sky soldier
JF-Expert Member
- Mar 30, 2020
- 5,407
- 19,264
- Thread starter
- #21
Nimewahi kupita ile barabara ya kiwira pale soweto inayotokea makunguru nimefika sehemu kuna nyumba ina msiba kweli na hapo hapo kuna vijana wa msibani hapo barabarani wana picha ya marehemu wanatusimamisha wenye magari, kiukweli nilisikitika japo nlitoa buku, hata wakiandika jina haina maana, mimi mpita njia tu hivi hela inakofika huko watanijuaje.Nakuunga mguu mia kwa mia! Hii tabia inakera sana pale Mbeya! Mwenyewe nimeishi Mby na nimeshuhudia ujinga huu sanaa! Hasa ile barabara ya Makunguru! Na fedha nyingi zinazochangishwa zinasimamiwa na vibaka, hadi wengine wanakuonyesha picha kumbe mtu alikufa miaka mitatu iliyopita au hata wanakurupua tu lipicha la mtu huko studio na kutembeza kuwa ni marehemu! Shenzi kabisa hawa!