Mimi ni muumini wa kanisa la KKKT, sasa Kuna Shida Moja inanisumbuaga Kanisani ni pale Mchungaji anakuwa anahubiri mara ghafla anakwambia mgeukie mwenzako au Mshike mkono Mwenzako.
Yaani unageuka unakutana na mdada mzuri mweupee ana shepu pale pale unahama Kanisani. Tena akiwa na yeye yupo interested mnahama wote Kanisani mnabadilishana number mnaanza kuchat.
Nimeliongea hapa kama Kuna ufumbuzi basi ufanyike wadada wakae siti zao.
Chupu niingie kwenye mahusiano ya mke wa mtu. Maana huyu mwanamke kanisave mchungaji wananipigia hadi usiku akiwa na mumewe mke wangu anapokea. Mke wangu hanielewi anadhani nimetembea naye. But sijatembea naye nilichokifanya siendi tena kanisani maana chat zetu zimefikia hatua ya mahusiano wakati mimi na mke wangu tuna majukumu mengi sana ya familia nikiingiza mahusiano mapya na mwanamke yule mrembo na mwenye pesa lazima mke wangu mpenzi na familia itasambaratika.
Kama Kuna mamlaka yoyote ikae ijadili hili jambo. Kwanini mchungaji asihubiri tu bila hii kitu au kama anataka attention basi atusimamishe tukae au Tupige magoti?
Tatizo sio kanisa wala utaratibu wa kanisa ni kile kilichoko ndani ya Moyo wako , kama Moyo wako umeweka uzinzi hata kama uko wapi utawaza Tu uzinzi, weka ndani yako neno la Mungu uone kama utapata hayo matatizo, kumshika MTU mikono nk haikupi uhalali wakuingia katika Matendo ya dhambi kuna nchi hapa duniani wanawaka hawaruhusiwi hata kutembea peke Yao barabarani lakini bado nchonhigo hiyo unaskia wanabakwa na kufanyiwa ukatili ? Kwa hiyo ni tabia ya mtu
Soma hapa
Zaburi 119:9,11
[9]Jinsi gani kijana aisafishe njia yake?
Kwa kutii, akilifuata neno lako.
[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako,
Nisije nikakutenda dhambi.
Pitia hapa
Roho ya uzinzi haishindwi kwa Sheria za Mwili za kutokugusana au kushikana Bali kwa Sheria ya Rohoni
Wakolosai 2:23
[23]Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili.
Soma habari za Yusufu ,hapa ..
Mwanzo 39:9Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
Usije kumkosa Mungu Kwa sababu ya weupe au shepu ya MTU , uzuri ni ubatili Leo upo kesho haupo tulia kwenye ndoa yako hakuna MTu Mbaya duniani ni maamuzi ya nafsi yako Tu , ndio yanaweza kusema Huyu mzuri au Mbaya , hata Bibi alikuwa binti na Mungu akusaidie