Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Huku kwetu maeneo ya msikiti wa Bondeni umeme hakuna sijui matengenezo bado !.
 
Waziri wa Nishati mh Makamba kwa mbwembwe nyingi alituaminisha kwamba tatizo la umeme itakuwa hadidhi baada ya kufanyia matengenezo makubwa mitambo ya kufua umeme kwa mda wa siku kumi.

Tena akaenda mbali anasema ya kwamba mitambo hiyo ni mibovu kwa sababu kwa kipindi chote cha marehemu JPM haikufanyiwa matengenezo kwa sababu makundi waliogopa kuizima mitambo hiyo ili kuifanyia matengenezo kwa kuogopa JPM. Lakini ajabu kubwa ni kwamba baada ya matengenezo ya mitambo hiyo ndiyo tatizo la umeme limeongezeka zaidi.

Je, mafundi waliiharibu mitambo hiyo badala ya kuutengeza? Na kama siyo hivyo ni bora warudishie ubovu ulikuwepo katika mitambo hiyo ili kutunusulu na tatizo hili la umeme. Kwani ilipokuwa mibovu hatukushuhudia tatizo hili la kukatika kwa umeme kila siku

RUSSIA NA UKRAINE SITISHENI VITA MNAUA RAIA WASIYO NA HATIA
 
Huku umekatika saa 12 jioni ndo umerudi muda sio mrefu.
 
Huku chanika sisi toka saa 3 asubuhi mpaka muda huu hamna umeme!

Kale katakataka pale wizarani sijui kana fanya nini.

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Jana umeme umekata kuanzia saa 12 jioni mpaka leo 3/3 saa 3 asubuhi.


Umerudi saa 3 umekaa mpaka saa 8 mchana umekata tena wakarudisha saa 1.

Mpaka saa tatu umeshitua karibia mara 4.


Shida ni nini?


TANESCO naombi mnijibu

Hii hali itaendelea mpaka lini?

Wiki ijayo naagiza generator kutoka China.

No way out!
 
Huwezi ukapata majibu.nahisi kuna jambo lipo serious.Nipo wilaya fulani ya mkoa wa Morogoro,hakuna siku itapita bila umeme kukatika na ukirudi unawaka na kuzimwa mara kwa mara.Tumeulizia lakini hakuna wa kutoa maelezo ya kina.
 
Back
Top Bottom