Kero ya Walimu msingi kudai michango mingi; ni makubaliano ya kikao feki cha wazazi feki

Umefafanua vyema sana
 
Well said mkuu,,
Hayo mambo yapo Sana kwenye hizi shule zetu za serikali.

Halafu ukiuliza wanasema wazazi walikaa na kupanga yote hayo.

Kumbe wazazi fake na vikao fake ..
 
1000 kila siku boss? Sema shule gan hiyo watu waifatilie.
 
Labda ni michango yenye baraka
Hakuna baraka zozote kwa wazazi,

Ktk Kila shule kunakuwa na kigenge Cha wahuni ambacho kinajiita wawakilishi wazazi,
Hao ndy wanakula na walimu,

Wao ndy hukaa na walimu na kuamua maamuzi yoyote yenye maslahi nao,
Kwa kisingizio kwamba wao ndy wawakilishi wa wazazi wa wanafunzi wote.

Kumbe janja janja yao ya upigaji.
 
Na sio shule za msingi pekee bali ni shule zote za serikali zina mambo hayo ya michango ya hovyo hovyo.
 

Wewe huwa unaenda kwenye vikao cha shule?
Mara nyingi wengi huwa hawaendi halafu wanalalamikia maamuzi ya walioenda
Dawa ni kwenda na kutoa maoni yako au kukataa hiyo michango kabla ya utekelezwaji wa maazimio ya vikao
 

Ndio uwe unaenda kwenye vikao ili upingie huko
 
Sasa unataka walimu waishije?
 
Wapeni support walimu wapate chochote kupitia hyo michango , hawa watu ni wa mhimu na wanapitia wakat mgumu kuliko wafanyakazi wote.... Hawana semina hawana marupu tupu yyte , mwisho wa sku wanakopa mpak Kwa boda
Sasa huyo unayemtaka atoe support yeye anapewa na nani?.

Yeye Mwalimu ana mshahara mwisho wa uhakika kila Mwezi anataka support ya Saidia Fundi asiye na uhakika wa kazi kwa siku zote 30 za mwezi.
 
Yaani fagio na ndoo ndio waalimu wanapiga, kwa Nini msishauri hao watoto wenu wakifanya usafi warudi na ndoo na mifagio nyumbani kila siku ili kuepuka waalimu kupiga? Na hio hela ya copy za mitihani, mzazi mmoja mwenye photocopy ajitolee wenzie wamchangie awe anadurufu yeye hio mitihani yote
 
Toeni hela, acheni kulalamika lalamika kama watoto.
 
Yaani unataka mwanao apewe kila kitu na serikali? Acheni uvivu wazazi mfanye kazi msapiti kidogo
 
Well said mkuu,,
Hayo mambo yapo Sana kwenye hizi shule zetu za serikali.

Halafu ukiuliza wanasema wazazi walikaa na kupanga yote hayo.

Kumbe wazazi fake na vikao fake ..
Wazazi wa mchongo
 
Yaani unataka mwanao apewe kila kitu na serikali? Acheni uvivu wazazi mfanye kazi msapiti kidogo
Basi Ijulikane ya jumla ya mwaka mzima tujue moja siyo kila siku kidogo kidogo ni kero
 
Basi Ijulikane ya jumla ya mwaka mzima tujue moja siyo kila siku kidogo kidogo ni kero
Wakipiga hesabu ya mwaka itashtua watu. Kwa hiyo wanaona bora waende na hesabu ya wiki wiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…