Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Kama ni hivyo basi apewe nauli aliyotumia kuripoti kwa mujibu wa maagizo aliyopewa kwenye barua, kisha apewe nauli ya kurudi nyumbani akisubiri kuitwa tena!!
Wakati unaomba kazi wangekwambia kama utahitaji kulipiwa nauli na serikali ya kuja kuripoti na kurudi basi usiombe kazi nawaza tu ungeomba au usinge omba hiyo kazi.
 
Wakati unaomba kazi wangekwambia kama utahitaji kulipiwa nauli na serikali ya kuja kuripoti na kurudi basi usiombe kazi nawaza tu ungeomba au usinge omba hiyo kazi.
Hayo ni mawazo mfu!! Utumishi wa umma unaongozwa Government standing orders na siyo matakwa ya mtu!! Haki za waajiriwa wapya lazima zilindwe! Kulipiwa nauli mwajiriwa anaporipoti kazini ni takwa la kisheria!!
 
Si awasiliane na mamlaka husika. Humu jf raia wanakukebehi wanalala mbele...a follow complaints channel sahihi ahudumiwe
 
nikujibu kwa uzoefu,

1. mara nyingi hizi ofisi hazina pesa kwa ajili posho ya kujikimu ambayo anapaswa apewe muajiriwa mpya.

2. na ndiyo maana ukishajaza fomu ya maelezo yako binafsi wanakuambia utapigiwa simu lengo lao ni kuwa ukishaingia kwenye mfumo wa mishahara hazina ndiyo unaitwa rasmi ukaanze kazi.
 
Hayo ni mawazo mfu!! Utumishi wa umma unaongozwa Government standing orders na siyo matakwa ya mtu!! Haki za waajiriwa wapya lazima zilindwe! Kulipiwa nauli mwajiriwa anaporipoti kazini ni takwa la kisheria!!
Mkisha pataga ajira ndio huwa mnaanza kujifanya mnajua standing order hayo huwa hatuyasikii wakati mna haha na bahasha mtaani 😂 nawaza tu mwenyewe kwa maandishi
 
So hata ukiitwa kuripoti usiache kwanza kazi hapo ulipojishikiza, si ndiyo?
 
We nimecheka unaongelea halmashauri ofisi za kizamani, wale Tena kwa uchoyo, mgeni siku ya kwanza anafika anaelekezwa kununua vitafunwa, kukaa kidogo sukari hakuna, hakuna ukarimu Wala nini., Ukiona migari nje utazani Kuna neema kweli ingia ndani mgeni.
 
Kuna dada mmoja tulikuwa nae hapa ofisin alikuwa anajitolea mungu si Athuman kalamba asali kupitia ajira portal kwenye mamlaka fulani ya maji nchini, ameenda kuripoti nae kaambiwa arudi kwa kitaa wafanye kwanza uhakiki, mimi nafikir ndio utaratibu wa sasa taasisi nyingi ufanya ivyo.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Ukisoma Barua Ile ya kupangiwa Kituo inamtaka mwajiri afanye uhakiki Wa vyeti vyako Kwanza ndipo akupokee rasmi. Nadhani hicho ndo kinakula muda
Kwani hao utumishi hadi wanakupa ajira hawakuhakiki hivyo vyeti?tuache ukiritimba aisee.....waliopewa dhamana ya kisaili watu waaminike na taratibu zifanyike punde tu unavyopewa barua mtu aingizwe kwenye mfumo wa payroll.
 
Mwambie mdogo wako aachane na hio nafasi, aludi zake nyumbani tu.

kupata kazi ni mbinde, kuripoti kazini nako unaambiwa subilia baada ya wiki mbili.
 

Kama mwajiri anakupa ruhusa ya kurudi nyumbani hadi atakapokuita, hapo ni nani anapaswa ampe mwenzie barua.

Nachoelewa ukishapewa barua ya kwenda kuripoti, ukafika kituo chako cha kazi kuondoka ni kwa ruhusa tu tena ukutane na mwajiri aliye fair atakupa labda siku 3 hadi 7.

Sasa hii ya kuambiwa nenda nyumbani tutakupigia simu ndo utaratibu gani.

Serikalini hakuna namna hiyo ya utendaji. Ni mwendo wa barua. Kijana asipoitwa tena itakuaje?
Ofisi za umma haziendeshwi kihuni hivyo.
 
Ni kweli kwa sasa huo ndio utaratibu, lakini je ni utaratibu mzuri? je ni utaratibu wa haki?. Huu utaratibu umezingatia kuepusha tatizo moja la mwajiriwa kukaa muda mrefu kazini kabla ya kuingizwa kwenye pay roll ya serikali ambapo pia ilikuwa inaleta usumbufu sana. Lakini huu utaratibu haukuzingatia matatizo anayoyapata mwajiriwa kambiwa arudi nyumbani hadi apigiwe simu wakati nyumbani ni mbali na pesa za kurudi nyumbani hana, na pesa za kujikimu hana!!

Wangefanya hivi: Wanapomwabia arudi nyumbani hadi atakapoitwa kwa simu, wamwezeshe kurudi nyumbani kwa maana ya kumrudishia nauli aliyotumia kuripoti na kumpa nauli ya kurudi nyumbani!! Hapo wataeleweka!!
 
kwa ofisi ambazo mahitaji ya watumishi ni ya haraka na zina fedha unaweza pewa posho ya kujikimu au ikibidi unapewa advance salary ila kwa ofisi zinazotegemea pesa toka hazina hizi mara nyingi hufanya kama nilisema pale juu.

wanakuita mapema ili kusaini job offer pamoja na fomu mbalimbali za maelezo binafsi ya mwajiriwa mpya kwa maana kuna waajiriwa wapya wanaitwa kuripoti lakini hawaendi, cha msingi ni kuvumilia tu maana ajira zenyewe za shida.
 
Kwa kweli
Mtu unakaa Zaidi Ya mwezi unasubiri Simu mpaka unapata wasiwasi
 
Yamenikuta mm hapa Nina mwezi na simu sijapigiwa
 
Kwahiyo hapa mkuu siku ukiitwa hamna pesa yoyote ya kujikimu utakayopewa?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…