Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Kero ya Kukatika Umeme Mara kwa Mara: Wiki hii kukatika umeme kunanitesa kuliko zile siku 10 za mgao

Ngoja aje hapa huyo Tanesco atakwambia
Nipe namba ya simu
Location
Halafu anapotea.
 
Huku nilipo umeme upo labda liluku tu ndiyo likate
 
Wameshajua hatuna la kuwafanya tutazoea tu.. poor Tanzanian.. Tuliyataka wenyewe lakini, ambao tuliwategemea watupiganie tuliwasaliti sahizi wapo ubeligiji na kwingineko huko.
 
Hujasema ni wapi maana mikoa mingine upo full nondo
 
Kwa nini unatumia picha ya Lissu wakati wewe ni mataga?!
Jana umeme umekata kuanzia saa 12 jioni mpaka leo 3/3 saa 3 asubuhi.


Umerudi saa 3 umekaa mpaka saa 8 mchana umekata tena wakarudisha saa 1.

Mpaka saa tatu umeshitua karibia mara 4.


Shida ni nini?


TANESCO naombi mnijibu

Hii hali itaendelea mpaka lini?

Wiki ijayo naagiza generator kutoka China.

No way out!
 
Subiri bwawa la Nyerere likamilike utapata umeme wa kutosha
 
Vipi waungwana kuunganisha umeme bei imeshapunguzwa au ni ile ile 320k
 
Kuna Mzungu mmoja mwenye hotel Arusha na Serengeti siku moja pale AICC alisema

''Among all other problems in Tanzania, Lacking of Electricity is the most''

Sidhani kama nimepatia kiingereza alichoongea. Ila aliongea kwa uchungu sana.
 
Ni mwendo wa miundombinu tu, utafikiri hizo miundombinu zimeanza awamu ya 6
 
Bora ubovu wa zamani urudi
 
Ukipita kwenye ofisi za tanesco ndo utagundua kuwa Tanzania tatizo la umeme haliwezi kwisha maana wale jamaa wanatengeneza matatizo maksudi ukiwakuta pale nje asubuh walivyo wengi bila kukata umeme wengi watakosa kazi za kufanya kiufupi wanatengeneza matatizo ili wapate hela za maintenance.
Huu ndio ukweli.
 
Nadhani ni vema kila mmoja aseme yupo wapi ili wajue tatizo kubwa lipo maeneo gani hii kila mtu kusema huku kwetu huku kwetu, siajabu wote mpo mtaa mmoja tu.

Tunapowasilisha haya malalamiko basi tutaje na maeneo ili tuone he ni kweli tatizo ni kubwa kiasi hiki?

Ushauri tu maana no wazi hata mitaa yetu umeme wanakatakata Tena unakaa dakika kumi wanarudisha Tena unakata Jana it was seven times hapa makonde Mbezi beach.
 
Back
Top Bottom