Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Msijali mambo yatakua poa. Kikubwa mtangulize Mungu mbele.

Tangazo 5.JPG
 
Kama ni hivyo basi apewe nauli aliyotumia kuripoti kwa mujibu wa maagizo aliyopewa kwenye barua, kisha apewe nauli ya kurudi nyumbani akisubiri kuitwa tena!!
Wakati unaomba kazi wangekwambia kama utahitaji kulipiwa nauli na serikali ya kuja kuripoti na kurudi basi usiombe kazi nawaza tu ungeomba au usinge omba hiyo kazi.
 
Wakati unaomba kazi wangekwambia kama utahitaji kulipiwa nauli na serikali ya kuja kuripoti na kurudi basi usiombe kazi nawaza tu ungeomba au usinge omba hiyo kazi.
Hayo ni mawazo mfu!! Utumishi wa umma unaongozwa Government standing orders na siyo matakwa ya mtu!! Haki za waajiriwa wapya lazima zilindwe! Kulipiwa nauli mwajiriwa anaporipoti kazini ni takwa la kisheria!!
 
Huwezi kuamini!! Vijana wanapambana sana na kujipa moyo kuwa kwa kuwa ni wanaume acha wapambane!! Kwa wale vijana wa kike wengine wao hujikuta wamelazimika kujirahisisha ili kupata ufadhili wa malazi na chakula wakati wanangoja hizo simu za miungu watu!! Wale wakiume wengine hushindia mkate wa buku na maji ya viroba na kulala popote hata kwenye stendi ya bus!! Ni mbaya sana na sijui kama huu utaratibu una baraka zote za serikali!! Wanaoga kwenye vibanda vya vyoo za kulipia!
Wewe fikiria kwa mfano yule aliyekuwa anabangaiza Dar na kisha kupata ajira Tabora!! anakopa nauli kwa ahadi kuwa akipata posho ya kujikimu atarudisha bpesa za watu!! Halafu anaripoti tabora na kuambiwa asubiri hadi apigiwe simu!! Nauli ya kurudi hana!! Hizo pesa kidogo alizobakiza anaona ni afadhali azitumie kwa kula chochote ili mradi aendelee kuwa hai na hajali analala wapi!! sawa wanavumilia hasa kwa kuwa wanajua mateso yanaelekea mwisho. Lakini je ni lazima watendewe hivyo? Haiwezekani kuwa na utaratibu ulio rafiki?
Si awasiliane na mamlaka husika. Humu jf raia wanakukebehi wanalala mbele...a follow complaints channel sahihi ahudumiwe
 
nikujibu kwa uzoefu,

1. mara nyingi hizi ofisi hazina pesa kwa ajili posho ya kujikimu ambayo anapaswa apewe muajiriwa mpya.

2. na ndiyo maana ukishajaza fomu ya maelezo yako binafsi wanakuambia utapigiwa simu lengo lao ni kuwa ukishaingia kwenye mfumo wa mishahara hazina ndiyo unaitwa rasmi ukaanze kazi.
 
Hayo ni mawazo mfu!! Utumishi wa umma unaongozwa Government standing orders na siyo matakwa ya mtu!! Haki za waajiriwa wapya lazima zilindwe! Kulipiwa nauli mwajiriwa anaporipoti kazini ni takwa la kisheria!!
Mkisha pataga ajira ndio huwa mnaanza kujifanya mnajua standing order hayo huwa hatuyasikii wakati mna haha na bahasha mtaani 😂 nawaza tu mwenyewe kwa maandishi
 
So hata ukiitwa kuripoti usiache kwanza kazi hapo ulipojishikiza, si ndiyo?
 
We nimecheka unaongelea halmashauri ofisi za kizamani, wale Tena kwa uchoyo, mgeni siku ya kwanza anafika anaelekezwa kununua vitafunwa, kukaa kidogo sukari hakuna, hakuna ukarimu Wala nini., Ukiona migari nje utazani Kuna neema kweli ingia ndani mgeni.
 
Kuna dada mmoja tulikuwa nae hapa ofisin alikuwa anajitolea mungu si Athuman kalamba asali kupitia ajira portal kwenye mamlaka fulani ya maji nchini, ameenda kuripoti nae kaambiwa arudi kwa kitaa wafanye kwanza uhakiki, mimi nafikir ndio utaratibu wa sasa taasisi nyingi ufanya ivyo.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
Ukisoma Barua Ile ya kupangiwa Kituo inamtaka mwajiri afanye uhakiki Wa vyeti vyako Kwanza ndipo akupokee rasmi. Nadhani hicho ndo kinakula muda
Kwani hao utumishi hadi wanakupa ajira hawakuhakiki hivyo vyeti?tuache ukiritimba aisee.....waliopewa dhamana ya kisaili watu waaminike na taratibu zifanyike punde tu unavyopewa barua mtu aingizwe kwenye mfumo wa payroll.
 
Mwambie mdogo wako aachane na hio nafasi, aludi zake nyumbani tu.

kupata kazi ni mbinde, kuripoti kazini nako unaambiwa subilia baada ya wiki mbili.
 
