KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

KERO: Masanja Mkandamizaji kutumia Ulokole kinyume na maadili ya Kipentekoste

Yaani kuna ujinga fulani hivi kwny akili za watu!
Kwamba mlokole asivae vzr,yy ni nguo za marinda,km mwanamke,na suruali za upanga/celebration kwa mwanaume na mashati ya rangi!

Yaani kwamba ulokole usitembelee maeneo ya ufukwe ,usitoke na iwe na familia nk kwenda ku refresh nk!
Ulokole usijichanganye

No ,huyo sio Mungu,kila kitu kimeumbwa na Mungu,biblia inasema dhahabu na fedha ni mali ya Bwana! Mungu hakutuleta tuteseke,no...hayo ni ya shetani!
Ndo maana Yesu alisema "duniani mnayo dhiki lkn jipeni moyo mimi nimeushonda ulimwengu"

Cha mhim kuwa makini sio kila fashen ni salama
 
Labda ungemshauri aache kabisa sanaa, maana usanii unamfanya avae, asuke au kunyoa kulingana na sanaa yake iliyomtambulisha hadi ukamfahamu!!
 
Habari ya mda Huu..

Asilimia kubwa ya watu duniani wanaamini uwepo wa Mungu, na uwepo huu wa Mungu umeleta Imani tofauti tofauti za ambazo binadamu huziishi. Na Imani hizi zinaheshimiwa, wapo wenzetu waroma, wakatholiki, wapentekoste, kila imani inataratibu zake na miiko yake inayoheshimiwa na kila muumini wa dini hiyo.


Kwa upande wa wapentekoste, sote twajua namna miiko yao ilivyo hasa katika mavazi, tumeona kwa waroma tumeona kwa waanglikana, zaidi sana hata kwa wenzetu waislamu.Uwepo wa dini hizi umekuwa msaada sana kwa jamii hasa kuibadilisha jamii na hasa vijana kuwa na miiko na heshima.

Lakini siku za hivi karibuni, kumekuwepo na wimbi la vijana wanaokimbilia ulokole lakini matendo yao hayaendani na miiko ya kilokole, bika kupepesa pepesa kumekuwa na celebrity huyu anayefahamika kama "Massanja mkandamizaji" ama "Emmanuel Mgaya" huyu amekuwa akijiita PASTOR.

Kumekuwa na malalamiko mengi hasa toka wa vijana wakilokole wakilalamika mienendo ya celebrity huyu na mavazi yake yasiyoendana na miiko ya kilokole, ki ukweki kuna wakati ukimwona ni kama kijana mwingine tu wa mitaani, kuvaa mlegezo, kusuka nywele, kofia kuvalia nyuma, hivi haviendani na miiko ya kikristo.

Kwenye jamii inaonyesha picha kuwa Anajifichia kwenye mwamvuli wa kipentekoste ili hali si mpentekoste...sasa unamdanganya nani massanja? hata moyo wako ukushuhudie kuwa.

Unachokifanya hakiendani na maadili ya kipentekoste, kumbuka wewe ni kioo na ni maarufu, hivyo either ubadili namna unavyovaa au uache kutumia ulokole kama kivuli cha maovu!


Unaharibu Taratibu za kipentekoste!


Ujumbe huu ukufikie mahali pote ulipo
92395f03f88a62a17fe2ae4374070d17.jpg
Utu si mavazi na wokovu si mavazi,hata kama akitembea uchi kama roho yake ni safi haina shida,msikimbilie kusafisha vikombe nje wakati ndani vimejaa ukoko
 
Tusiifananie dunia kwa mwenendo,matendo wala mavazi,maana hayo humwakilisha tunayemtumikia,Mungu ana mavazi YAKE,shetani nae ana mavazi YAKE,itategemea wewe unamwakilisha nani

Sent from my itel it1703 using JamiiForums mobile app
 
Huyu mwizi tu kama wezi wengine tuache kupepesa macho na imani kabisa dini kivuli huyu bwana
 
Gwajima je siasa kanisani?
Siasa kanisani ni sawa tu. Dini inajishughulisha na maisha ya watu na siasa nayo hivyo hivyo. Kiongizi yoyote wa Dini anejiepusha na siasa hajui wajibu wake.
 
Yaani watu bwana
Hivi unajua haya mambo ni ya rohoni? Uhusiano wa Mungu na mtu ni personal,mwingine utaishia kuongea tu!

Kwa mavazi hayo kwny picha sioni tatizo!

Hayo ya kusuka ,milegezo sidhani tangu aache komedy bado anafanya nachojua alishaacha kabisa!
Ht page yake baada ya kuoa alifuta pics zote sijui km kaanza tena kuweka
bila shaka na wewe, ni mvaaji wa mavazi yasiyo na maadili ya kipentekoste,
 
Huyu jamaa bado anaushamba flani hivi pamoja na mafanikio yote aliyonayo.

Kuna siku niliona amepost picha ndani ya ndege na mama mmoja wa kizungu amelala ameachama mdomo! ule ni ujinga wa kiwango kikubwa. Yule mama angaliona picha ile angalimfungulia mashtaka ya udhalilishaji.
Real . Haishi katika maadili yakiroho.
 
Real . Haishi katika maadili yakiroho.
Na hii inaleta ukakasi sana, hata watu ukiwashuhudia wanakupiga maswali tena wakimhusisha massanja yaani mpaka unachoka!
 
Na hii inaleta ukakasi sana, hata watu ukiwashuhudia wanakupiga maswali tena wakimhusisha massanja yaani mpaka unachoka!
Yaani hata kama kaamua awe mpiga hela bac naajifiche angalau asisababishe ukristo wote kudharaulika
 
Kuna siku niliona post yake kavaa t shirt ina li nembo la pyramid kama za ma freemasonry nikaona jamaa kajificha tu kwenye neno ila ndo wale wale
Ulokole ni kombinenga kuanzia kuvaa,kuongea,kutenda nk mtu akikuona tu hatii shaka na ww kama unachembechembe ya kiibilisi haijifichi kamwe
 
Nani alikwambia kila celebrity kanisani kafuata injili? Hiyo chumvi tu kwenye mboga, ukizingatia kuna biashara kubwa huko. Ndio maana kila siku unawaona kanisa la "nabii" mpya linapokatwa pochi nene zaidi. Rose Muhando si yule pale, Oo Yesu, Yesu (wakati ana pesa) alivyofulia akamiss msikitini (kasahau kashatuimbia kila kitu ni possible kwa Yesu) mara ghafla huyooo kwenye ngada.
Sio kweli kuhusu Ngada.Walimsingiziaaaaà
 
Back
Top Bottom