Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Kero ya kuripoti kazini baada ya kupangiwa ajira na sekretarieti ya ajira, halafu unaambiwa urudi nyumbani mpaka upigiwe simu kuitwa!

Hata

niliporipoti na barua ya kupangiwa kituo ilikuwa ni rasmi na ni lazima igharimiwe!! Ni kwa kigezo kipi unasema sijaripoti rasmi wakati nilikuwa barua rasmi inayonitaka niripoti ndani ya siku 14 vunginevyo nafasi yangu atapewa mwingine? Hivi haiwezekani kuwa na utaratibu rafiki usiokuwa na usumbufu?
Kijana ukimaliza probation yako ya miezi isiyopungua 9 ndio utaelewa kiasi fulani taratibu za kiserikali...
Nimekupa hints muhimu za kukuongoza otherwise fanya unavyotaka wewe kwa experience ya kukaa home na story za vijiweni...
 
Mtu ambaye yupo pwani mkuranga na anateseka aje nyumbani kwangu akae Hadi atakapo itwa kazini.Namaanisha mtu ambaye ametokea mkoani sio aliopo Dar .Utakula utalala pazuri na ukihitaji kwenda mjini kama nauli ipo ntakupa mara Moja Moja kama unaenda mjini.Mimi ni Me na Niko nafamilia yangu.Sijali ke au Me, yeyote anayesumbuka.Hatutahitaji malipo yoyote kutoka kwako.Karibu sana
Hapo Kwa mdada unataka uanze ugomvi na mkeo
 
Ajira zenyewe za Halmashauri 😂😅 mnakuja kutupigia kelele JF.. mnaelekezwa mnajifanya wajuaji haya kalaleni getini basi muone kama mtafanyiwa mnavyotaka nyie... Serikal ina taratibu zake hawawez kufanya kazi na kukupa stahiki za kiutumishi kwasabab umeenda tu na barua yako... Rudi kijijini kamalizie kupalilia alizet
 
Ukisoma Barua Ile ya kupangiwa Kituo inamtaka mwajiri afanye uhakiki Wa vyeti vyako Kwanza ndipo akupokee rasmi. Nadhani hicho ndo kinakula muda

Huu ni upuuzi pia linapokuja suala la uhakiki wa vyeti.

Kwa nini utumishi wanahamisha majukumu. Wao ndio wanaajiri, na michakato yote wasailiwa wanaaenda na vyeti halisi kila hatua ya usaili.

Inamaana gani tena kuendelea kudai vyeti halisi siku ya kwenda kuripoti.

Tujifunze namna ya kuhakiki taarifa za wajiriwa bila kuleta usumbufu.

Tuna watu wenye elimu lakini hawajaelimika kutumia elimu zao kurahisisha changamoto/taratibu.
 
Kwa taarifa yako mimi ni mtumishi umma mstaafu!! Ninaandika hapa kwa maufaa mapana ya watanzania wanaonyanyasika kwenye ajira mpya!! Nimeandika kwa kirefu ili kutoa picha halisi ya tatizo. Shida ni kwamba kuna vwatu ni wavivu hata kusoma nusu ukurasa wanaona ni taabu!! Ila kitu kizuri ni kwamba wewe ni mvivu pekee kati ya wasomaji karibu kama 40 hivi!!
Ndugu yangu Mstaafu;

1. Mimi sijapingana na wewe. Uko sawa kabisa na hicho inachofanya serikali ni kuonesha kuwa hawakujiandaa vyema. Na ishu hapo huwa ni fedha tu, hakuna kingine. Yaani unaajiri mtu, lakini fedha zinakuwa bado hazipo!!

2. Ishu siyo uvivu wa kusoma. Nimekusoma na kukielewa vyema kabisa

3. Mwishoni nilikushauri tu kuwa, weka andiko lako kwenye paragraphs.

Au nimefanya vibaya kukushauri hivyo ndugu Mstaafu?
 
