Kero ya Walimu msingi kudai michango mingi; ni makubaliano ya kikao feki cha wazazi feki

Kero ya Walimu msingi kudai michango mingi; ni makubaliano ya kikao feki cha wazazi feki

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Shule nyingi za msingi za serikali siku hizi zimejaa michango mingi sana ambayo inaleta matabaka kwa watoto!

Walimu wanachangisha hela ya mitihani kila siku 1000.
Ndoo mpya kila term,
Fagio jipya kila mwezi,

Hela ya safari (tour) kwa mgongo wa hiari huku nyuma wanawapiga mkwara watoto kwenda!

Vitabu vidogodogo wanalazimishwa kununua n.k

Hii tabia ukihoji wanasema ni makubaliano ya kikao cha wazazi lakini ajabu kila mzazi analalamika! Sasa hiko kikao huwa wanakalia wapi?

Mambo haya yameshamili sana na maafisa elimu wapo, wakurugenzi wapo, DC na RC wapo, mawaziri wapo, tamisemi wapo, Yaani ni kero mtupu lakini kiiimyaaa!

Walimu wanachukua mikopo halafu wanarudi kulalamika mshahara hautoshi wanasahau mikopo ya anasa ndo tatizo!

Ugumu wa maisha wao kutwa kuchangisha michango isiyo na kichwa wala miguu kila siku!
Kwanza tuition za kulipia za nini kwenye shule za serikali?
 
Dah! Inaumiza sana darasa la saba kila siku 400 afu alkhamis 1500 noma sana
 
Wapeni support walimu wapate chochote kupitia hyo michango , hawa watu ni wa mhimu na wanapitia wakat mgumu kuliko wafanyakazi wote.... Hawana semina hawana marupu tupu yyte , mwisho wa sku wanakopa mpak Kwa boda
 
Shule nyingi za msingi za serikali siku hizi zimejaa mijango mingi sana ambayo inaleta matabaka kwa watoto!
Walimu wanachangisha hela ya mitihani kila siku 1000.
Ndoo mpya kila term,
Fagio jipya kila mwezi,

Hela ya tour kwa mgongo wa hiari huku nyuma wanawapiga mkwara watoto!
Vitabu vidogodogo wanalazimishwa kununua n.k

Hii tabia ukihoji wanasema ni makubaliano ya kikao cha wazazi lakini ajabu kila mzazi analalamika! Sasa hiko kikao huwa wanakalia wapi?

Mambo haya yameshamili afisa elimu wapo, wakurugenzi wapo, DC na RC wapo, mawaziri wapo, tamisemi wapo, Yaani ni kero mtupu lakini kiiimyaaa!
Uko wilaya gani mkuu, penye hilo tatizo, kurahisisha ufuatiliaji.
 
Wapeni support walimu wapate chochote kupitia hyo michango , hawa watu ni wa mhimu na wanapitia wakat mgumu kuliko wafanyakazi wote.... Hawana semina hawana marupu tupu yyte , mwisho wa sku wanakopa mpak Kwa boda
Bora ada ya Mara moja kuliko kila siku hela wazazi wanaumia
 
Shule nyingi za msingi za serikali siku hizi zimejaa michango mingi sana ambayo inaleta matabaka kwa watoto!

Walimu wanachangisha hela ya mitihani kila siku 1000.
Ndoo mpya kila term,
Fagio jipya kila mwezi,

Hela ya safari (tour) kwa mgongo wa hiari huku nyuma wanawapiga mkwara watoto kwenda!

Vitabu vidogodogo wanalazimishwa kununua n.k

Hii tabia ukihoji wanasema ni makubaliano ya kikao cha wazazi lakini ajabu kila mzazi analalamika! Sasa hiko kikao huwa wanakalia wapi?

Mambo haya yameshamili sana na maafisa elimu wapo, wakurugenzi wapo, DC na RC wapo, mawaziri wapo, tamisemi wapo, Yaani ni kero mtupu lakini kiiimyaaa!

Walimu wanachukua mikopo halafu wanarudi kulalamika mshahara hautoshi wanasahau mikopo ya anasa ndo tatizo!

Ugumu wa maisha wao kutwa kuchangisha michango isiyo na kichwa wala miguu kila siku!
Kwanza tuition za kulipia za nini kwenye shule za serikali?
Hilo nilisikia juzi Waziri mkuu akilikemea shule za sekondari za umma kuchapa joining instruction zenye vifaa vingi sana zaidi ya 200k!

Mkuu nimefurahishwa na kichwa cha habari, lakini kwenye 'content' "umemumunya" maneno.

Kifupi michango ni ya gharama kubwa kuliko ada.

Halafu "vikao vya wazazi" nilishavihudhuria vina mamluki vipandikizi waliojipanga huwashindi hoja.

Hakuna cha wazazi hapo ni wazazi feki kama ulivyoandika kichwa chako cha habari.

Utashangaa hoja za rejareja za kijinga jinga zinazotolewa pale zinaungwa mkono 100%, wanakuwa wanejipanga haswa kwa manufaa binafsi.

Hakuna anayehoji matumizi ya hela ya shule inayoletwa mgao na serikali kwa elimu bila malipo na mchanganuo wake kuonesha zinafanya kazi gani.

Rim za karatasi pamoja na vikorombweso kibao ukiunga gharama zake vinazidi ada.

Marufuku ya michango iliyotolewa na serikali ya awamu ya 5 ingeliendelezwa kukomesha umumiani huu ulioibuka tena kama kweli serikali imeamua kulivalia njuga suala la kubeba gharama za kusomesha watoto.

"Mwenye kuguswa ama mkereketwa" apeleke mchango wake kwa Mkurugenzi kama ilivyokwisha kuagizwa, wanashindwa nini?

Hatukatai harambee za ujenzi wa madarasa kutokana na ongezeko la watoto lisilokuwa na kikomo, lakini double standard ya gharama zinazobebwa na serikali halafu wazazi wanageukiwa kuhamasishwa kuchangia gharama hizo hizo, tunasema hapana.
 
Back
Top Bottom