KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

Kwa hiyo kwa jibu hilo alimaanisha kuvuta sigara sio dhambi?
 
kuhusu utajiri wake sina shida kabisa naye, nina shida naye kwenye mavazi na mienendo yake, haiendsni na miiko ya Kikristo kabisa,na ni kama kajifichia kwenye ukristo li afanye yake. kiufupi anawaharibia walokole.

Naona ungeanza na waumini kwanza.
 
acheni kupangia maisha ya mtu.kuokoka kusikufanye usivae vizuri ili mradi husiwe nyuma ya maadili tu.ulitaka havae magunia.haja wai kumkosea mtu kwa baya.usiwe na mtazamo mbovu.tatizo la sisi watanzania ukiona mtu ana mafanikio basi roho zetu nyeusi zinakuwa na chuki na kuanza kupangia maisha yatu.mwanga si aje usiku.hata mchana
 
Hakuna kitu kinachoitwa "maadili ya kipentekoste" makanisa haya yako mengi na kila moja linaendeshwa kwa matashi ya mwanzilishi, wapo mapasta wanaovaa hvyohvyo kama masanja kwa utashi wao na wapo wanaovaa vzr zaidi nao kwa utashi wao vilevile.

hakuna chombo kilichoko juu ya mwenye kanisa zaidi ya yeye mwenyewe.

Kama mtoa mada umebahatika kuwa ktk moja ya makanisa yenye uongozi mzr mshkuru Mungu na wala usijivune kwani leo ya masanja yaweza kuwa kesho yakwako maana mfumo uliokutengeneza wewe ndio huohuo uliomtengeneza masanja.

Na hata siku moja usijerudia kulinganisha madhehebu ya kilokole na kanisa katoliki ktk mambo ya kanuni, sheria, taratibu na kanuni za maadili ya kikanisa, wale wako mbali sana ktk mambo hayo.

Siku zote usisahau "umoja" ndiyo ishara ya "upendo" na "Mungu" ni "upendo". Mgawanyiko ni alama ya " laana" toka enzi za babiloni na "laana" haijawahi kumwacha mtu salama.

Kwa sbb hyo, tumeona na tutaona mengi toka kwenu.

Mwenyezi atunusuru.
 
Heeee heeee anaeibiwa ameanza kushtuka sasa msikomae na Masanja tu wako wengi ambao mnawaita mitume,manabii na wanawapiga sarafu ndefu kila siku anzeni na hao kwanza.
 
Ulokole mgumu, anataka kushika mambo mawili kwa wakati mmoja, Dunia anaipenda na mbinguni anapatamani. Yu vuguvugu, Mungu atamtapika. kila kitu na kanuni zake
 
Tusiwe wepesi wa kuhukumu,hatujui moyo wake ,ukimyooshea kidole kimoja vinne vyote vinakugeukia mwenyewe
 
Milokole mishamba siipendi kama nini, kwa hiyo ukiokoka ndo umeambiwa uvae magunia, kama huwezi kwenda na wakati pita hivi [emoji118]
kwenda na wkt kwa kuvaa mileage na kusuka nywele?
 
Wa kuhukumu Mungu tu mwacheni masanja kama anadanganya n yy na Mungu wake....yeye ndio anaujua ukwl.....ila sijaona shida ya mavaz yake kiukwel au avae Yale masuti ya vilebo mikoni? Na masuruali ya kwaya? Usikariri maisha.
 
Dini ya kikiristo ndio ina mizwazwa mingi ya kupiga pesa....ndio maana kila mpuuz anakuwa anakimbilia huko kuchota mpunga
 
Leo nimeona picha ,yuko kwny ndege na binti mmoja,sasa jamaa akaanza kumhusisha mungu kweny mambo yake,anamsifia yule binti ni mzuri,na anamshukuru aliyepanga seat za ndege,huyu jamaa ni jipu
 
Mbingu ngumu! Pesa inatafutwa kwa njia nyingi ila tuweni macho na hawa watu wengi hutumia dini kama kivuli cha kutenda uovu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…