Inawezekanaje watu wapange utaratibu ambao siyo rafiki kwa waajiriwa wapya? Iko hivi: Ukipangiwa ajira na sekretarieti ya ajira kwa maana ya kufaulu usaili, unapewa barua ya kuripoti kazini ndani ya siku 14 vinginevyo nafasi yako atapewa mwingine! Hii inmfanya mwajiriwa atafute nauli hata kwa kukopa toka huko aliko na kusafiri hadi kituo alichopangwa. Akifika huko wanakagua vyeti vyake halisi, na kujaza taarifa zake binafsi kisha huambiwa RUDI NYUMBANI NA TUKIKAMILISHA TARATIBU ZA AJIRA TUTAKUITA KWA SIMU!! Hapo wameshamaliza na unatoka ofisini bila hata senti moja! Hawajali utalala wapi na utakula wapi na usalama wako ni upi! na utasafiri vipi na utarudi tena vipi!! Niliposikia kwa mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa amepangiwa halmashauri moja huko tabora sikuamini kuwa huo ndio utaratibu!! Nilifikiri ni roho mbaya tu ya wahusika huko halmashauri ya tabora!! Juzi juzi kuna dogo alipata nafasi katika moja ya manispaa za Dar. Naye aliporipoti alipokelewa na kukaguluiwa vyeti vyake na kujaza fomu za personal particulars na kuambiwa arudi hadi atakapopigiwa simu! Ni wiki nimepita sasa na bado hajapigiwa simu na anajibanza tu kwa watun na hajui hadi lini!! Huu utaratibu una usumbufu sana!! Ninachofahamu watu huitwa wakati serikali imeshafanya maandalizi tayari ya kuwapokea na kuwahudumia!! Yaani kijana amesota na interview kibao kwa gharama kubwa sana ya nauli, malazi na chakula, sasa ameitwa kwenye ajira bado anasoteshwa! Niwaulize nyie mnaowafanyia hivyo wenzenu mnajua masaibu wanayopambana nayo wanaposubiria? Wengine wanalala kwenye vituo vya mabasi kwa kukosa pesa za gesti na nauli ya kurudi tena nyumbani hawana! Tafadhali angalau siku wanaporipoti wapeni zile posho za kujikimu zilizopo kisheria ili ziwalinde wanaposubiria!
Hilo kokoro linaloitwa serikali linakera sana . Hapo unatakiwa ulipowe nauli ya kwenda na kurudi na pesa ya kulala mpaka zoezi likamilike. Wewe na wategemezi wako Na pesa ya ya kusafirishIa mizigo yako
Muone hr au mkuu wa idara acha kulalamika jf
Adui mkubwa wa mtz ni uwoga
 
Inawezekanaje watu wapange utaratibu ambao siyo rafiki kwa waajiriwa wapya? Iko hivi: Ukipangiwa ajira na sekretarieti ya ajira kwa maana ya kufaulu usaili, unapewa barua ya kuripoti kazini ndani ya siku 14 vinginevyo nafasi yako atapewa mwingine! Hii inmfanya mwajiriwa atafute nauli hata kwa kukopa toka huko aliko na kusafiri hadi kituo alichopangwa. Akifika huko wanakagua vyeti vyake halisi, na kujaza taarifa zake binafsi kisha huambiwa RUDI NYUMBANI NA TUKIKAMILISHA TARATIBU ZA AJIRA TUTAKUITA KWA SIMU!! Hapo wameshamaliza na unatoka ofisini bila hata senti moja! Hawajali utalala wapi na utakula wapi na usalama wako ni upi! na utasafiri vipi na utarudi tena vipi!! Niliposikia kwa mara ya kwanza kwa mtu aliyekuwa amepangiwa halmashauri moja huko tabora sikuamini kuwa huo ndio utaratibu!! Nilifikiri ni roho mbaya tu ya wahusika huko halmashauri ya tabora!! Juzi juzi kuna dogo alipata nafasi katika moja ya manispaa za Dar. Naye aliporipoti alipokelewa na kukaguluiwa vyeti vyake na kujaza fomu za personal particulars na kuambiwa arudi hadi atakapopigiwa simu! Ni wiki nimepita sasa na bado hajapigiwa simu na anajibanza tu kwa watun na hajui hadi lini!! Huu utaratibu una usumbufu sana!! Ninachofahamu watu huitwa wakati serikali imeshafanya maandalizi tayari ya kuwapokea na kuwahudumia!! Yaani kijana amesota na interview kibao kwa gharama kubwa sana ya nauli, malazi na chakula, sasa ameitwa kwenye ajira bado anasoteshwa! Niwaulize nyie mnaowafanyia hivyo wenzenu mnajua masaibu wanayopambana nayo wanaposubiria? Wengine wanalala kwenye vituo vya mabasi kwa kukosa pesa za gesti na nauli ya kurudi tena nyumbani hawana! Tafadhali angalau siku wanaporipoti wapeni zile posho za kujikimu zilizopo kisheria ili ziwalinde wanaposubiria!
Mimi nina mfano wa vijana wawili.
Waliitwa kazini na kurudi.
Nlipongea nao kila mmoja anasema aliambiwa taratibu za mshahara zitachelewa hivyo either ajaze fomu ya ruhusa kurudi mpk atakapopigiwa au aendelee na kazi huku akisubiri taratibu za mshahara.
Mmoja aliitwa Baada ya miezi miwili, mwingine Baada ya km wiki tano na wote waliingiziwa mishahara yao yote walipofika tu
 
