Kero: Wasukuma kuongea kilugha kila mahali

Hhii nchi haina mipaka ya matumizi ya lugha na si kila ndugu yako anaweza kuongea kiswahili fasaha. Unapoleta maada ufikirie kuna wenye akili zaidi yako.tupo tunaoishi mikoa mingine lakini tunasemeshwa kwa lugha ya wenyeji pia, ingekuwa kero thread km hii zingekuwa nyingi. Msukuma ni mtu asiyependa kujionyesha kuwa amesoma sana hivyo lugha mama kwake ni jadi. Mbona huzungumzii wamasai, wanyaturu, wasambaa na wapare hata wachanga. Ni kwasababu huna exposure. Nahisi unajisikia fahari kuongea lugha yako kuliko msukuma kutumia lugha yake ufinyu wa akili huo. Nyie ndo mkihamia mjini ukirudi kwenu unajidai hujui kilugha chenu. Ulitaka kisukuma kizungumzwe na nani kama si msukuma na km hutaki watumie kisukuma basi go and fight with nature.....
Nb. Wamasai wao hata kiswahili chako hawajui. Unahitaji kurudi darasani wewe umkaririshwa ile tabia ya kuvalishana kengele kwa kuongea lugha nje ya kizungu.
 
Weee shida yako ni kiluga au mtoko. Je hujawaki kutoka na sie wa BK.!! Acha ushamba weee.
Achana naye mbona ye akiwa na jambo lake mbele ya mama/baba asiyesoma anatumia kiingereza ili wasimwelewe. Hajui kuwa hivi vitu vipo by nature.
 
Yaani wengine wanaongea hata kwenye basi akigundua kondakta ni msukuma mwenzake yaani wanaongea kwa sauti toka siti ya nyuma hadi huku kwa Kondakta ni taabu tupu.
 

Tatizo siyo kuongea kilugha...tatizo ni kukosa ustaarabu na kuwasumbua wengine kwa kuongea kwa nguvu na makelele yenu....mbona kuna makabila yanaongea kilugha sana lakini hawawasumbui watu wengine?
 
Wanadumisha utamaduni na sio kero pia lugha hizi Mara nyingi hukuza kiswahili. we kama huna lugha ya kwenu we sio mtz. mfano kabila letu neno masanga alikua analitumia bibi yangu ambae baada ya miaka mingi neno masanga nikakuta kua ni neno LA kiswahili sanifu ..kwa hiyo nakubaliana nao waongee kila sehemu japo mi sio msukuma.
 
Ishindo lyako!
 
Wasukuma ndio Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…