Waziri wa Nishati mh Makamba kwa mbwembwe nyingi alituaminisha kwamba tatizo la umeme itakuwa hadidhi baada ya kufanyia matengenezo makubwa mitambo ya kufua umeme kwa mda wa siku kumi.
Tena akaenda mbali anasema ya kwamba mitambo hiyo ni mibovu kwa sababu kwa kipindi chote cha marehemu JPM haikufanyiwa matengenezo kwa sababu makundi waliogopa kuizima mitambo hiyo ili kuifanyia matengenezo kwa kuogopa JPM. Lakini ajabu kubwa ni kwamba baada ya matengenezo ya mitambo hiyo ndiyo tatizo la umeme limeongezeka zaidi.
Je, mafundi waliiharibu mitambo hiyo badala ya kuutengeza? Na kama siyo hivyo ni bora warudishie ubovu ulikuwepo katika mitambo hiyo ili kutunusulu na tatizo hili la umeme. Kwani ilipokuwa mibovu hatukushuhudia tatizo hili la kukatika kwa umeme kila siku
RUSSIA NA UKRAINE SITISHENI VITA MNAUA RAIA WASIYO NA HATIA