Hicho ni kisingizio tu!! 1. Vyeti vilivyopandishwa kwenye mfumo vimethibitishwa kisheria na mahakama au wakili. 2. Wakati wa usaili (written interview) wahusika walikagua vyeti halisi kwa kuwatumia watu wenye utaalam wa kuhakiki vyeti na wanakula posho kwa kazi hiyo.
3. Wakati wa usaili wa oral walikagua tena vyeti na kuvihakiki!!
4. Wakati unaporipoti kituoni ulikopangiwa ajira unaenda na vyeti halisi wanavikagua, wanavihakiki na kuchukua nakala yake.
Kwa hiyo vyeti vimehakikiwa mara nne!! Hakuna sababu ya kudai bado wanahakiki tena!! Vinginevyo kabla ya placement kwa kuwa vyeti vipo kwenye mfumo wa ajira basi vitumwe NECTA na kwenye vyuo walikosoma vihakikiwe na zoezi hilo ni jepesi na la haraka sana. Kisha ndio watoe placement!! Watanzania wanatesana kwa visingizio visivyokuwa na sababu!!
Hii nchi bado kuna ujinga ujinga mwingi sana usio na sababu.
 
Naomba nijibu kama ifuatavyo....unakuwa bado hujaingizwa kwenye mfumo, na mpaka uingizwe kwenye mfumo anaweza kuchukua mwezi au ndani ya miezi miwili ili upate mshahara wako, ili upate mshahara wako inabidi utumishi wa approve taarifa zako, kwa kuzikagua kiundani ili tusipate udanganyifu......kwa kuwa hakuna bajeti Yako ya kujikimu kwa mda ule,ndio maana tunakwambia kuwa kakae kwanza nyumbani mpaka tukupigie simu....jamani sio kwa ubaya,maana hakuna wa kukulisha hapa mjini.....kama hamuamini kawaulize walimu wanavyopata ajira,wanakaa zaidi ya mwezi ndio wanaingiziwa mshahara wao..muda wote huwa wanahudumiw na wakuu wa shule mpaka wanapopata mishahara Yao kwa mara ya kwanza.....alisikika HR mmoja wa michango.

Hii ni shida kubwa sana. Hebu tazama mfumo wa uombaji ajira kwa sasa ulivyo.

Hii inahitaji hata siku 3 kuhakiki taarifa za mwajirirwa.

Tunashida kubwa sana kama taifa.

Binafsi nachukia sana kushindwa kutumia teknolojia tena katika taasisi zetu wenyewe.

Necta, vyuo vya elimu ya juu, Nida hizi zote ni taasis za serikali.
Facts findings inakuchukuaje miezi.

Elimu zetu zitusaidie kufanya mambo kwa wepesi na kwa usahihi.
 
Kijana ukimaliza probation yako ya miezi isiyopungua 9 ndio utaelewa kiasi fulani taratibu za kiserikali...
Nimekupa hints muhimu za kukuongoza otherwise fanya unavyotaka wewe kwa experience ya kukaa home na story za vijiweni...
Taratibu za serikali nazijua sana!! Mimi ni mumishi wa umma mstaafu!! Niliajiriwa katika utumishi wa umma mwaka 1986 baada ya kuhitimu chuo kikuu cha Dar, na nimestaafu mwaka 2019!! Kinachofanyika sio taratibu za utumishi wa umma bali uhuni. Taratibu za utumishi wa umma zinaongozwa na Government standing orders toleo la 2009 na marekabisho yake ya mwaka 2011!! Huo utaratibu wa mtu kuripoti kazini kwa wito rasmi halafu unarudishwa nyumbani bila kuhudumiwa kwa lolote ni uhuni wa watu!! Naomba unukuu hapa waraka wowote rasmi wa serikali unaoelekeza hivyo!!
 
