Kero Makanisani: Mwambie mwenzako, mshike mkono mwenzako, mkumbatie mwenzako. Haya maneno chanzo cha michepuko mipya Kanisani

Kero Makanisani: Mwambie mwenzako, mshike mkono mwenzako, mkumbatie mwenzako. Haya maneno chanzo cha michepuko mipya Kanisani

Mimi ni muumini wa kanisa la KKKT, sasa Kuna Shida Moja inanisumbuaga Kanisani ni pale Mchungaji anakuwa anahubiri mara ghafla anakwambia mgeukie mwenzako au Mshike mkono Mwenzako.

Yaani unageuka unakutana na mdada mzuri mweupee ana shepu pale pale unahama Kanisani. Tena akiwa na yeye yupo interested mnahama wote Kanisani mnabadilishana number mnaanza kuchat.

Nimeliongea hapa kama Kuna ufumbuzi basi ufanyike wadada wakae siti zao.
Ukizungumzia hilo wapo wanaopata hamu ya ushoga kupitia mgusano huohuo
 
Yaani akasali sehemu Moja na Majin(a.k.a mashetani) wamwombe Mungu mmoja? Yaani hapo ndio unamdumbukiza shimoni kabisa

Kwani kanisani hakuna majini????

Usitafute kuharibu uzi ,ukitaka ligi fungua uzi wako watu watakuja kuchangia huko.

IMG_4852.jpg
 
Mimi ni muumini wa kanisa la KKKT, sasa Kuna Shida Moja inanisumbuaga Kanisani ni pale Mchungaji anakuwa anahubiri mara ghafla anakwambia mgeukie mwenzako au Mshike mkono Mwenzako.

Yaani unageuka unakutana na mdada mzuri mweupee ana shepu pale pale unahama Kanisani. Tena akiwa na yeye yupo interested mnahama wote Kanisani mnabadilishana number mnaanza kuchat.

Nimeliongea hapa kama Kuna ufumbuzi basi ufanyike wadada wakae siti zao.

Chupu niingie kwenye mahusiano ya mke wa mtu. Maana huyu mwanamke kanisave mchungaji wananipigia hadi usiku akiwa na mumewe mke wangu anapokea. Mke wangu hanielewi anadhani nimetembea naye. But sijatembea naye nilichokifanya siendi tena kanisani maana chat zetu zimefikia hatua ya mahusiano wakati mimi na mke wangu tuna majukumu mengi sana ya familia nikiingiza mahusiano mapya na mwanamke yule mrembo na mwenye pesa lazima mke wangu mpenzi na familia itasambaratika.

Kama Kuna mamlaka yoyote ikae ijadili hili jambo. Kwanini mchungaji asihubiri tu bila hii kitu au kama anataka attention basi atusimamishe tukae au Tupige magoti?
Njoo huku kwa Ngalalekumtwa.
 
Yaani unageuka unakutana na mdada mzuri mweupee ana shepu pale pale unahama Kanisani. Tena akiwa na yeye yupo interested mnahama wote Kanisani mnabadilishana number mnaanza kuchat.

Hizi ni shida zako mkuu sababu wadada wazuri tunakutana na kujumuika nao kwa kugusana, kuongeleshana na kutazamana kwa ukaribu sehemu nyingi tu mathalani kwenye daladala, supermarkets, kwenye masanga n.k...

Tamaa zako mwenyewe ndio zitakuongoza kwenda hatua inayofuata...
 
Kwani kanisani hakuna majini????

Usitafute kuharibu uzi ,ukitaka ligi fungua uzi wako watu watakuja kuchangia huko.

View attachment 2744794
Sio sera ya kanisa kama ilivyo kwenu. Ninyi Kuna Aya kabisa za kuyaita ,kuyatengeneza na kuyatumia majini ( mashetani), Nimetembea karibu Tanzania nzima Kila nje ya nyumba zenu za ibada Kuna vijana wanauza madawa na kutoa tiba za kienyeji.Kwenu mtu akifuga majini (mashetani) anasifiwa kwa kuitwa mamwinyi au masharifu.Kwetu akikengeuka mtu na kujifunza majini au ushirikina akigundulika anafungiwa na kutengwa
 
...kampun ya aim global ina hako ka tabia... Hii tabia isifike kwenye mabasi... nakemea...
 
Back
Top Bottom