[emoji23][emoji28] sasa mbona unajichanganya mwenyew tena... Unapewa vipi barua wakat tayar ulipata barua ya ajira... Halafu sasa ukitaka twende kwa utaratibu basi yeye ndiye alipaswa kuandika barua ya kukiri kufika kituoni na kuruhusiwa kurudi nyumban kusubiri taratibu nyingine za kikazi... Vijana msi complicate mambo ya kiserikali hayahitaji papara, by the way hakuna wa kuwazurumu stahiki zenu...
Zamani watu walikua wanaripoti kituoni na wanalipwa stahik za muhimu kama nauli na pesa za mizigo kusafirisha utokapo, tatizo likaja kuonekana wengi hawarudi tena... Anyways all in all kuweni wapole

Kama mwajiri anakupa ruhusa ya kurudi nyumbani hadi atakapokuita, hapo ni nani anapaswa ampe mwenzie barua.

Nachoelewa ukishapewa barua ya kwenda kuripoti, ukafika kituo chako cha kazi kuondoka ni kwa ruhusa tu tena ukutane na mwajiri aliye fair atakupa labda siku 3 hadi 7.

Sasa hii ya kuambiwa nenda nyumbani tutakupigia simu ndo utaratibu gani.

Serikalini hakuna namna hiyo ya utendaji. Ni mwendo wa barua. Kijana asipoitwa tena itakuaje?
Ofisi za umma haziendeshwi kihuni hivyo.
 
nikujibu kwa uzoefu,

1. mara nyingi hizi ofisi hazina pesa kwa ajili posho ya kujikimu ambayo anapaswa apewe muajiriwa mpya.

2. na ndiyo maana ukishajaza fomu ya maelezo yako binafsi wanakuambia utapigiwa simu lengo lao ni kuwa ukishaingia kwenye mfumo wa mishahara hazina ndiyo unaitwa rasmi ukaanze kazi.
Ni kweli kwa sasa huo ndio utaratibu, lakini je ni utaratibu mzuri? je ni utaratibu wa haki?. Huu utaratibu umezingatia kuepusha tatizo moja la mwajiriwa kukaa muda mrefu kazini kabla ya kuingizwa kwenye pay roll ya serikali ambapo pia ilikuwa inaleta usumbufu sana. Lakini huu utaratibu haukuzingatia matatizo anayoyapata mwajiriwa kambiwa arudi nyumbani hadi apigiwe simu wakati nyumbani ni mbali na pesa za kurudi nyumbani hana, na pesa za kujikimu hana!!

Wangefanya hivi: Wanapomwabia arudi nyumbani hadi atakapoitwa kwa simu, wamwezeshe kurudi nyumbani kwa maana ya kumrudishia nauli aliyotumia kuripoti na kumpa nauli ya kurudi nyumbani!! Hapo wataeleweka!!
 
kwa ofisi ambazo mahitaji ya watumishi ni ya haraka na zina fedha unaweza pewa posho ya kujikimu au ikibidi unapewa advance salary ila kwa ofisi zinazotegemea pesa toka hazina hizi mara nyingi hufanya kama nilisema pale juu.

wanakuita mapema ili kusaini job offer pamoja na fomu mbalimbali za maelezo binafsi ya mwajiriwa mpya kwa maana kuna waajiriwa wapya wanaitwa kuripoti lakini hawaendi, cha msingi ni kuvumilia tu maana ajira zenyewe za shida.
 
Hicho ni kisingizio tu!! 1. Vyeti vilivyopandishwa kwenye mfumo vimethibitishwa kisheria na mahakama au wakili. 2. Wakati wa usaili (written interview) wahusika walikagua vyeti halisi kwa kuwatumia watu wenye utaalam wa kuhakiki vyeti na wanakula posho kwa kazi hiyo.
3. Wakati wa usaili wa oral walikagua tena vyeti na kuvihakiki!!
4. Wakati unaporipoti kituoni ulikopangiwa ajira unaenda na vyeti halisi wanavikagua, wanavihakiki na kuchukua nakala yake.
Kwa hiyo vyeti vimehakikiwa mara nne!! Hakuna sababu ya kudai bado wanahakiki tena!! Vinginevyo kabla ya placement kwa kuwa vyeti vipo kwenye mfumo wa ajira basi vitumwe NECTA na kwenye vyuo walikosoma vihakikiwe na zoezi hilo ni jepesi na la haraka sana. Kisha ndio watoe placement!! Watanzania wanatesana kwa visingizio visivyokuwa na sababu!!
Kwa kweli
Mtu unakaa Zaidi Ya mwezi unasubiri Simu mpaka unapata wasiwasi
 
Ukipata placement kitu Cha muhim ni kwenda kuripoti kituo Cha KAZI. Taratbu za vyeti zikiisha inabidi urudi ulikotoka na uendelee kutafta pesa zako had utakapopigiwa simu. Kuna watu hikaa hata mwez mzma na sehm Kisha ndo wanapigiwa simu.

Na huo ndio mfumo ulivo.
Yamenikuta mm hapa Nina mwezi na simu sijapigiwa
 
nikujibu kwa uzoefu,

1. mara nyingi hizi ofisi hazina pesa kwa ajili posho ya kujikimu ambayo anapaswa apewe muajiriwa mpya.

2. na ndiyo maana ukishajaza fomu ya maelezo yako binafsi wanakuambia utapigiwa simu lengo lao ni kuwa ukishaingia kwenye mfumo wa mishahara hazina ndiyo unaitwa rasmi ukaanze kazi.
Kwahiyo hapa mkuu siku ukiitwa hamna pesa yoyote ya kujikimu utakayopewa?.
 
Back
Top Bottom