Mkuu hapana,Mimi nimelsaidia watu wengi sana nikiwa na mke wangu so worry not.Anayepata shida wa mkoani siyo wa mjini
Basi wako ni mwelewa Kuna mtu alikuwa wakusaidia mkewe alijua ni mdada anaenda kuharibu uko sasa sijui ndio uchawi na roho mbaya
 
Nyie vijana hamjitambui muwe mnauliza ili mpate kujua mambo, ukienda kuripoti kituo cha kazi ukiambiwa rudi nyumban tena inabidi ushukuru umepewa muda wa kujiandaa vzuri kwa maisha mapya... Hapo maana yake umepewa siku sio chini ya 14 kurudi kujiandaa... Hapo maana yake rudi kavute pumzi wakat wanajiandaa kukuingiza ktk mfumo wa Payroll... Hapo maana yake hawajataka ubaki kazini wakat taratibu za stahiki zako kama mtumish hazijakamilika, kumbuka mifumo ya serikal inafanya kazi kwa mawasiliano na documents sahihi... As long as umetoa namba zako za cm na email sahihi tuliza komwe lako nyumban utaitwa... Halafu pia ukiripoti kituoni na kuambiwa rudi utapigiwa cm ni vizuri uombe namba ya wahusika acheni uoga wa kijinga... Zamani watu walikua wanaripoti kituoni wanaanza kazi then mishahara inachelewa hata miezi 3 unaishi vipi..? Ndiyo maana sikuhiz wanachukua taarifa zako zote wakishakamilisha taratibu ndio unaitwa kazini... Serikal sio private sector... All in all mkipata kazi fanyeni kazi kwa bidii weledi uaminifu na mkubali kujifunza kazi kwa waliotangulia na kamwe msiige tabia mbaya mtakazozikuta kwasabab kilamtu kaingia kazini na anafanya kazi kwa malengo take binafsi...

Ukisharipoti ni ajira imekamilika. Hizo ni taratibu tu.
Ilipaswa kumpa hata barua kuwa ameripoti na sasa wanakamilisha taratibu nyingine arudi tarehe fulani.
 
Miongozo na taratibu zozote zinazopangwa ambazo hazizingatii Government standing orders toleo la 2009 na ,marekebisho yake ya mwaka 2011 ni batili!!
 
Serikali irekebishwe huu upumba.vu na usumbufu ndio maana umaskini hauishi hii kitu ya taratibu ingeweza kufanyika na Kila jambo kukamilika ndio mtu aitwe Sasa huu mlolongo mrefu wa Nini in the name eti taratibu na mtu anajiona yuko kazini huku hawezi ku solve changamoto mapema.
Pia ka watu vyeti vimetolewa na vyuo na vimehakikiwa Kwa mwanasheria huo usumbufu Huwa wanini Ina maana hamna coordination.
Ni huko serikalini jambo la siku moja waweza zungushwa miezi miwili kisingizio mara kiwe mfumo uko chini mara kile, ni mdada Sasa watu waanze kulipwa kulingana na huduma wanafanya uone ka itachukua mda
 
Jamaa unajua kulalamika unaandika gazette wewe unachembe chembe ya umbea
 
Unapofikiria una Kila kitu kuwa makini sana unaweza kupoteza Kila kitu ukahitaji msaada Kwa mtu ambaye hakuwa na kitu sasa hivi anacho na yeye.
 
Mimi nina mfano wa vijana wawili.
Waliitwa kazini na kurudi.
Nlipongea nao kila mmoja anasema aliambiwa taratibu za mshahara zitachelewa hivyo either ajaze fomu ya ruhusa kurudi mpk atakapopigiwa au aendelee na kazi huku akisubiri taratibu za mshahara.
Mmoja aliitwa Baada ya miezi miwili, mwingine Baada ya km wiki tano na wote waliingiziwa mishahara yao yote walipofika tu
Ingetakiwa akae hotelini siku zote hzo akisubiria
 
Tangazo la ajira likitoka maana yake ni kuwa: 1. Nafasi hizo ziko wazi. 2. Kibali cha ajira kimeshatolewa. 3. Pesa za kushughulikia mchakato huo wa kujaza nafasi hizo zipo. 4. Pesa za mishahara na malipo mengine yanayoambatana na ajira mpya zipo. Kama ndivyo kwa nini mchakato uchukuwe muda mrefu sana kiasi cha zaidi ya miezi sita hadi mwaka mzima?? Lazima kuna tatizo mahali fulani!!
 
Back
Top Bottom