa Sana watakapoenda kutambulishwa.
Siku ya kutambulishwa maongezi ya punguza yanaendelea, ila Mwisho kabisa wazazi na Ndugu wa MKE wakaishia milioni 2 taslimu (million 1 kwa ajili ya mahari na million 1 Ni faini ya uchafuzi- kuzalisha kabla ya kuoa ). Na mkaja wa mama laki 5 na vitu mchanganyiko vinavyogharimu laki 7. Jumla vyote unapata million 3 na laki 2.
Kijana kasema yeye hicho kiwango hana na hawezi kupata kabisa kwa sasa, kwa kazi anayofanya haimruhusu kabisa kupata kiasi icho. Akasema yeye alijiandaa kwa million 1 na laki 5 kwa Mambo yote.
Mshenga akaliwasilisha kwa Wazee, Wazee wakasema "ilo haliwezekani kijana maana kwenye ukoo wetu hamna mtu ameolewa chini ya million 2 mahari na vitu vyetu, iyo umependelewa kutokana na uchumi Wako Kama alivyotuambiwa na binti yetu"
Kijana akakubali ila akaomba alipe kwa awamu, 1.5million afu baadae atamalizia 1.7million. Wazee Nalo wakakataa kata kata kua hamna cha kupunguza hapo, labda akajipange KWANZA akiwa tayari aje
Kijana amepanik, Ameondoka amemuacha binti kwao na anazunguka uku na kule Anaomba akopeshwe pesa ili akamilishe zoezi. Kaja KWANGU kwetu Kama watu wake wa karibu tumsaidie kwa Hali na mali kakamilisha zoezi lake ili alilokwisha lianza. Kaniomba nimsaidie au nimkopeshe kiasi icho, Kiukweli nafsi yangu imegoma kabisa na nimemwambia kabisa kua yeye Ni rafki yangu ila kumchangia suala Hilo maana naona anajitwika mzigo mkubwa wkt uwezo wake ni mdogo.
Kuna vipaumbele vingi vya Ela ila sio kwa ilo, ila Kama uwezo anao apambane mwenyewe tutamsapoti kwa vingine.
Kijana
Amepambana kwa kuuza baadhi ya vitu vyake vya ndani Kama laptop, dressing table na stendi ya viatu. Jumla vyote kauza kapata laki 5 na 50.
Amepambana tena ameenda Kwenye taasisi flani izi za mitaani ya kukopesha fedha, ameweka bond kiwanja alichaochiwa na marehem mama ake mzazi kwa ajili ya mkopo wa 1.3 million kwa miezi 6. Kaniomba nikamdhamini, na kiroho Safi nimemdhamini na mkopo kapata chap kaenda kumaliza zoezi lake.
Ila baada ya kijana kuondoka NIMEBAKI NA MASWALI YAFUATAYO KICHWANI:
1. mahari Ni malipo ya shukrani kwa wazazi kwa kumtunza vema binti yao.
-Inakuaje kijana alazimishwe kulipia mahari kubwa kwa binti ambae alimkuta bila bikra?
Kibaya Zaid binti alishazalishwa kabla.
2. Inakuaje kijana atozwe faini ya uchafuzi wakati binti mwenyewe tayar alikua keshazalishwa hapo awali na binti tayar alikua na mtoto mkubwa? Maana Ake iyo mimba ya jamaa inakua ni mimba ya pili kwa uyo binti?
3. Wazee inakuaje wang'ang'anie binti yao hawezi kuolewa na kijana bila kumaliza kabisa mahari wakati wanaona kabisa kijana uwezo wake kiuchumi Ni mdogo?
4. Wamechukua hatua gani kwa kijana aliemzalisha binti yao hapo kabla ya kulipa mahari?
5. Wazee, je Binti yao amegeuka bidhaa ya kuuzwa kiasi kwamba lazima awekewe kiwango maalum Cha gharama za kuolewa rasmi, na isipofikiwa Basi haiwezekani? Yaani eti "Hakuna binti yetu yoyote ameolewa kwa mahari chini ya mil 3"
6. Kijana anajiskiaje anapokua na mke ndani ambae ameingia madeni na gharama za kuuza vitu vyake kwa hasara ili mradi amuoe? Yaan una MKE ambae umepata kwa gharama,madeni na Maumivu makali sana?
7. Itakuaje endapo atashindwa kurejesha Deni ndani ile miez 6 na kiwanja Cha urithi kichukluliwe kisa Ela ya ule mkopo ulienda kulipia mahari ya kuoa MKE?
8. Binti alishindwa Nini kusimama na mwanaume wake kusimama na yeye pamoja kumtetea dhidi ya Wazee wenye tamaa ya Ela ya mahari?
Kiukweli, ili suala limeniacha na sintofahamu nyingi kwa jamii zetu hizi kuhusu ustaarabu na mtizamo wao Kwenye suala Zima la Utoaji wa mahari.